Wanazuoni washauri kubadilishwa mfumo wa elimu

Wanazuoni washauri kubadilishwa mfumo wa elimu

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,274
Reaction score
25,322
warioba 2.jpg

Wanazuoni wameshauri kubadilishwa kwa mfumo wa elimu ulio hivi sasa ili kuendana na sera ya Tanzania ya viwanda kwa kuwajengea uwezo zaidi wanafunzi walioko katika vyuo na shule mbalimbali hapa nchini.

Wanazuoni hao wakichangia mjadala wa Tanzania kuelekea uchumi wa viwanda kufikiri upya sera ya elimu ya kujitegemea wamesema dhamira ya serikali ya viwanda inaweza kufikiwa kikamilifu endapo serikali kupitia wizara ya elimu itaufanyia mageuzi mfumo wa elimu ulipo ili uendane na sera ya viwanda.

Mjadala huo wa siku mbili uliohudhuliwa na viongozi mbalimbali waandamizi serikalini, ofisi ya waziri mkuu inasema imekuja na mpango maalum kwa miaka mitano unaolenga kuwajengea uwezo vijana kuelekea katika uchumi wa viwanda.

Waziri wa nchi ofisi ya rais TAMISEMI aliyesoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya waziri mkuu pamoja na masuala mengine amesema serikali iko tayari kufanyia kazi mapendekezo yote yatakayoibuliwa katika mjadala huo huku mtendaji mkuu wa taasisi ya haki elimu akitaka uwepo wa falsa itakayoongoza sekta ya elimu kuelekea uchumi wa viwanda.

Mjadala huo wa siku mbili wenye kauli mbiu ya tafakuri ya sera ya elimu ya kujitegemea kuelekea maendeleo ya viwanda, umeandaliwa na jumuiya wa wahitimu wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na taasisi ya elimu Tanzania na kushirikisha wdau mbalimbali wa sekta ya elimu.


ITV
 
Back
Top Bottom