Waomba mikopo heslb 2013/14 wote watapata mikopo kwa 100%

Brother James

Brother James

Senior Member
Joined
Feb 21, 2012
Messages
173
Points
225
Brother James

Brother James

Senior Member
Joined Feb 21, 2012
173 225
Leo HESLB wametoa taarifa kwa Umma juu ya idadi ya waombaji wa mikopo kama ilivyoandikwa hapa chini:

UTANGULIZI:
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawafahamisha waombaji wa mikopo kwa mara ya kwanza, Wanafunzi wanaondelea na masomo na Umma kwa ujumla kwamba mchakato wa maombi mikopo kwa mwaka wa masomo 2013/2014 ulizinduliwa rasmi tarehe 1 Mei, 2013. Mchakato huo unaendelea vizuri na kwamba wanafunzi wengi wameweza kujaza fomu za maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao (OLAS).

WAOMBAJI WA MIKOPO WA MARA YA KWANZA:
Utaratibu wa kujaza fomu za maombi kwa waombaji wa mara ya kwanza, unawaelekeza waombaji hao kutoa taarifa zao za kihistoria kama vile shule za sekondari walizosoma (Kidato cha IV na Kidato cha VI), hali ya mwombaji au wazazi wake kiafya na pia taarifa za mdhamini wa mwombaji mkopo. Taarifa hizo zinaiwezesha Bodi kuchambua na kujua iwapo mwombaji husika ana sifa ya kukopesheka au la. Ikumbukwe kwamba lengo la utoaji wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ni kuwawezesha wanafunzi wasio na uwezo wa kulipia gharama za elimu ya juu kusaidiwa kufikia malengo yao. Kwa njia ya uchambuzi huo Bodi inaweza kubaini kiasi cha mkopo unaohitajika au kiasi ambacho mwanafunzi anapaswa kuchangia katika gharama zake za elimu ya juu.Kwa vile taarifa za ufaulu katika mitihani ya kidato cha sita hazihitajiki katika hatua hii ya Mwanzo, mwombaji wa mkopo haulizwi mahali popote katika fomu yake ya maombi kuhusu kiwango cha ufaulu. Hapo baadaye Bodi itakapohitaji kuthibitisha kiwango cha ufaulu wa mwombaji itapata taarifa hizo za ufaulu moja kwa moja kutoka Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA). Kutokana na utaratibu huu, mwanafunzi aliyehitimu kidato cha sita mwaka 2013 anaweza kuomba mkopo hata kabla ya matokeo ya Kidato cha Sita kitaifa kutolewa. Hii ni muhimu ili kuipa Bodi muda wa kutosha kupokea maombi ya mikopo, kuchambua na kisha kupanga mikopo kwa wanafunzi stahiki watakaokuwa wamedahiliwa kwa mwaka mpya wa masomo 2013/2014

WANAFUNZI WALIOKWISHA OMBA MIKOPO:
Hadi kufikia tarehe 30 Mei, 2013, waombaji mikopo wa mara ya kwanza waliokwishakamilisha maombi yao ni 424, Waombaji wa mara ya kwanza ambao wako kwenye hatua mbalimbali za ukamilishaji ni 5,320 na wanafunzi wanaoedelea na masomo waliokwishathibitisha kuendelea kupatiwa mikopo kwa mwaka ujao wa masomo ni 60,367, kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini.

HITIMISHO:
Bodi inatoa msisitizo kwa waombaji wa mikopo kama ifuatavyo:(i) Kuzingatia taratibu zote muhimu zilizowekwa kwa ajili ya maombi ya mikopo.(ii) Kutumia huduma ya msaada kwa wateja (Help Desk) kikamilifu kila wanapopata tatizo lolote katika mchakato wa ujazaji wa fomu za maombi. Huduma hiyo inapatika kwa kupiga namba 022 550 7910; kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 2 usiku siku za jumatatu hadi ijumaa na kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 alasiri siku ya jumamosi.(iii) Kuzingatia muda uliopangwa wa maombi ya mikopo ambapo siku ya mwisho ni tarehe 30 Juni, 2013.
IMETOLEWA NA:

BODI YA WAKURUGENZI

BODI YA MIKOPO YA ANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

NB:
Budget ya Wizara ya Elimu kwa mwaka wa fedha 2013/2014 ni kutoa mikopo kwa jumla ya waombaji 98,025; yaani waombaji wapya watakao pata mikopo ni watu 35,649 na waombaji wanaoendelea na masomo ni 62,376.

Mbrazili

Mbrazili

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Messages
652
Points
195
Age
27
Mbrazili

Mbrazili

JF-Expert Member
Joined May 7, 2013
652 195
Naombeni niulize swali dogo wadau mnaweza kunisaidia....katika kuijaza fomu ya mkopo online ilikuwa inaniambia school name was not found nikaamua kuendelea mbele mpaka nimejaza details zote....lakini pale sehemu ya shule jina halipo bali kuna namba tu na nashindwa jinsi ya kulipata hilo jina ili niliweke.....swali langu je kama nitaipeleka fomu nitakuwa bado sahihi kwa kuwa namba ipo au ni makosa??.....na kama ni makosa nifanyeje ili kufix hili tatizo???
MSAADA PLEAAAASE
 
C

Concrete

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Messages
3,605
Points
0
C

Concrete

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2011
3,605 0
Please mleta mada badilisha hiyo title ya topic yako au Moderator wafute kabisa hii topic kwani inaupotoshaji mkubwa sana.

Hakuna mahali popote kwenye hiyo taarifa ya bodi ya mikopo inapoonesha kutoa mkopo Asilimia 100 kwa waombaji wote, sasa mleta mada nani kakutuma kuandika Title yenye kusema ''Bodi ya mikopo kutoa mkopo 100% kwa waombaji wote''

NOTE:
JF sio kijiwe cha uzushi na umbeya, ni home of great thinkers, tuwe makini tunachokiandika.
 
Mkuu wala usipate taabu sana.
Bodi ya mikopo ina watu rasmi wa kukusaidia tatizo lako.

*Tumia mawasiliano haya ya simu kuwapigia ili uongee nao.
0225507910 (muda wowote kati ya 2asubuhi na saa 2usiku kwa siku za kazi na 2asubuhi na saa 10jioni siku ya Jumamosi)

Ukiona inashindikana na kama upo Dar, basi nenda moja kwa moja ofisini kwao(Maandazi Road, Msasani-TIRDO)
 
Brother James

Brother James

Senior Member
Joined
Feb 21, 2012
Messages
173
Points
225
Brother James

Brother James

Senior Member
Joined Feb 21, 2012
173 225
RumumbaDAR,

Nilidhani kuwa wewe kama mmoja wa Ma-Great Thinkers ungeelewa tafsiri ya ujumbe uliomo ndani ya hii thread lakini umeonyesha udhaifu kuwa huna uwezo wa ku-interpret contents hiyo in relation to the Title given instead umeamua kulalamika as if umetukanwa, If you could try to ask an assistance of interpreting the title then ningekusaidia kwa urahisi kuliko kutokwa na mapovu.

Look here my friend, Tafsiri ya Title ni kwamba: Kama Wizara imetenga budget ya mikopo kwa wanachuo/waombaji zaidi ya 35,000 (New applicants) then hadi siku ya 30/60 ya kuomba mikopo hiyo zimekwisha na kuonyesha kuwa waombaji chini ya 5,800 (424-completed + 5320-in progress) ndio waliokwisha tambulika kuwa wapo katika process ya kukamilisha maombi hayo basi kwa makadirio ya siku 30 zilizobaki si zaidi ya waombaji 15,000 wataomba mikopo na kukamilisha. Kwa hiyo kwa tafsiri ya ki-statistics tofauti ya waombaji (wanachuo) 14,200 (35000-20800) inayoonekana itawafanya waombaji wapya 20,800 waongezewe fedha/mikopo zilizoachwa na waombaji 14,200 ambao hawajaomba mikopo na kusababisha kupanda kwa grades zao za mikopo na kufikia 100%. Kumbuka kuwa Serikali imekwisha tenga fedha hizo kupitia budget yake ya mwaka 2013/14 kwa waombaji wapya zaidi ya 35,000.

Kama hukunielewa vizuri basi don't hesitate to contact me pls.

Please mleta mada badilisha hiyo title ya topic yako au Moderator wafute kabisa hii topic kwani inaupotoshaji mkubwa sana.

Hakuna mahali popote kwenye hiyo taarifa ya bodi ya mikopo inapoonesha kutoa mkopo Asilimia 100 kwa waombaji wote, sasa mleta mada nani kakutuma kuandika Title yenye kusema ''Bodi ya mikopo kutoa mkopo 100% kwa waombaji wote''

NOTE:
JF sio kijiwe cha uzushi na umbeya, ni home of great thinkers, tuwe makini tunachokiandika.
 
Brother James

Brother James

Senior Member
Joined
Feb 21, 2012
Messages
173
Points
225
Brother James

Brother James

Senior Member
Joined Feb 21, 2012
173 225
Mbrazil,

Kwanza kabisa, hukutakiwa kum-support LumumbaDAR kwa ku-like aliposema kuwa title ya thread hii ina makosa; kama ungepata wasaa mzuri wa kufikiri na kutafsiri ile title. Wewe pia kama hukuelewa vizuri waweza kwenda kwenye message yake nime-mjibu vizuri tu just to help you guyz.

Pili, ninataka nikushauri kuhusu hapo ambapo jina la shule halikutokelezea;yawezekana ni human errors tu ambazo umezifanya. Kwanza fanya uthibitishe namba ya shule husika kwa kwenda website ya NECTA ambako shule zote na namba zake zinapatikana then utapata jibu kama umekosea namba au shule haitambuliki na NECTA. Ninachofahamu, shule zote zilizosajiliwa na serikali zinatambulika na NECTA na huonekana katika website yao kwa urahisi.

Sipendi sana kukushauri kuwasiliana na HESLB kwa haraka haraka kwa sababu HESLB si watu wepesi sana kupokea simu za applicants wanapopiga na pia hawana ushauri mzuri saana kwa applicants zaidi zaidi huonyesha jazba zao na kuwadharau (indirectly) applicants kuwa ni ignorants ktk matumizi ya online applications. Ikishindikana sana basi usisite kuwatafuta HESLB.

Naombeni niulize swali dogo wadau mnaweza kunisaidia....katika kuijaza fomu ya mkopo online ilikuwa inaniambia school name was not found nikaamua kuendelea mbele mpaka nimejaza details zote....lakini pale sehemu ya shule jina halipo bali kuna namba tu na nashindwa jinsi ya kulipata hilo jina ili niliweke.....swali langu je kama nitaipeleka fomu nitakuwa bado sahihi kwa kuwa namba ipo au ni makosa??.....na kama ni makosa nifanyeje ili kufix hili tatizo???
MSAADA PLEAAAASE
 
Mbrazili

Mbrazili

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Messages
652
Points
195
Age
27
Mbrazili

Mbrazili

JF-Expert Member
Joined May 7, 2013
652 195
Mbrazil,

Kwanza kabisa, hukutakiwa kum-support LumumbaDAR kwa ku-like aliposema kuwa title ya thread hii ina makosa; kama ungepata wasaa mzuri wa kufikiri na kutafsiri ile title. Wewe pia kama hukuelewa vizuri waweza kwenda kwenye message yake nime-mjibu vizuri tu just to help you guyz.

Pili, ninataka nikushauri kuhusu hapo ambapo jina la shule halikutokelezea;yawezekana ni human errors tu ambazo umezifanya. Kwanza fanya uthibitishe namba ya shule husika kwa kwenda website ya NECTA ambako shule zote na namba zake zinapatikana then utapata jibu kama umekosea namba au shule haitambuliki na NECTA. Ninachofahamu, shule zote zilizosajiliwa na serikali zinatambulika na NECTA na huonekana katika website yao kwa urahisi.

Sipendi sana kukushauri kuwasiliana na HESLB kwa haraka haraka kwa sababu HESLB si watu wepesi sana kupokea simu za applicants wanapopiga na pia hawana ushauri mzuri saana kwa applicants zaidi zaidi huonyesha jazba zao na kuwadharau (indirectly) applicants kuwa ni ignorants ktk matumizi ya online applications. Ikishindikana sana basi usisite kuwatafuta HESLB.
Duuuugh....sawa ahsante kwa ushauri ila siamini kama mi na utu uzima huu nichanganye namba yangu ya shule........kinachonipa wasi labda ni kwamba pale shuleni sisi ndo tulikuwa form 4 wa kwanza hivyo pia ni wa kwanza juingia chuo mwaka huu sasa hapa nahisi kuna delay of information katikati hapa kwa sababu wote wa shule hii tunakutana na hiki kitu......nafikiri solution ni kuwafuata tu
 
Brother James

Brother James

Senior Member
Joined
Feb 21, 2012
Messages
173
Points
225
Brother James

Brother James

Senior Member
Joined Feb 21, 2012
173 225
Mmbrazili,

Wish you all the best man.
Goodlucky
 
S

Sima70

Senior Member
Joined
Apr 9, 2013
Messages
162
Points
195
Age
32
S

Sima70

Senior Member
Joined Apr 9, 2013
162 195
Fungua kitabu cha TCU 2013/2014 uone possible loans zilivyo sio kuja na hesabu zako za ajab alaf unapotosha umma kwa kutumia jukwaa letu la watu makin

Kwa mfano UDSM 100% itatolewa kwa watu wa sayansi na mainjinia
 
Pakawa

Pakawa

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Messages
4,948
Points
2,000
Pakawa

Pakawa

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2009
4,948 2,000
Kwa hivi mikopo ni kwa ajili ya waliosoma shule za serikali au ni aje? Msaada wakuu
 
vicent x

vicent x

Member
Joined
Mar 15, 2013
Messages
91
Points
0
vicent x

vicent x

Member
Joined Mar 15, 2013
91 0
Wahusika wanalalamika hasa Arusha kua MTANDaO(website yao»»olas.heslb.go.tz) inasumbua xana xaxa itAkuaje apo afu kuna mahala wanajaziwa io FORM yA mkopo kwa Tsh 39000/= je ni halali???
 
tofali

tofali

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Messages
3,996
Points
2,000
Age
34
tofali

tofali

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2013
3,996 2,000
Na pia kwa wale walosoma diploma..mfano sehemu ya kujaza uliposomea diploma...chuo cha muhimbili hakipo...na wakati mujimbili kuna koz nyingi za diploma..je mtu aache wazi pale kwenye chuo na ajaze kwa mkono.. au afanyeje..hii ni kwa equivalent applicants..sielewi kwann kimesahaulika
 
F

Frekim

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2013
Messages
321
Points
195
F

Frekim

JF-Expert Member
Joined Mar 29, 2013
321 195
hivi waliotoka diploma watapata mkopo kweli? Naomba kuliza wakuu...
 
Brother James

Brother James

Senior Member
Joined
Feb 21, 2012
Messages
173
Points
225
Brother James

Brother James

Senior Member
Joined Feb 21, 2012
173 225
Sima70,

Naomba nikujuze kuwa lengo la budget ya serikali ni kuhakikisha pesa zinazotengwa kwa ajili ya kitu fulani sharti itumike yoote ndio maana kila wizara au Idara ya serikali inapofikia mwisho wa mwaka wa fedha huwa wana hakikisha fedha zilizobaki zinatumika zote hata kwa kuziwekeza kwenye shughuli nyingine yoyote ili mradi pesa yote iliyo budgetiwa ionekane imekwisha.

Kwa budget ya mikopo kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali lake ktk hotuba ya wizara ya elimu ni kwamba pesa zilizotengwa kwa ajili ya mikopo hususani kwa waombaji 98,025 (new & continuing students) sharti zitumike kwa ajili ya kazi hiyo; inapotokea waombaji hawakutimia 98,025 basi pesa zao huwa wanaongezewa wale walioomba mikopo kiasi kwamba wengine hufikia kiasi cha 100% lengo likiwa ni kuhakikisha ile pesa imewekezwa kwenye kusudi lake na ndio maana kuna watu huomba courses ambazo ktk allocation ya TCU zinaonekana ni nil (dash) lakini mwisho wa siku hupewa hadi 90%, je umewahi kujiuliza hizi pesa walizopewa hawa walio omba courses ambazo hazina allocations za pesa zimetoka wapi?? Je umetambua kuwa pesa zinazobaki baada ya waombaji wengine kutoomba huwa zinaongezwa kwa waombaji walioomba kabla hata hawajaripoti Vyuoni???

Yawezekana bado ni mchanga ktk haya mambo yanavyo kwenda ndio maana unaita statistics zangu ni za uongo.
Kile kitabu cha TCU na zile percentages zake zisikuehushe hadi ukadhani kuwa zile programmes zenye dash means hawatapewa mikopono thank you , ili mradi tu uwe ume-qualify basi hata kama umeomba course ambayo haijapewa percent ya mkopo (not priority) tambua kuwa aidha utapata tuition fees na meals&accomodation au utapata kimojawapo kati ya hivyo vilivyotajwa

Ukiwa na swali la ziada unakaribishwa kuuliza. Stay blessed

Fungua kitabu cha TCU 2013/2014 uone possible loans zilivyo sio kuja na hesabu zako za ajab alaf unapotosha umma kwa kutumia jukwaa letu la watu makin

Kwa mfano UDSM 100% itatolewa kwa watu wa sayansi na mainjinia
 
Brother James

Brother James

Senior Member
Joined
Feb 21, 2012
Messages
173
Points
225
Brother James

Brother James

Senior Member
Joined Feb 21, 2012
173 225
PAKAWA,

Ninachofahamu mimi ni kuwa Mikopo hutolewa kwa watanzania woote wenye sifa za jumla (yaani zilizo ainishwa na TCU) na zile zilizowekwa kulingana na chuo na fani husika. Pamoja na sifa hizo mkopo hutolewa tofauti tofauti in terms of percentages kulingana na courses zilivyoainishwa (Priority and non-priority courses) hii hutegemea sera ya nchi kwa mwaka husika wa masomo. Hapa haijalishi umesoma chuo gani bora tu uwe mtanzania basi mkopo ni haki yako.

Nakushauri uwe mwangalifu sana wakati wa kuchagua fani za kusoma na kama umejielekeza zaidi kutegemea mkopo tena kwa asilimia kubwa na sifa unazo basi chagua fani zenye priority, utafurahia matokeo yake.

Kwa hivi mikopo ni kwa ajili ya waliosoma shule za serikali au ni aje? Msaada wakuu
 
Brother James

Brother James

Senior Member
Joined
Feb 21, 2012
Messages
173
Points
225
Brother James

Brother James

Senior Member
Joined Feb 21, 2012
173 225
Ndugu yangu Vicent x,

Kiukweli mtandao wa HESLB umekuwa very slow kwa sababu upo overloaded na watumiaji kiasi kwamba access yake inasumbua saaana, hii hutokana na idadi kubwa ya wahitaji wa mikopo wanaofungua website ya HESLB kwa wakati mmoja na hii imetokana na wengi wao kumaliza usajili kule TCU na sasa wamehamia HESLB. Kama utakuwa na computer/Laptop na access ya Internet nakushauri jaza mambo yako usiku hususani kuanzia saa mbili angalau access yake inakuwa ipo vizuri kutokana na kuwa idadi kubwa ya internet cafe huwa zimefungwa na waombaji wachache hubaki online.

Wajua, kipindi kama hiki ni neema kwa baadhi ya watu hususani wafanya biashara wa internet cafe, kutokana na soko huria tulilo nalo TZ kila msajili hujiwekea bei yake kwenye suala zima la usajili, ila kiuhalisia usajili kwa ujumla (TCU&HESLB) pamoja na kuprint zile page 5 za HESL haitakiwi kuzidi 10,000, hii ndio bei ambayo hata hapa mtaani kwetu watu hutozwa

Wahusika wanalalamika hasa Arusha kua MTANDaO(website yao»»olas.heslb.go.tz) inasumbua xana xaxa itAkuaje apo afu kuna mahala wanajaziwa io FORM yA mkopo kwa Tsh 39000/= je ni halali???
 
Mbrazili

Mbrazili

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Messages
652
Points
195
Age
27
Mbrazili

Mbrazili

JF-Expert Member
Joined May 7, 2013
652 195
Wahusika wanalalamika hasa Arusha kua MTANDaO(website yao»»olas.heslb.go.tz) inasumbua xana xaxa itAkuaje apo afu kuna mahala wanajaziwa io FORM yA mkopo kwa Tsh 39000/= je ni halali???
Inaeza kuwa poa tu kwa sababu M pesa 30000 gharama ya kuprint 5000 na hiyo 4000 ni ya internet cafe kwani somtymez unaeza tumia hata masaaa 5 na bado usifanye chochoteeee
 
Pakawa

Pakawa

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Messages
4,948
Points
2,000
Pakawa

Pakawa

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2009
4,948 2,000
PAKAWA,

Ninachofahamu mimi ni kuwa Mikopo hutolewa kwa watanzania woote wenye sifa za jumla (yaani zilizo ainishwa na TCU) na zile zilizowekwa kulingana na chuo na fani husika. Pamoja na sifa hizo mkopo hutolewa tofauti tofauti in terms of percentages kulingana na courses zilivyoainishwa (Priority and non-priority courses) hii hutegemea sera ya nchi kwa mwaka husika wa masomo. Hapa haijalishi umesoma chuo gani bora tu uwe mtanzania basi mkopo ni haki yako.

Nakushauri uwe mwangalifu sana wakati wa kuchagua fani za kusoma na kama umejielekeza zaidi kutegemea mkopo tena kwa asilimia kubwa na sifa unazo basi chagua fani zenye priority, utafurahia matokeo yake.
Asante sana mkuu
 
M

MASSIVE BOOM

Member
Joined
Jun 9, 2012
Messages
8
Points
0
M

MASSIVE BOOM

Member
Joined Jun 9, 2012
8 0
Bro James, kwa data na maelezo yako kwa kweli nimefarijika na kwa kweli 100% nakubaliana na wewe
Sima70,

Naomba nikujuze kuwa lengo la budget ya serikali ni kuhakikisha pesa zinazotengwa kwa ajili ya kitu fulani sharti itumike yoote ndio maana kila wizara au Idara ya serikali inapofikia mwisho wa mwaka wa fedha huwa wana hakikisha fedha zilizobaki zinatumika zote hata kwa kuziwekeza kwenye shughuli nyingine yoyote ili mradi pesa yote iliyo budgetiwa ionekane imekwisha.

Kwa budget ya mikopo kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali lake ktk hotuba ya wizara ya elimu ni kwamba pesa zilizotengwa kwa ajili ya mikopo hususani kwa waombaji 98,025 (new & continuing students) sharti zitumike kwa ajili ya kazi hiyo; inapotokea waombaji hawakutimia 98,025 basi pesa zao huwa wanaongezewa wale walioomba mikopo kiasi kwamba wengine hufikia kiasi cha 100% lengo likiwa ni kuhakikisha ile pesa imewekezwa kwenye kusudi lake na ndio maana kuna watu huomba courses ambazo ktk allocation ya TCU zinaonekana ni nil (dash) lakini mwisho wa siku hupewa hadi 90%, je umewahi kujiuliza hizi pesa walizopewa hawa walio omba courses ambazo hazina allocations za pesa zimetoka wapi?? Je umetambua kuwa pesa zinazobaki baada ya waombaji wengine kutoomba huwa zinaongezwa kwa waombaji walioomba kabla hata hawajaripoti Vyuoni???

Yawezekana bado ni mchanga ktk haya mambo yanavyo kwenda ndio maana unaita statistics zangu ni za uongo.
Kile kitabu cha TCU na zile percentages zake zisikuehushe hadi ukadhani kuwa zile programmes zenye dash means hawatapewa mikopono thank you , ili mradi tu uwe ume-qualify basi hata kama umeomba course ambayo haijapewa percent ya mkopo (not priority) tambua kuwa aidha utapata tuition fees na meals&accomodation au utapata kimojawapo kati ya hivyo vilivyotajwa

Ukiwa na swali la ziada unakaribishwa kuuliza. Stay blessed
 
Forum statistics

Threads 1,284,923
Members 494,338
Posts 30,845,062
Top