Wanyonge mkiungana-shairi

Wanyonge mkiungana-shairi

KAMBOTA

Senior Member
Joined
Mar 21, 2011
Posts
176
Reaction score
104
mtotoooooo.jpg

Na Nova Kambota, +255712 544237
Jumapili, 16 Novemba 2014
Dar es salaam, Tanzania.

Tano miongo yapita, taifa ladidimia


Wengi wameshastuka,dawa wajitafutia

Viongozi kadhalika, mali walimbikizia

Wanyonge mkiungana, minyororo mtakata



Tazama kwenye ramani, utaona hiyo nchi

Nchi ya wasio soni, wenye tabu wananchi

Raia wapo kinuni, watwangaji wana mchi

Wanyonge mkiungana, minyororo mtakata




Chama kisicho na dira, kimekamata hatamu

Wanakula kwa papara, hamu ya kula utamu

Roho zao za harara, mikono yao ya damu

Wanyonge mkiungana, minyororo mtakata




Wameileta rasimu, bila maoni ya watu

Kutawala wana hamu, roho zimekosa utu

Chama kisicho nidhamu, mfumo wake wa kutu

Wanyonge mkiungana, minyororo mtakata




Unganeni masikini, mijini na vijijini

Zinduka jitambueni, enyi tabaka la chini

Mmefanywa kuwa duni, jitoeni kitanzini

Wanyonge mkiungana, minyororo mtakata




Ondoeni hilo giza, enyi wana afrika

Hakuna cha kubakiza, pigeni kura ya zika

Nchi yazidi kuviza, inakumbwa na gharika

Wanyonge mkiungana, minyororo mtakata




Si dawa si pembejeo, hazipo tele nchini

Heri jana sio leo, taifa la watu duni

Amebanwa kwa koleo, hana hali masikini

Wanyonge mkiungana, minyororo mtakata




Zindukeni kina mama, mlete mabadiliko


Kataeni hiko chama, cha hao wavuta kiko

Idondosheni zahama, kataeni matambiko

Wanyonge mkiungana, minyororo mtakata




Vijana msitumike, bendera fata upepo

Lazima mmakinike, msiwe mfano popo

Pigeni ngumi na teke, hao walamba makopo

Wanyonge mkiungana, minyororo mtakata



Tamati nimefikia, beti kumi natulia

Wavuja jasho sikia, mwongozo fatilia

Unyonyaji kukataa, nchi ipate kupaa

Wanyonge mkiungana, minyororo mtakata.



Mtunzi wa shairi hilini Nova Kambota, ni mchambuzi na mwandishi wa siasa anayeishi jijini Dar es salaam, anapatikana kwa simu 0712-544237 , barua pepe; novakambota@gmail.com , waweza kutembelea Blog yake; Nova Kambota | Mchambuzi&Mwanaharakati
 
.. FaizaFoxy.. Lizaboni.. simiyuyetu na magamba wengine natumai ujumbe huo wenye hisia kali urakuwa umewapata...
 
Last edited by a moderator:
Huo maisha yamemshinda alifikiri kila kitu unakaa ukaletewa mezani.

Amechanganyikiwa.
 
Back
Top Bottom