Wanawakena uongozi - I

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
14,770
10,650
Wakuu amani kwenu.

Wadau wengi wamenitaka niseme kuhusu msimamo wangu juu ya wanawake na uongozi, hasa wakitolea mifano kadhaa ya wanawake walioongoza katika zama za maandiko. Hoja hii nikiri wazi kuwa imeligawa kanisa kwa kiasi kikubwa sana, kwani wako wanaoamini kuwa katika Agano Jipya wanawake wako huru kufanya yote kama wanaume, ilhali wapo wanaoamini kwamba Mungu aliwaumba mtu mume na mke kila mmoja kwa majukumu yake tofauti. Binafsi sichagui kambi bali huyafuata yaliyo maagizo ya Mungu.

Agano la kale
Nabii Deborah hutumika kama mfano bora kwa wanawake wengi watakao kujiinua dhidi ya elimu ya Mungu. Ni kweli Deborah aliwaamua Israeli katika nyakati hizo, lakini hakuwa mfano mzuri wa viongozi wanawake. Kujua majira ya nabii Deborah tusome Isaya sura ya tatu:

𝘐𝘴𝘢𝘪𝘢𝘩 3 (𝘒𝘑𝘝)
1 For behold, the Lord GOD of hosts
is taking away from Jerusalem and from Judah
support and supply,
all support of bread,
and all support of water;
2 the mighty man and the soldier,
the judge and the prophet,
the diviner and the elder,
3 the captain of fifty
and the man of rank,
the counselor and the skillful magician
and the expert in charms.
4 And I will make boys their princes,
and infants shall rule over them.

Pale taifa linapokuwa na viongozi wa hovyo, ndipo Mungu huondoa watu wote wenye hekima, manabii, makamanda nk afu huruhusu wavulana kuwa wakuu na watoto kutawala juu ya watu. Hapa ina maana watu wenye akili za kitoto wasio na hekima watatawala na kuumiza watu. Hizi ni dalili kuwa taifa liko kwenye hukumu ya Mungu (God's judgement). Angalia aya zinazofuata:

12 As for my people—infants are their oppressors,
and women rule over them.
O my people, your guides mislead you
and they have swallowed up the course of your paths.
13 The LORD has taken his place to contend;
he stands to judge peoples.

Mungu anasema wazi kuhusu watu wake Israeli, watoto wachanga ndio wanaowakandamiza (hawa ni wenye akili za kitoto, watawala wapuuzi) na WANAWAKE NDIO WANAOWATAWALA. Sasa ingekuwa ni kawaida (natural) kwa wanawake kuwatawala wanaume Mungu asingeonyesha kuhuzunishwa ni hili. Tena akasema wazi Mungu amesimama mahali pake ili kutoa hukumu juu ya taifa lililoasi. Hukumu ni ipi? Kutawaliwa na watoto na wanawake baada ya wenye hekima kuondoshwa.

Sasa turejee nyakati za waamuzi tuone hali ya taifa la Israeli wakati wa utawala wa Deborah:

Waamuzi 2 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Kisha malaika wa Bwana alikwea juu kutoka Gilgali kwenda Bokimu. Akasema, Mimi nimewaleta ninyi mkwee juu kutoka nchi ya Misri, nami nimewaleta hata nchi niliyowaapia baba zenu; nami nilisema, Mimi milele sitalivunja hilo agano langu nililoagana nanyi;
² nanyi msifanye agano lo lote na hawa wenyeji wa nchi hii; zipomosheni nchi madhabahu zao; lakini hamkuisikia sauti yangu; je! Mmefanya haya kwa sababu gani?
³ Basi kwa ajili ya hayo mimi nilisema zaidi, Mimi sitawafukuza watoke mbele zenu; lakini watakuwa kama miiba mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa ni tanzi kwenu.

Wana wa Israeli walimwasi Mungu, ndipo alipowaambia atawatia mikononi mwa adui zao.

Waamuzi 2 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹¹ Wana wa Israeli walifanya yaliyokuwa ni maovu mbele za macho ya Bwana, nao wakawatumikia Mabaali.
¹² Wakamwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri, wakafuata miungu mingine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote, wakajiinamisha mbele yao; wakamkasirisha Bwana, akaghadhibika.
¹³ Wakamwacha Bwana, wakamtumikia Baali na Maashtorethi.
¹⁴ Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia katika mikono ya watu waliowateka nyara, akawauza na kuwatia katika mikono ya adui zao pande zote; hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao.
¹⁵ Kila walikokwenda mkono wa Bwana ulikuwa juu yao kuwatenda mabaya, kama Bwana alivyosema, na kama Bwana alivyowaapia; nao wakafadhaika sana.

Baada ya Waisraeli kutenda mabaya Mungu aliwaacha wateswe na maadui zao. Lakini walipomlilua akawainulia waamuziwaamuzi, hata hivyo waliendelea kufanya matendo maovu:

Waamuzi 2 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁶ Kisha Bwana akawainua waamuzi, waliowaokoa na mikono ya watu hao waliowateka nyara.
¹⁷ Lakini hawakuwasikiliza hao waamuzi wao, maana walifanya uasherati kwa kuifuata miungu mingine, wakajiinamisha mbele yao; wakageuka upesi, na kuiacha njia ile waliyoiendea baba zao, waliozitii amri za Bwana bali wao hawakufanya hivyo.
¹⁸ Na wakati Bwana alipowainulia waamuzi, ndipo Bwana alikuwa pamoja na mwamuzi huyo, akawaokoa na mikono ya adui zao siku zote za mwamuzi huyo; maana Bwana alighairi kwa ajili ya kuugua kwao kwa sababu ya watu wale waliowaonea na kuwasumbua.

Licha ya huruma ya Mungu, waliendelea kufanya mambo maovu na hivyo Mungu aliamsha hasira yake juu yao na akawaacha:

Waamuzi 2 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁹ Lakini ikawa, wakati alipokufa mwamuzi huyo, wakarudi nyuma wakafanya maovu kuliko baba zao, kwa kuifuata miungu mingine ili kuitumikia, na kuinama mbele yao; hawakuacha matendo yao, wala njia zao za ukaidi.
²⁰ Basi hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akasema, Kwa kuwa taifa hili wamelihalifu agano langu nililowaamuru baba zao, wala hawakuisikiliza sauti yangu;
²¹ mimi nami tokea sasa sitalifukuza taifa mojawapo la hayo aliyoyaacha Yoshua alipokufa;
²² ili kwa njia ya hayo nipate kuwajaribu Israeli, kwamba wataishika njia ya Bwana kwenda katika njia hiyo, au sivyo.
²³ Basi Bwana akawaacha mataifa yale, wala hakuwafukuza kwa upesi, wala hakuwatia katika mikono ya Yoshua.

Sasa tumtazame Deborah na utendaji wake nyakati hizo:

Waamuzi 4 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Hata alipokufa Ehudi, wana wa Israeli wakafanya yaliyo maovu tena mbele za macho ya Bwana.
² Bwana akawauza na kuwatia katika mkono wa Yabini, mfalme wa Kanaani, aliyetawala huko Hazori; na Sisera, aliyekaa katika Haroshethi wa Mataifa, alikuwa amiri wa jeshi lake.
³ Wana wa Israeli wakamlilia Bwana; kwa kuwa Sisera alikuwa na magari ya chuma mia kenda; naye akawaonea wana wa Israeli kwa nguvu muda wa miaka ishirini.

Wakatenda tena maovu, wakimwacha Mungu,naye akawatia kwenye mikono ya adui zao.

Waamuzi 4 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁴ Basi Debora, nabii mke, mkewe Lapidothi, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule.

... ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule! Wakati gani? Wakati wa uasi wa wana wa Israeli sawasawa na Isaya 3. Ni wakati ambapo taifa la Israeli lilikuwa kwenye hukumu ya Mungu. Wenye hekima na watawala, manabii waume nk waliondolewa kusudi hukumu ya Mungu isimame.

Kwa kutumia maandiko haya katika Isaya 3 unaweza kuona hata Esta, nabii Anna nk waliibuka wakati taifa la Israeli likiwa kwenye hukumu ya Mungu. Sasa huu sio mfano mzuri hata kidogo kwa wanawake wanaolilia kuongoza wanaume. Mwanamke aongozapo taifa la Mungu ni dalili za wazi kuwa taifa hilo lipo chini ya hukumu. Tutaona kwa habari ya Agano Jipya wakati mwingine.

Be blessed

Amina
 
Napita tu....
 
Back
Top Bottom