PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 354
- 396
Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Makunduchi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wanu Hafidh Ameir, amesema uamuzi wa Chama cha ACT Wazalendo kutoweka mgombea wa urais mwaka huu ni ishara tosha ya kutambua kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye amethibitisha kuwa ni mwanamke shupavu na kiongozi imara wa mfano.
Wanu ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Gereji Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja, ambapo aliwataka wananchi kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Tanzania pamoja na viongozi wengine wanaoendana na dira ya maendeleo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Amesema hakuna shaka kwamba kazi kubwa na mageuzi makubwa ya maendeleo yaliyofanywa na Dkt. Samia katika kipindi cha uongozi wake ni uthibitisho wa umahiri na uthubutu wake katika kusogeza huduma kwa wananchi.
Wanu ameongeza kuwa wananchi wa Makunduchi na Watanzania kwa ujumla wanapaswa kuendelea kumuamini Dkt. Samia, kwa kuwa chini ya uongozi wake Tanzania inaendelea kupaa katika nyanja zote za maendeleo.