Tabia ya wanawake kuchukiana ni sijui tuseme ni nini,mfano mdogo tu hata hapa jf
kwenye segment ya 'love connect' we angalia mwanamke anapokuwa anatafuta partner na pengine ana umri mkubwa labda 30+,wengi watakao mvunja moyo ni wanawake
utaona mara,siku zote ulikuwa wapi,mara kwa umri huo labda aliyefiwa na mke wake,mara kwa umri huo huna hata mchumba si bure.
Badala wao ndio wangekuwa wa kwanza kumuelekeza na kumuinua.
Sijui kama wanawake tutaja badilika.
soraya my dear unataka kunambia hujawahi kuona jinsi wanaume wanavyowashambulia wenzao humu wanaokuja kutafuta wachumba?lol
Kwa uzoefu wangu mim,mtu akija kutafuta mchumba watu humchukulia kimasihara na wanawake kwa wanaume humuuliza maswali ya kejeli.
Naombeni mnisamehe kwa kutokubaliana na msemo wenu wa kuwa wanawake hatupendani sbb mim mwenzenu nimesaidiwa sana na wanawake wenzangu.
Nadhani mtu unachukiwa sbb ya jinsi ulivyo kwa wenzako,kama una nyodo,show off nyingi,dharau,ukipata kitu kidogo tu kazi kuwaambia wenzio mtajibeba lazima utaishia kuamini kuwa wanawake hatupendani hadi siku ya kuingia kaburini.
Tujichunguze sisi wenyewe kwanza,kwanini hatupendwi na wenzetu,ukishajua kasoro yako na ukajirekebisha na tukajifunza kuishi vizuri na wanawake wenzetu,na kujifunza kupuuza mapungufu madogo madogo ya wenzetu tukiamini kwamba hata sisi hatujakamilika na kuacha imani kuwa hatupendani lazima tutagundua kuwa kuna wanawake wenye wivu mbaya kama ilivyo kwa wanaume na kuna wanawake wenye roho ya kupenda kuona na kusaidia wenzao wasonge mbele.
Inaaminika wanaume ndio wanaochukiana zaidi wao kwa wao kuliko wanawake kwa wanawake sbb idadi ya mauaji ya mwanaume kwa mwanaume ni makubwa zaidi ya idadi ya mauaji kati ya wanawake kwa wanawake.
Pia inaaminika kwamba wanaume wanachukiana zaidi wao kwa wao zaidi ya mwanamke kwa mwanamke sbb wanaume wana sifa kama za wanyama za kuamini kwamba wanaume wengine wanaweza kuingilia territory zao wakati wowote,hivyo wanaogopana na kuchukiana.