Wantanzania 29 wakwama Saudi Arabia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wantanzania 29 wakwama Saudi Arabia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Emanuel Makofia, Nov 23, 2011.

 1. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  [h=3]Wantanzania 29 wakwama Saudi Arabia[/h] Kuna watanzania 29 ambao wamekwama baada ya kuachwa na ndege kwa uzembe wa Kiongozi wa msafara wao. Leo hii ninavyoandika habari hii, imekuwa ni siku ya Tatu Watanzania hao hawajui hatima ya msafara wao, Kila wakienda uwanja wa Ndege wanaambiwa bado tunashughulikia.

  Imefikia mpaka kiongozi waliokuwa naye, amekata tamaa, hawa watanzania wamenyang'anywa passport zao za kusafiria na wanakaa kama watumwa. Inabidi ieleweke wazi kuwa watoto, familia, ndugu, na jamaa wa hizi familia wana wasiwasi mkubwa, kwani wanaweza kuhisi kuwa ndugu hawa wamekanyagwa na kufa/ama kutokewa na jambo baya.
   
 2. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Ama hao ndugu walio baki TZ wafanye mipango ya mawasiliano na Riyadh.. Mungu apishie mbali,wasije hao ndugu wakawa wameshikwa na shida au tamaa kisha wakageuka ombaomba!
   
 3. Bu'yaka

  Bu'yaka JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 851
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 80
  Sio kwamba yamechelewa ndege ni kwamba eti passport zao kashika mtu mwingine na "uzembe wa kiongozi wa msafara." Utakwamaje sehemu kwa sababu ya "uzembe wa kiongozi wa msafara"?

  Mi nimeondoka nyumbani mtoto mdogo kwenda kuanjia elimu na maisha nchi za watu na sikuwa na cha kiongozi wa msafara wala cha mtu wa kunishikia passport, na ushamba wangu wote na ugeni sikuwahi kukwama airport za watu eti kuna mjinga mjinga kanishikia passport. Ndio hizi mentality za kibongo, polisi anakukamata anakunyang'anya driver's license yako! Unishikie passport yangu? Nitakukula nyama!
   
 4. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Iwapo ni mahujaji basi uzembe utakuwa wa viongozi wao. Ama juu ya ppt zao ni kawaida mahujaji wanapowasili ppt zao huhifadhiwa na wizara ya dini kupitia maajenti maalumu wenye uzoefu wa kazi hiyo ambao hata hao mahujaji wanakuwa chini ya dhima yao hadi watakapondoka nchini Saudi Arabia. Kila nchi inapewa agenti wake ili kuwarahisishia mahujaji matatizo. Ipatikane sababu ya kweli kwanini wameachwa kabla kumlaumu mtu au taasisi.
   
 5. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Iwapo wataachiwa ppt zao basi kutakuwa na hatari ya baadhi yao kuzipoteza na wengine kupata mwanya wa kujichimbia huko wakabakia huko wasirudi makwao. Ppt zote huhifadhiwa katika makabati ya fire proof.
   
 6. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Kama individual kila mtu anakabidhi ppt yake kwa ajenti wa wizara kabla hajatoka mjengo wa airport. Utaipokea tena hio ppt yako airport wakati unarudi. Kiongozi wa msafara ndiye anayeratibu na maajenti kuhakikisha kusiwe na tatizo. So sio kuwa ni ujinga bali wenye nchi yao wamepanga hivyo.
   
 7. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Poleni sana watz wenzangu. Kuna haja ya serikali kusimamia safari za hijja hawa "viongozi" wetu wameshindwa kabisa hili zoezi
   
 8. Bu'yaka

  Bu'yaka JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 851
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 80
  Hakuna kitu kama hicho. Haulazimishwi kwenda kuhiji na Mkuu wa msafara! Sio lazima uwe kwenye msafara, period.

  Na utasemaje Mkuu wa Msafara yupo kuhakikisha kusiwe na tatizo wakati obviously tunaona huyu ndio chanzo cha matatizo?
   
 9. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Bu'yaka unataka kufanya ubishi? Huwezi kwenda kuhiji as individual lazima uwe katika msafara wa taasisi za hapa nyumba zilizosajiliwa hapa na kukubalika kule Saudi Arabia.
   
Loading...