Wangapi Mngechukua Hii Kazi?

TinyMonster

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2009
Posts
242
Reaction score
154
Huyu ni kijana anaefanya sanaa ya uchoraji kapewa kazi na jeshi la polisi kuandika bango la onyo/vitisho kwa raia ambao walikuwa wanajiandaa kwenda kwenye mkutano wa chama cha siasa wilayani Ngara. Swali la kizushi, ungekuwa wewe ungeikubali hii kazi?

Si ajira unadhani hata FFU anapogonga virungu anapenda??Huwa tunazungumza nao wanasema hata wao roho zinawauma ila ni kazi jamani!!!!
 
Yeah, ningekamata kazi hiyo, halafu naenda kuhudhuria huo mkutano kama kawaida
 
Kuna fundi cherehani mmoja kiongozi wa CCM huko Sumbawanga alipata tenda ya kushona bendera za CHADEMA zilizokuwa zinatumika wakati wa kampeni ya ubunge 2010. Jamaa alichukua hiyo kazi, lakini wana CCM wakaja kumfukuza uongozi na uanachama!
 
Hahaha majanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…