Waoga wanavyoharibu nchi

Hii ya kuwa waoga ni tz tu huko wenzetu wanakiamsha sana..mfano south Africa..

Ila na wewe mtoa mada unapotoa mifano ya kina Nyerere hapo unakosea hivi kipind wanadai uhuru ulishasikia Nyerere alitekwa na wakoloni au mtu alipigwa risasi..

maana yake ni kuwa ingawa tulitawaliwa na wakoloni lkn hao wakoloni walikuwa na humanity kwa kiasi kikubwa ukicompare na sasa ingawa african tulikuwa daraja la chini kabisa...

jaribu kuwa mwanaharakati sasa namaanisha mwanaharakati kweli sio njanjaa then ndio utajua hujui..

masiki akipata madaraka huwa na ubinafsi na roho mbaya sanaaa na yupo tayar afanye chochote ili alinde ugali wake..
 
Hakika, ukoloni mweusi umetia fora Africa
 
Unafikiri raia wote wakingia barabarani na mitaani polisi,jeshhi sjui nani watawazuia...si unaona srilanka maana inabidi Jeshi liwatizame tu

Ova
 
Mleta thread,tufanye nini ili tusionekane waoga tena mbele ya macho na akili zako?
Tuchukue hatua kupinga matendo mabaya yanayofanywa na watawala yanayoumiza Nchi.Tuwafanye watekeleze majukumu yao kwa kufuata haki.Haya yoye yanawezekana pale wtz wakiondoa uwoga ikiwa ni pamoja na kufanya maandamano yasiyo na kikomo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhusu maandamano yasiyo na kikomo:
-Umetuandalia mawakili wa kesi zetu za ugaidi na uchambuzi wa PGO?
-Unaweza kutumegea mbinu mlizotumia "hapo kale" kukwepa au kukabiliana na kipigo cha kuchakaa kama mbwa-koko?
 
Kuhusu maandamano yasiyo na kikomo:
-Umetuandalia mawakili wa kesi zetu za ugaidi na uchambuzi wa PGO?
-Unaweza kutumegea mbinu mlizotumia "hapo kale" kukwepa au kukabiliana na kipigo cha kuchakaa kama mbwa-koko?
Mbinu tulizotumia hapo kale ni ujasiri tu hakuna kingine.Kwa sasa mawakili wapo wengi sana ikiwa tu na wao wakaondoa uoga maana mifumo kandamizi huumiza wote ikiwemo na hao mawakili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbinu tulizotumia hapo kale ni ujasiri tu hakuna kingine.Kwa sasa mawakili wapo wengi sana ikiwa tu na wao wakaondoa uoga maana mifumo kandamizi huumiza wote ikiwemo na hao mawakili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona kama unarahisisha,kututupia mizigo na kutuacha tujicheki.Kwa hiyo tukiwa maamdamanoni na kuanza kubondwa marungu,fimbo,mateke na hata kuvurumishiwa marisaa tutoe macho tu kwa ujasiri?Na hao mawakili "waliojaa siku hizi" tutawalipa madebe ya ubuyu mkavu?Tufafanulie.Akili yetu ni nyembamba kama tishu.
 
Kuhusu pesa za kuwalipa hawo mawakili ondoa hofu kabisa.pesa ninazo nyingi sana si unaona jina langu linajieleza kuwa pesa zipo zakutosha tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Si tumeambiwa tusitumike na mabeberu tulinde amani yetu na nchi nyingi sana zinatuonea wivu sisi kwa kua ni kisiwa cha amani.
mindset [emoji23][emoji23][emoji23]huyu mzee angezewe moto....
 
HAKUNA VIJANA kuna WAHUNI tu kazi yao kubwa kulamba SOLI za Viatu za WATAWALA
 
Kwa hiyo bora wakoloni wangeendelea kubaki, unaona ni bora kutawaliwa na mzungu kuliko mwafrika mwenzako. Mmh hatari

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…