Wanayoyafanya viongozi wa CCM wameiga alivyofanya Mh Magufuli na wanajua anayafurahia

H.T.P

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,169
1,298
Nashangaa sana mtu anaposema mawaziri na viongozi wote wa CCM wakiwemo wabunge eti wanamfitini raisi huu ni unafiki na uongo mkubwa sana.

Viongozi wote hawa wanayoyafanya kukimbia kimbia na makamera, kutoa matamko bila kutoa mrejesho, kuvunja nyumba za watu hovyo hovyo, kuzuia mikutano ya siasa, kukurupukia mambo na mengine chungu nzima.

Nimatokeo ya yale alofanya raisi wakiwa wanaona, hivyo wakajua kwamba, ili kulnda ugali wao lazima wafanye yale yatakayo isuuza nafsi yale yatakaisuuza nafsi ya mkubwa.
 
Wanaofanya kazi na rais magufuli wanasema ni mtu mwenye msimamo wake, anaingia kwenye kikao akiwa tayari na picha ya kile anachokitaka, halengi katika kumfurahisha mtu, analenga katika utimizaji wa lengo lililo mbele yake. Hivyo wale wanaojaribu kumwombea mabaya au mikosi, nadhani wanapoteza muda. Rais anasimamia katika misimamo, hatazami upepo unakwenda vipi anatazama ufanisi utakuwa ni wa kiwango kikubwa kiasi gani. Wasaidizi wake ni lazima waendane na viwango vyake, ndio maana ya kitu kinachoitwa collective responsibility, tunafanya kazi pamoja, tukifanikiwa tunachinja mbuzi na kunywa bia na soda, tusipofanikiwa kule kushindwa kunamuumiza kila mmoja wetu.
 
Back
Top Bottom