Waomba ajira watengwa kwenye usaili

KWEZISHO

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
7,519
6,511
Hili jambo halijakaa vizuri na wala halipendezi. Kwa kweli limenisikitisha sana:

Waombaji 27 wa nafasi za kazi ya mtendaji wa kijiji daraja la III katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe wamelalamika wakidai wamezuiwa kusailiwa.
Waombaji hao wenye cheti cha mipango ya maendeleo vijijini kutoka Chuo cha Mipango cha Dodoma wanalalamika wakidai wamekataliwa kusailiwa wakielezwa hawana sifa katika muundo wa utumishi.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Amina Kiwanuka, akizungumza kwa simu na Mwananchi leo Jumapili amesema hawezi kuzungumzia suala hilo isipokuwa wanaoweza kulisema ni Bodi ya Ajira na Wizara ya Utumishi.
Taarifa kuhusu suala hilo zimesambaa mtandaoni leo Jumapili ikiwemo video inayomuonyesha mtu aliyeelezwa kuwa ofisa utumishi wa wilaya hiyo akiwaita waomba ajira hao na kuwapa tangazo akisema:
“Ninyi ndiyo vijana mnatafuta maisha, mimi wala si mzee ni kijana kama ninyi, siwezi kufanya kitu chochote cha kuwasaidia lakini sisi tuna muundo, yaani scheme of service ambao sifa zake hazijataja watu wa rural, maendeleo vijijini. Ingawaje ulikuja kwangu, mimi kama mimi naona mna fit, ila muundo ambao ndiyo tunausimamia haukutaja.”
Alisema vijana hao kama wangesailiwa kwenye ajira wangepata matatizo, hivyo ili kuepusha shida waliwaondoa kwenye usaili.
Hata hivyo, aliwaeleza wanaotaka kufanya kazi kwa kujitolea waandike barua ili wafikiriwe.
Mmoja wa waomba ajira hao aliyejitambulisha kwa jina la Ayoub Kavina alisema wao 27 ni miongoni mwa wengine walioitwa wilayani humo kusailiwa lakini walitengwa.
“Jana tuliitwa wilayani Wanging’ombe kufanya usaili. Mimi ni mmoja wa waliosoma Cheti cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, tumesomea Chuo cha Mipango Dodoma. Tangazo lililotolewa lilitaja sifa zetu, lakini tukashangaa wenzetu wanasailiwa na sisi tukatengwa,” amesema Kavina.
“Tangazo lile la ajira lilionyesha sifa zetu, lakini tunashangaa tumefika huko wanasema muundo wa utumishi hauturuhusu. Miongoni mwetu kuna watu wametoka Kilimanjaro na Mwanza. Mimi nimetoka Dar es Salaam ijapokuwa kwa sasa naishi Dodoma. Tumeishiwa fedha na hatuna tena matumaini ya kuajiriwa,” alisema.
Mwingine aliyeomba ajira ni Lusajo Mwabulambo aliyesema wasailiwa 900 waliitwa kuwania nafasi 52 za utendaji wa vijiji daraja la tatu.
“Ni kweli tatizo limetukuta sisi tuliosoma kozi ya mipango. Tangazo lilisema wanataka watu waliosoma Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo na vyuo vyote vya maendeleo ya jamii na mipango vinavyotambuliwa na Serikali. Chuo cha Mipango Dodoma si tu kinatambuliwa na Serikali, bali pia ni cha Serikali,” amesema Mwabulambo.
Amesema licha ya wao kukataliwa kufanya usaili, wana taarifa kuwa wenzao wameruhusiwa katika wilaya nyingine.
Akizungumzia hilo, Fausta Lukuba amesema tangazo la kazi lilitaka watu waliosoma sheria na maendeleo vijijini kwa ngazi ya cheti, lakini wanashangaa kuambiwa muundo wa utumishi umewakataa.
Kwa upande wake, Naomi Maendaenda amesema wameandika barua kwenda Wizara ya Utumishi kueleza kero hiyo.
“Hatuelewi kosa letu kwa sababu kozi tuliyosoma inaendana na kazi tuliyoomba. Ndiyo maana tumemwandikia barua mkuu wa chuo na itakwenda hadi Wizara ya Utumishi kujua hatima yetu,” amesema.
Malalamiko hayo pia yametolewa na Benadetha Magungu anayesema, “Naona tumeonewa kwa sababu tulipoona tangazo tuliandika barua na tukaitwa kwenye usaili. Kama hatukuwa na sifa kwa nini tuliitwa? Tumefika pale wanatuambia muundo haututambui.”
Amesema, “Tumetoka mikoani, tumetumia nauli, halafu tunakataliwa kufanya usaili na hakuna fidia yoyote tuliyopewa.”
By Elias Msuya, Mwananchi emsuya@mwananchi.co.tz
 
Hiyo hali imewakuta hadi watu walioenda kwenye usaili masasi, mfumo unakataa! Kiukweli huo mfumo uache ubaguzi Mungu hapendi
 
Mimi ninachojiuliza je walibe shortlisted au walijepekea tu kwa walisikia kuna interview? kama wali be shortlisted huo wahusika walikutwa na nini mpaka kuwashortlist watu wasio na sifa?
poor them!
 
Back
Top Bottom