Wanazuoni wa Kiislamu waonya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanazuoni wa Kiislamu waonya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Father of All, Oct 22, 2012.

 1. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  TAASISI ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislam Tanzania imewaasa Watanzania kuzingatia utawala wa sheria na kutii amri za mamlaka zilizoundwa kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo, Sheikh Khamis Mataka, alisema kuwa wamelazimika kutoa kauli hiyo kutokana na baadhi ya Waislamu kuwa na ghadhabu na kusababisha uharibifu wa mali za watu wasio na hatia na kuchoma makanisa.

  Alisema taasisi hiyo ilifanya mkutano kwa siku mbili kutafakari afya ya jamii kufuatia tukio la kunajisiwa kwa Kuran Tukufu na ghasia zilizotokea Mbagala zilizohusisha kutotii sheria na amri za mamlaka na uchomaji wa makanisa.

  Sheikh Mataka aliongeza kuwa sekretarieti yao imetazama suala la vurugu zilizotokea Kariakoo ambapo baadhi ya waumini waliishia mikononi mwa vyombo vya dola na pia waliangalia vurugu za Zanzibar ndipo wakatoa tamko hilo.

  Alisema taasisi hiyo imesikitishwa sana na baadhi ya Wasilamu kutumia mikusanyiko isiyo halali kupingana na Jeshi la Polisi chini ya shinikizo la kutaka kuachiwa watuhumiwa waliokuwa wamekamatwa.

  Mataka alisema kinachofanyika sasa ni watu kutozingatia mafundisho ya dini kwani yanahimiza utulivu, amani na kuheshimu kila kilichowekwa kwa taratibu na kuwataka viongozi wote wanaohamasisha machafuko kurejea mafunzo hayo kama msingi wa kudumisha amani nchini.

  Alibainisha kuwa taasisi hiyo imeshtushwa na baadhi ya matamko ya viongozi wa dini ya Kikristo yanayotaka kuitumia kadhia hii kuutia doa Uislamu na Waislamu na kujenga uhalali wa kuitikisa misingi ya udugu kiasi cha kutamani kuzaliwa Tanzania mpya.

  Sheikh Mataka alisisitiza kuwa kauli ya maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) iliyotolewa hivi karibuni ilikuwa na mafumbo na hivyo kuzua hofu.

  Hata hivyo alisema kuwa taasisi hiyo imesikitishwa na baadhi ya askari waliotumia vibaya ruhusa ya kutumia nguvu katika kuzima fujo hizo, bila kuzingatia mazingira na maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu na shughuli za kiuchumi.

  "Taasisi pia inatoa pole kwa Rais wa Zanzibar na Mkuu wa Jeshi la Polisi kufuatia kuuawa kinyama kwa askari asiye na hatia, Saidi Abdulrahman na pia kutokana na vurugu hizo tunatarajia kuitisha kikao cha masheikh na viongozi wa taasisi mbalimbali za Kiislamu ili kutafuta dawa ya tatizo hili," alisema Mataka.

  Aliongeza kuwa mbali na kuitisha kikao cha viongozi wa Kiislamu lakini pia taasisi inatarajia kuitisha kikao cha viongozi wa dini mbalimbali ili kujadili miundo bora ya kudumisha amani, utulivu na uhusiano mwema baina ya wanadini kwa misingi ya kila mmoja kumheshimu mwenzake.

  Taasisi hiyo pia iliwatahadharisha wanasiasa kujiepusha kwa namna moja au nyingine kubariki vurugu za vikundi vya kidini na jamii kwa ujumla na ikawataka waache kutoa ushawishi wa kujichukulia sheria mikononi na kuhamasisha kutotii amri halali za mamlaka za nchi.

  Akijibu swali la waandishi waliotaka kujua endapo angekutana na Sheikh Ponda leo atamshauri nini, alisema atamwambia azingatie Uislamu katika kufanya mambo yake.
   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Somebody has sense after all!
  This is what we wanted to hear. Nashangaa kwa nini imechukua muda vile. Usijali magumbo ya tamko la kkkt, phd tupu zikikutana nazo ni shughuli, that is perfectly understood. Ritz, msaada hapa. Hii taasisi ni yetu eh?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,394
  Trophy Points: 280
  Taasisi ya Idd simba hiyo!Mataka nae mchumia tumbo tuu.kauli zao huwa sawa na za bakwata ili waendeleze ufisadi
   
 4. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hawa Wanazuoni wa Kiislam elimu yao ni ndogo sana ndio maana hawajawaelewa maaskofu wa KKKT. Nawashauri waende shule.
   
 5. s

  salmar JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 782
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Mataka ni jina ama?
   
 6. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Hongera sana baba mkuu mkuu makumazan! maneno hayo siyo tuu yametoka kinywani mwako bali pia ni maneno ya mungu kupitia kinywa chako. Yanaliwaza sana kwa sisi wakristo tuliochomewa makanisa na kuvunjiwa mimbali. Mungu awe pamoja nanyi. Amen
   
 7. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  waislamu na wakristo wamekua na undugu wa pamoja tangia kuja kwa mjerumani hapa Tanzania na vita vya majimaji. Lakini tangia tanznaia ilipoanzisha uhusiano wa kibalozi na Iran, hali imebadilika sana. Iran ikaanza kufadhili Balukta! na Leo hii Inafadhili mission impossible za Ponda emanuel Ponda! Sasa kwa nini wizara ya mabo ya nchi za nje inaichukia Israel vibaya sana kuliko Iran? Hivi Israel imeikosea nini Tanzania mpaka Tanzania haitaki kuweka ofisi ya Ubalozi pale Tel Aviv?
   
 8. MGANGA WA KIENYEJI

  MGANGA WA KIENYEJI JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 507
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sisi waislamu tuna wajua hawa kua ni masheikh ubwaba. Wauza sura katika vyombo vya habari. A . K. A, misters misifa. Islamu doesn not need them.
   
 9. Kakende

  Kakende JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 2,734
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Unafiki mtupu, mlikuwa wapi tangu mwanzo ambapo Mihadhara, CD zikisambazwa, Radio imani ikichochea watu. Eti mnadai mnataka usawa tanzania, eti mnaonewa. Mbona muonewe Tanzania, Kenya, Nigeria. nk? Mna nini nyie muonewe kila kona ya dunia. Hayo mafundisho yenu ya jino kwa jino, fia dini yako ndiyo yanayosababisha nchi zote zenye waislam zishindwe kufanya shughuli za maendeleo na kubaki kugharamia majeshi ili kujilinda. Endeleeni na fujo zenu tumewazoea
   
 10. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kumbe wapo Waislamu wenye hekima pia? Hii ni kauli nzuri na iliyojaa hekima!!! Lakini inatia walakini!!!! Mnafumbia macho kiini cha tatizo na baadala yake mnaparamia "side effects" za tatizo. Mihadhara na matangazo ya kashifa za kidini kupitia radio Imani inapotolewa huwa mmelala? Mbona hatujawasikia mkitoa karipio?? Hadi vurugu zitokee ndipo mjinadi????
   
 11. J

  Jajani Senior Member

  #11
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Chokochoko kama hizi za kujichukuli sheria mkononi kwa muda tangu tumepata uhuru zinaendelezwa na waislam.

  Baya zaidi zinaboreshwa na watu wenye kujifanya wana maneno ya busara na huku ndani ni mbwa mwitu wakali. Rejea mwaka huu tu Zanzibar Kanisa limechomwa na ukitafuta sababu ni uchokozi wa waislam, hamkusema kitu. Na hakuna aliyekamatwa hata washukiwa tu, jambo lipo kiiiimya kama halijatokea. Askari ameuawa kikatili na waislam wa Zanzibar, angeuawa raia yangezuka maandamano ya waislam nchi nzima.

  Hilo la mbagala ndiyo mchezo wa kuigiza na kabisa Ponda ndiyo mhamasishaji mzuri. Amekamatwa lakini atatoka na hamna kesi.
  Utasema nini juu ya watu wanaohubiri uongo kama vile matapeli wa dini yao, Mwaipopo na wengine. Ambao wameshindwa kuhubiri koran yao na badala yake huhubiri Biblia walofundishwa kinyume ili kuuharibu UKRISTO jambo lisilowezekana.

  Mimi nawashauri wote ambao ni wana wa mjakazi kuwa wanatengeneza vita wenyewe TZ ya amani iliyoimarishwa na MZEE JULIUS K. NYERERE.

  USHAURI KWA TAASISI:
  Waislam wote hubirini korani tukufu yenu kwa nguvu zenu zote na waKristo tuhubiri BIBLIA TAKATIFU kwa nguvu zetu zote.

  Bila kudanganya hamna kitu cha kuhubiri na mkihubiri Injili, ni TAKATIFU kwa hiyo mpaka MUOKOLEWE, MTAKASWE NA MPATE NGUVU ili muhubiri Injili.

  Na vurugu zenu waislam zilianza wakati wa utawala wa Mzee Mwinyi ndipo walipoinuka kina Ngariba Musa Fundi, Mwaipopo na wengine. Mwisho wao naujua ukitaka ntasema. Na sasa vurugu zinaimarishwa nanyi kwa sababu gani ?

  Waislam hubirini Korani yenu na acheni uchokozi wa kujifanya mna hasira kali, hizo kila mtu anazo ndiyo maana ana nyongo.
   
 12. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #12
  Oct 22, 2012
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  MGanga wa kienyeji makuunga mkono ila kinachonitatiza Sikuoni kwenye safu ya mbele ya jihad hii takatifu, wewe na Ritz na Zomba na Chama mnawaunga mkono huku JF lakini hampo mstari wa mbele, hampo kwenye kikosi kazi si mbagala wala kariakoo, vita yenu ni ya maneno tu kuhamasisha watu wapinge mfumo kristo, ila wachezaji wawe vijana waliochoka maisha...........


  Raha ya ngoma ni kuicheza, mpaka nikuone kwenye maandamano na harakati Ndio nitajua una nia thabiti ya kuutetea uislAm, ukinipigia kelele hapa na kutoa kejeli Kama kawaida yako, nitaendelea kupuuziA michango yako , kwAni wewe na wenzio hamuutakii mema uislAm, unahamasisha watu wewe uko kwenye shughuli zako, polisi wakisema baki nyumbNi unakaa ndani, majasiri Kama Ponda Ndio wanaingia mtaani

  Huna tofauti na Hao unaowashangaa
   
 13. Inanambo

  Inanambo JF-Expert Member

  #13
  Oct 22, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,864
  Likes Received: 1,149
  Trophy Points: 280
  hawa wanazuoni hawana uelewa lile tamko la kkkt lililoandikwa kwa kiswahili fasaha FUMBO liko wapi? Au kwa vile halikusema Wakristo walipe Kisasi. Nyie ni Wasomi msijiharibie sifa kwa Unafiki. Hamtaki Izaliwe Tanzania mpya ya Amani Upendo na Kuelewana You have no Idea jinsi MlivyoJeruhi Nyoyo za Wakristo kwa Vurugu zenu dhidi ya Makanisa yasiyohusika
   
 14. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #14
  Oct 22, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kidogo hawa wamejitahidi, Hivi Ponda ana kiwango gani cha elimu naombeni kujua wana jamvi.
   
 15. jamiif

  jamiif JF-Expert Member

  #15
  Oct 22, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 2,417
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  hao waliofanya vurugu ni wale wachache wanaotaka kuutia doa uislam. Jamani uislam ni dini ya AMANI..hivyo kwa wale ambao mna mtazamo tofauti, futeni mawazo hayo..kumbukeni kuwa kwenye msafara wa kenge hata mamba wamo..hivyo basi ndugu zangu waislam tuendeleeni kumcha Mwenyezi Mungu na kuzidi kuiombea nchi hii na zaidi hao wachache wanaotaka kuuchafua uislam waache mawazi yao hayo.
   
 16. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #16
  Oct 22, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  mmm! Shehe Mataka anasema tamko la maaskofu lilikuwa na mafumbo yanayotia hofu?! Yeye si mwanazuoni kwa nini asifumbue mafumbo hayo? Tafadhali aliye nalo alimwage hapa ili tudadavue hayo mafumbo.
   
 17. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #17
  Oct 22, 2012
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Bado tu maadui wa waislamu hawajajua nani wa kuzungumza nao katika jamii ya kiislamu ili kuleta maridhiano.Kila siku wanapoteza muda na akina Mataka.

  Inaonekana nia si kupata suluhu bali kuwasambaratisha waislamu kwa kuwagonganisha wenyewe kwa wenyewe. Heko ukoloni wa kiiengereza.
   
 18. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #18
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hapo kwenye red unamaanisha sheikh Ponda?
   
 19. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #19
  Oct 22, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Ni wale wale tu! Kwani Ponda naye si sheikh?!
   
 20. THE BIG SHOW

  THE BIG SHOW JF-Expert Member

  #20
  Oct 22, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 13,926
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  Huyo shekhe ubwabwa tuh
  sembuse idd inakairibia next wk hii sasa naona anaanza mapemaaa kujikomba komba apate mchele na viungo vya pilau,njaa mbaya sana
   
Loading...