Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,943
- 6,863
Wakati sisi wamisheni tunajiandaa kusheherekea Krismas na wenzetu kusheherekea Iddi hivi karibuni, ni wangapi katika sisi tunaojivunia weusi wetu tutakaosheherekea Kwanzaa? Hasa wenzetu mlio kwa Obama!
Kwa wale wasiojua Kwanzaa ni nini, waangalie hapa The Official Kwanzaa Web Site - Kwanzaa African American Celebration of Family, Community and Culture by Maulana Karenga
Amandlaa.......
Wakati sisi wamisheni tunajiandaa kusheherekea Krismas na wenzetu kusheherekea Iddi hivi karibuni, ni wangapi katika sisi tunaojivunia weusi wetu tutakaosheherekea Kwanzaa? Hasa wenzetu mlio kwa Obama!
Kwa wale wasiojua Kwanzaa ni nini, waangalie hapa The Official Kwanzaa Web Site - Kwanzaa African American Celebration of Family, Community and Culture by Maulana Karenga
Amandlaa.......
Leo tunatafakari: Kujichagulia (Self-Determination)
To define ourselves, name ourselves, create for ourselves and speak for ourselves.
Sisi kama watu weusi tuna nafasi gani katika kujitambua? Kwa nini mpaka leo tunakubali identity tuliyopewa na wengine? Kukubali huko ndiko kunakotupelekea kuamini kuwa " Miafrika ndivyo tulivyo." Kukubali huko ndiko kunakotufanya tuamini kuwa tuna laana na hakuna anayeweza kutubadili. Kukubali huko ndiko kunatufanya tuwakumbatie wakina Mugabe ambao wamejiteua kuwa ndio wasemaji wetu. Ni lini tutaacha kukumbatia tuliyoletewa na kukumbatia cha kwetu? Sikukuu hii ikiwa ni mojawapo!Ni lini, tutakataa, na kusema kwa nguvu, kwa sauti kubwa " hapana, sivyo tulivyo!"
Amandla...........
Actions speak louder than words....I can show you better than I can tell you...your bark is worse than your bite...etc. etc.....
Mpaka tutakapoanza kuongea kwa vitendo tutabaki kuwa Ndivyo Tulivyo hata mfanyeje. Hata wakiniondolea signature yangu, hata hata nikibaki peke yangu nisemaye ndivyo tulivyo, yaani hata iweje, tusipotenda maneno yetu ya kukataa kuwa ndivyo tulivyo hayatabadilisha ukweli. Kitu kitakachobadilisha ukweli ni vitendo. Maneno hayabadilishi ukweli.
Leo tunafakari Ujamaa (Cooperative Economics):
To build and maintain our own stores, shops and other businesses and to profit from them together.
Wangapi tumeweza kufanya hivi? Au hii sera haina nafasi tena katika jamii ya leo?
Fundi kwanza asante. Hii itawezekana pale tu tutakapojijengea uaminifu kwa kila mmoja wetu (mtu binafsi) na uaminifu kwa society. Kama mtu anaweza kukikimbia na michango ya harusi aliyochangiwa kwa ajili ya harusi yake mwenyewe, tunaweza kumuamini na kumpa usimamizi wa hizo biashara ?
Kuna mahali hili somo la kuwafikiria wengine kama tunavyojifikiria wenyewe linatolewa ? May be tutaachana na selfishness leadind to elimination of ufisadi.
Baada ya hapo FM, hili litawezekana. Kwa sasa hata kuwa na sera, bado hatutaweza.....ni wizi mtupu.
Leo tunatafakari, Nia (Purpose):
To make our collective vocation the building and developing of our community in order to restore our people to their traditional greatness.
Hii kwangu mimi ina uzito wa pekee hasa katika wakati huu ambapo kila ukiangalia kuna mifano ya jinsi sisi kama watu weusi tulivyo nyuma kimaendeleo. Ni rahisi sana kutumbukia katika aidha dhana ya kusema " sisi ndivyo tulivyo" au kuwanyoshea vidole wengine na kudai wao ndiyo waliosababisha na ndiyo wanaoendelea kusababisha matatizo yetu! Hivi kweli, tukiamua, hatuwezi kweli kujitoa huku tuliko? Tunahitaji kweli upendeleo au mfadhili wa kutukwamua? Mimi siamini hivyo. Sijui mwenzangu?
Fundi, tukiamua kufanya kweli tunaweza! Lakini kabla ya kuamua inabidi tukasirike na kusema sasa enough is enough. Nikisema sisi Miafrika Ndivyo Tulivyo watu wananikasirikia mimi. Hiyo ni misplaced outrage. Kinachotakiwa kukasirikiwa ni hali tuliyonayo. Unapomkasirikia Ngabu haisaidii lolote. Ngabu akiacha kusema hivyo ina maana hali yetu itabadilika? Hell no.
Najua wengi hawanielewi nini maana na dhumuni la kwangu kusema sisi Miafrika Ndivyo Tulivyo. Wanadhani labda mimi kweli naamini hivyo. Hata hivyo hamna neno. Ipo siku nitakuja kuweka bayana nini namaanisha nikisema hivyo.
Kwa hiyo niko na wewe katika kuamini kuwa tukiamua tutaweza tena bila hata hao wafadhili. Mimi ni mmoja wa wapinga misaada ya kutoka kwa wafadhili wa nguvu sana. Misaada imetudekeza mno. Kuweza tunaweza lakini kabla ya kuweza inabidi tukasirike kwanza. Hayo ndo yangu machache tu kwa leo.....