Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,707
- 1,729
Nimekuwa nikibahatika kuona mijadala hasa kwenye televisions za Star(Startv) na ITV kuhusiana na mambo mbalimbali.
Kitu nilichogundua mpaka sasa ni kuwa kama patakuwa na mada inayohusisha vyama vya siasa mfano pawe na mwakilishi wa CCM, CHADEMA, CUF n.k. basi uongoza mjadala atazidiwa (sijui makusudi au ushabiki) na mmoja wa waalikwa kwa kwenda NJE kabisa na mada husika.
Niliona kwenye Startv wakati Yahya Mohamed akiongoza mjadala uliowahusisha mh Migulu Nchemba (CCM), mh Zito Kabwe (CHADEMA) na Julius Mtatilo (CUF). Wale wa CHADEMA na CUF walijikita HASWA kwenye mada lakini wa CCM yeye aliamua kuingiza ya kwake na kumshambulia Zito na chama chake huku Yahya akiangalia tuu bila ya kumkosoa.
Jana pia nilibahatika kuona mjadala kwenye ITV (Kipima Joto), muongozaji ni mtangazaji mahiri bwana Masako. Kwenye mjadala huo licha ya kuhusisha CCM (mh Ndugai) na CHADEMA (mh Lisu) pia palikuwa na waalikwa wawili toka asasi nyingine. Kama kawaida (hii naamini sasa) mh Ndugai akatoka kwenye mada husika na kuanza kumshambulia Lisu na chama chake bila hata bwana Masako kumkatiza mpaka pale mh Lisu alipoingilia kati.
Sasa kama hakuna nidhamu ya kujadili MADA husika basi pasiwe na ajenda bali iwe kama mkutano tu wa kisiasa.