Mi naomba kujua umefikiria nini hadi kuuliza hili swali?
Kilichopelekea nifikirie kulileta hili, nadhani hata wewe kuna wkt inakutokea uka'create Thread accordingly enviroment around.
Tulikua tumekaa sehemu mimi na wenzangu wa4, eneo ambalo tunakaa mara kwa mara ku'buz time.
Katika eneo hilo hua kuna paka wengi wanaozungukazunguka, na inapofika saa 12 Mbwa wa hapo hufunguliwa.
Mbwa wakishafunguliwa Paka hukosa amani kwn haipiti muda Paka wanakurupushwa.
Hasa yupo Mbwa mweupe dume mtemi kwelikwl, yeye ndiyo hua hakubali kumuona Paka upeo wa macho yake.
Leo kuna Paka mmoja wa Rangi michirizi kama njano au kahawia hivi, akamdindia mtemi huyo Mbwa. Paka yule alijitunisha akapanda juu karibu akaribie urefu wa Mbwa, (wakati huo sisi wote tukawa makini kuangalia ligi hiyo )
Kilichofata wakaungurumiana kisha mtemi Mbwa ndiyo alianza kuondoka, na akatambaa.
Kupita kama nusu saa hivi, Mbwa mtemi akarudi tena eneo hilohilo palipotaka kutokea ugomvi.
Mara hii akamkuta Paka mweusi.
Akamvagaa Paka black akaumwaga.
Hapo ndy sisi tukaanza kujadili, baadhi yetu wakawa wakisema yule Mbwa alidhani ni Paka yule wa kwanza, wengine wakakataa, kua hapana Mbwa ana utambuzi wa kutambua rangi kua yule Paka wa kwnz ni rangi nyingine na huyu rangi nyingine.
Inshort pale hatukupata ufumbuzi which is which !
Ndiyo nikashawishika nililete huku kwa watu waliokwenda Shule .