Wanawake wastaarabu bado wapo

Amicus Curiae

JF-Expert Member
Sep 12, 2012
4,809
6,342
Moja kwa moja kwenye mada.

Amini nawaambia kwamba, wasichana/wanawake wastaarabu bado wapo. Unaweza ukajiuliza kwanini wewe hukutani naye, hukutani naye kwasababu unatumia akili za kibinadamu kumtafuta, ukimshirikisha Mungu kwa imani yako NAKUHAKIKISHIA kwamba atakukutanisha naye.

Mimi nimeshakutana nao 3, na nakiri kwamba nimewapoteza kwa ujinga wangu mwenyewe. Nimeweka nadhiri kwamba this time around sitarudia makosa. Sitawazungumzia wale wawili wa kwanza, nitamzungumzia huyu wa 3.

Anafanya kazi kwenye shirika moja la Kimataifa. Ana Shahada ya Mining Engineering. Ni mrefu wa wastani mwenye rangi ya udhurungi, ana sura na umbo zuri na ni Mcha Mungu.

Haikuwa rahisi kumpata. Nakumbuka day one tumekutana aliniuliza maswali ambayo niliamini kwamba she is indeed very smart upstairs. Aliniuliza, Amicus Curiae, unataka mwanamke wa aina gani? Ili kama hizo sifa hana basi tupotezeane mapema tu. Nikajibu kwa kupuyangapuyanga wee , akapotezea. Maswali yalikuwa mengi hili ni mojawapo tu.

Akanitaka tena nimueleze kuhusu mimi. Nilivomuona anajielewa ikabidi nimuleze ukweli kwamba hapo zamani mimi nilikuwa mzinzi sana, na mlevi pia, lkn kwa sasa nimeamua kubadilika, akafurahi sana kwa kuwa nilikuwa mkweli.

Akaomba nimpe muda anichunguze. Aisee, she went an extra mile, kuna taarifa zangu aliniambia nikashtuka sana amezipataje! Salama yangu ni vile nilimwambia ukweli tangu awali, kwasababu alivyonichunguza aliambiwa yaleyale ya uzinzi na ulevi wangu. Mwisho wa siku akanikubali kwa sharti kwamba hatutafanya zinaa mpaka ndoa, kwa mara ya kwanza maishani NIKAKUBALI kwamba sitamfanya chochote mpk ndoa! Because I saw a WIFE in her. Akasema hataangalia madhaifu yangu ya zamani, yeye na mimi tutaanzia pale ambapo nimebadilika tunaendelea mbele.

Nikasema ngoja nimjaribu kwenye eneo la fedha, nikamuomba awe anatunza hela ya kila siku ya saluni yangu ya kiume. Kwahiyo kinyozi akawa anamtumia pesa yeye badala ya mimi. Aisee ile hela alikuwa haigusi pamoja na kumwambia kwamba akiwa na shida awe anatumia. Hata vocha alikuwa hanunui pamoja na kumshinikiza awe anatumia ile akiba. Ikifika siku ya kulipa kodi ya pango la saluni, anatoa pesa, tunalipa halafu ana-screenshot balance iliyosalia, aisee this girl was fine.

Kuna siku tukitoka anaomba alipe bills. Halafu alikua akinitoa yeye hela ananipa mimi ndiyo nilipe.

Nikamwambia nataka kulima mkonge, aisee alisapoti kuliko kawaida. Nilivyoenda kukagua shamba kwa ajili ya kupeleka trekta nikamtumia picha nikiwa shamba, nakumbuka kuna msg aliniandikia akasema "nimuandalie rainboots" na yeye anataka nimpeleke shamba! Angekuwa slayqueen ingekuwa vita!

Akaniambia yeye anapenda mwanaume ambaye ataanza naye from the scratch. Lkn pia anapenda mwanaume ambaye ni problem(s) solver; yaani mwanaume ambaye anaweza kutatua matatizo, mwanaume anayemcha Mungu na mwanaume atakayempenda kwa matendo siyo maneno.

Kuna wakati nikasema nimpime kwenye material possessions. Nikawa natoka naye napanda Bajaj badala ya kutumia gari, cha kushangaza ni kwamba alikuwa hata haulizi "gari iko wapi leo?". Kuna wadada niliwahi ku-date nao siku asipokuona na gari hata kutoka anaweza asitoke kwa hasira!

This girl ..baada ya kumpeleka kwa Mchungaji na hatimaye kwa wazazi, nikaja kuzingua tena mimi mwenyewe! Nisamehe sana 'Z', najua nimekuumiza lakini nisamehe sana. Nanyenyekea mbele za Mungu ili anisamehe pia. Usinisononekee 'Z', machozi yako yanaweza kuwa laana maishani mwangu. I thank God kwamba sijafanya zinaa na wewe kwahiyo machungu hayawezi kuwa makubwa sana. Nisamehe tena na tena.

Wanaume wenzangu nimewaletea hiki kisa hapa ili tujifunze. Asanteni.
 
Wewe uwajui wanawake huwezi mpima kwa mtazamo huo, hizo ni mbinu za wasaka kuolewa.
Shemeji yenu uchumbani alikuwa hata pesa ukimpa apokei leo hadi suruari anasachi.
Hakuna formula ya kuishi na mtu ishi jinsi atakavyokuwa.
Unaweza ukaomba Mungu akupe mke shetani akajibu maombi YAKO akakupa wa kwake.
Mwanadamu sio static ni kiumbe anaebadilika badilika. Huwezi mjua mtu ni hadi uishi nae.
Tabia zote za uchumbani zote zile ni feki sio tabia halisi.
Huwezi pata malaika bali muhimu ni kujifunza kuishi na mtu kupitia madhaifu yake.
Maana KILA mmoja uoa kwa interest tofauti
Wengine. Ngono, watoto, mwenza, mapenzi, nk.
Maisha ya ndoa ni ongoing process, talaka huja pindi shetani akichungulia future ya watoto akaona kipo kipawa lazima alete talaka Ili awawini watoto, ndoa yeyeto isiyo na mtoto mwenye kipawa shetani hawezi leta roho ya talaka.
 
Wewe uwajui wanawake huwezi mpima kwa mtazamo huo, hizo ni mbinu za wasaka kuolewa.
Shemeji yenu uchumbani alikuwa hata pesa ukimpa apokei leo hadi suruari anasachi.
Hakuna formula ya kuishi na mtu ishi jinsi atakavyokuwa.
Unaweza ukaomba Mungu akupe mke shetani akajibu maombi YAKO akakupa wa kwake.
Mwanadamu sio static ni kiumbe anaebadilika badilika. Huwezi mjua mtu ni hadi uishi nae.
Tabia zote za uchumbani zote zile ni feki sio tabia halisi.
Huwezi pata malaika bali muhimu ni kujifunza kuishi na mtu kupitia madhaifu yake.
Maana KILA mmoja uoa kwa interest tofauti
Wengine. Ngono, watoto, mwenza, mapenzi, nk.
Maisha ya ndoa ni ongoing process, talaka huja pindi shetani akichungulia future ya watoto akaona kipo kipawa lazima alete talaka Ili awawini watoto, ndoa yeyeto isiyo na mtoto mwenye kipawa shetani hawezi leta roho ya talaka.
You have said it all, mkuu. Nashukuru sana kwa mawaidha haya ya kibabe kabisa. Nimejifunza kitu. Barikiwa.
 
Formula ya kuoa oa mwanamke yeyeto mzuri machoni mwako, akibadilika badilika nae.
Key points ni kujifunza kuishi nao na sio kutafuta malaika hayupo, hata uoe sister wa katoliki aliyeacha usister dhou ni mwanadamu hawezi kuwa perfect.
Huwezi ishi bila changamoto we jini?
Uonacho chochote iwe mahusiaano, kilimo, biashara, Kazi, malezi, ndugu lazima kuna up and down. Usikimbie, ni kuangalia jinsi ya kutatua tu.
Hata walioachana waliona ni chaguo sahihi.
Key points jifunze changamoto za ndoa zisiingie kwenye mfumo wako wa maisha.
 
85564cb7-d5b7-4775-9d3d-902e337e3eb6.jpg
 
Back
Top Bottom