Brother James
JF-Expert Member
- Feb 21, 2012
- 233
- 172
Mkuu wala usipate taabu sana.Naombeni niulize swali dogo wadau mnaweza kunisaidia....katika kuijaza fomu ya mkopo online ilikuwa inaniambia school name was not found nikaamua kuendelea mbele mpaka nimejaza details zote....lakini pale sehemu ya shule jina halipo bali kuna namba tu na nashindwa jinsi ya kulipata hilo jina ili niliweke.....swali langu je kama nitaipeleka fomu nitakuwa bado sahihi kwa kuwa namba ipo au ni makosa??.....na kama ni makosa nifanyeje ili kufix hili tatizo???
MSAADA PLEAAAASE
Please mleta mada badilisha hiyo title ya topic yako au Moderator wafute kabisa hii topic kwani inaupotoshaji mkubwa sana.
Hakuna mahali popote kwenye hiyo taarifa ya bodi ya mikopo inapoonesha kutoa mkopo Asilimia 100 kwa waombaji wote, sasa mleta mada nani kakutuma kuandika Title yenye kusema ''Bodi ya mikopo kutoa mkopo 100% kwa waombaji wote''
NOTE:
JF sio kijiwe cha uzushi na umbeya, ni home of great thinkers, tuwe makini tunachokiandika.
Naombeni niulize swali dogo wadau mnaweza kunisaidia....katika kuijaza fomu ya mkopo online ilikuwa inaniambia school name was not found nikaamua kuendelea mbele mpaka nimejaza details zote....lakini pale sehemu ya shule jina halipo bali kuna namba tu na nashindwa jinsi ya kulipata hilo jina ili niliweke.....swali langu je kama nitaipeleka fomu nitakuwa bado sahihi kwa kuwa namba ipo au ni makosa??.....na kama ni makosa nifanyeje ili kufix hili tatizo???
MSAADA PLEAAAASE
Mbrazil,
Kwanza kabisa, hukutakiwa kum-support LumumbaDAR kwa ku-like aliposema kuwa title ya thread hii ina makosa; kama ungepata wasaa mzuri wa kufikiri na kutafsiri ile title. Wewe pia kama hukuelewa vizuri waweza kwenda kwenye message yake nime-mjibu vizuri tu just to help you guyz.
Pili, ninataka nikushauri kuhusu hapo ambapo jina la shule halikutokelezea;yawezekana ni human errors tu ambazo umezifanya. Kwanza fanya uthibitishe namba ya shule husika kwa kwenda website ya NECTA ambako shule zote na namba zake zinapatikana then utapata jibu kama umekosea namba au shule haitambuliki na NECTA. Ninachofahamu, shule zote zilizosajiliwa na serikali zinatambulika na NECTA na huonekana katika website yao kwa urahisi.
Sipendi sana kukushauri kuwasiliana na HESLB kwa haraka haraka kwa sababu HESLB si watu wepesi sana kupokea simu za applicants wanapopiga na pia hawana ushauri mzuri saana kwa applicants zaidi zaidi huonyesha jazba zao na kuwadharau (indirectly) applicants kuwa ni ignorants ktk matumizi ya online applications. Ikishindikana sana basi usisite kuwatafuta HESLB.
Fungua kitabu cha TCU 2013/2014 uone possible loans zilivyo sio kuja na hesabu zako za ajab alaf unapotosha umma kwa kutumia jukwaa letu la watu makin
Kwa mfano UDSM 100% itatolewa kwa watu wa sayansi na mainjinia
Kwa hivi mikopo ni kwa ajili ya waliosoma shule za serikali au ni aje? Msaada wakuu
Wahusika wanalalamika hasa Arusha kua MTANDaO(website yao»»olas.heslb.go.tz) inasumbua xana xaxa itAkuaje apo afu kuna mahala wanajaziwa io FORM yA mkopo kwa Tsh 39000/= je ni halali???
Wahusika wanalalamika hasa Arusha kua MTANDaO(website yao»»olas.heslb.go.tz) inasumbua xana xaxa itAkuaje apo afu kuna mahala wanajaziwa io FORM yA mkopo kwa Tsh 39000/= je ni halali???
Asante sana mkuuPAKAWA,
Ninachofahamu mimi ni kuwa Mikopo hutolewa kwa watanzania woote wenye sifa za jumla (yaani zilizo ainishwa na TCU) na zile zilizowekwa kulingana na chuo na fani husika. Pamoja na sifa hizo mkopo hutolewa tofauti tofauti in terms of percentages kulingana na courses zilivyoainishwa (Priority and non-priority courses) hii hutegemea sera ya nchi kwa mwaka husika wa masomo. Hapa haijalishi umesoma chuo gani bora tu uwe mtanzania basi mkopo ni haki yako.
Nakushauri uwe mwangalifu sana wakati wa kuchagua fani za kusoma na kama umejielekeza zaidi kutegemea mkopo tena kwa asilimia kubwa na sifa unazo basi chagua fani zenye priority, utafurahia matokeo yake.
Asante sana mkuu
Sima70,
Naomba nikujuze kuwa lengo la budget ya serikali ni kuhakikisha pesa zinazotengwa kwa ajili ya kitu fulani sharti itumike yoote ndio maana kila wizara au Idara ya serikali inapofikia mwisho wa mwaka wa fedha huwa wana hakikisha fedha zilizobaki zinatumika zote hata kwa kuziwekeza kwenye shughuli nyingine yoyote ili mradi pesa yote iliyo budgetiwa ionekane imekwisha.
Kwa budget ya mikopo kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali lake ktk hotuba ya wizara ya elimu ni kwamba pesa zilizotengwa kwa ajili ya mikopo hususani kwa waombaji 98,025 (new & continuing students) sharti zitumike kwa ajili ya kazi hiyo; inapotokea waombaji hawakutimia 98,025 basi pesa zao huwa wanaongezewa wale walioomba mikopo kiasi kwamba wengine hufikia kiasi cha 100% lengo likiwa ni kuhakikisha ile pesa imewekezwa kwenye kusudi lake na ndio maana kuna watu huomba courses ambazo ktk allocation ya TCU zinaonekana ni nil (dash) lakini mwisho wa siku hupewa hadi 90%, je umewahi kujiuliza hizi pesa walizopewa hawa walio omba courses ambazo hazina allocations za pesa zimetoka wapi?? Je umetambua kuwa pesa zinazobaki baada ya waombaji wengine kutoomba huwa zinaongezwa kwa waombaji walioomba kabla hata hawajaripoti Vyuoni???
Yawezekana bado ni mchanga ktk haya mambo yanavyo kwenda ndio maana unaita statistics zangu ni za uongo.
Kile kitabu cha TCU na zile percentages zake zisikuehushe hadi ukadhani kuwa zile programmes zenye dash means hawatapewa mikopono thank you , ili mradi tu uwe ume-qualify basi hata kama umeomba course ambayo haijapewa percent ya mkopo (not priority) tambua kuwa aidha utapata tuition fees na meals&accomodation au utapata kimojawapo kati ya hivyo vilivyotajwa
Ukiwa na swali la ziada unakaribishwa kuuliza. Stay blessed