Clayton Paul
JF-Expert Member
- Aug 22, 2022
- 2,129
- 4,393
Sio uongo wanawake wengi hawapendi waliowaoa Bali wanafurahia tu kitendo Cha kuolewa na kugawana Mali.
Kwa mwendo huu matatizo hayawezi kuisha.
Angalia tu mwenyewe we angalia tu:
✓ Pep Guradiola alimpoteza mke wake kwa sababu alilalamika kuwa alitumia muda mwingi na soka, soka lile lile lililompatia mamilioni.
✓ Roberto Carlos mali zake zote zimeenda kwa mke Yeye kabaki kulala inje Kama Mlinzi wa Santiago Bernabeu baada ya mke kufanya wanayofanya wezi wengine.
Ukumbuke huyu Ni make wa zaidi ya Miaka 20 na Wana watoto pia.
✓ Kaka aliachwa na mke wake kwa sababu alilalamika kuwa alikuwa nice man sana kwake. Katika ndoa yao yote, hakukuwa na mchezo wa kuigiza. Kaka hakuwa akiibua mabishano, hakuwa akidanganya na alikuwa akimpa umakini. Alikuwa akienda kwa likizo zote alizotaka na marafiki. Kwa sababu ya kuwa mkarimu sana, Kaka alimpoteza mke wake.
✓ De Bruyne alipoteza mpenzi wake kwa Courtois kwa sababu Courtois alimpikia mara moja. De Bruyne alimpa kila kitu na kulipia kila likizo aliyotaka. Likizo moja aliyoomba kutoka kwake kwenda Uhispania ni wakati alipompoteza kwa sababu ya Ufisi wake na Courtois .
✓ Akiwa Tajiri zaidi ya Icardi wakati huo, Lopez alipoteza Wanda kwa Icardi ambaye alimnunulia iPad. Miaka kadhaa baadaye, Wanda akamsaliti Icardi akaliwa na, Balde.
✓ Stergen alimpoteza mke wake kwa sababu mke alikuwa akimcheat na mkufunzi ambaye alikuwa akimlipa kumfundisha. Mke Alidai mkufunzi wa binafsi kwaajili ya umbo la mwili wake.
Mke ameondoka kipindi Testergen anapambana na sintofahamu yake ya kuwa nje ya uwanja na ni kipindi alimuhitaji zaidi kuoiko nyakati zote ila huyoo kaishia kwa basha ake.
Udugu Unatakiwa Kuwa Makini Huko Nje, Bado Tuna Mamilioni ya Delila Wanaoishi Kati Yetu