Wanawake wapatao 26 wa mwandikia barua papa...!

Wanawake wapatao 26 wa mwandikia barua papa...!

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,687
Kundi moja la wanawake walio na
hisia za kimapenzi na mapadre wa
kikatoliki wamemuandikia barua
kiongozi wa kanisa katoliki duniani
Papa Francis ya kumtaka kubadilisha
sheria za kanisa hilo zinazowazuia
viongozi hao wa dini kuoa.
Wanawake hao 26 kutoka Italy na
maeneo mengine wanasema kwamba
wamekuwa wakishiriki ama wanataka
kushiriki katika uhusiano wa
kimapenzi na mapadre na kwamba
wametoa ombi hilo kwa niaba ya
wanawake wengine ambao wako
katika hali kama hiyo.
Barua hiyo inazungumzia kuhusu
uchungu wa kushindwa kuishi maisha
yao kikamilifu mbali na kutaka
kukutana na papa Francis.
Papa Francis amekuwa akiunga
mkono utamaduni wa useja,lakini
mwaka 2010 aliandika akisema kuwa
huenda msimamo wake ukabadilika.
Papa francis amekuwa akimtembelea
mjane wa aliyekuwa kasisi Jeronimo
Podesta ambaye alijiuzulu katika
utumishi wake na kuoa, zaidi ya
miaka 40 iliopita.


bbc
 
Mmhhh kweli kabisa..mi mesoma shule ya masisters na walikuea wanapakuliwa na mapadre saanaa tu.so bora wahalalishe
 
Ndoa ni sakramenti!
Upadre pia ni sakramenti!
Option ipo clear,chagua kati ya haya na si mawili haya!

Hutaki ondoka !
 
Niliwahi kumsikia gombera/rector akiongea na kimada wake kwa njia ya simu.

Nilichanganyikiwa kwani jamaa alikua kioo changu katika wito wangu uliokua mchanga.

Since that day, ndoto za senior seminary zilikufa na wito ulipeperuka.

I hate that day!
 
Back
Top Bottom