Wanawake wanavyoivaa mikenge kwenye ndoa..............! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake wanavyoivaa mikenge kwenye ndoa..............!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Felixonfellix, Jul 11, 2012.

 1. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  Ngoja leo niyadadavue makosa yanayofanywa na wanawake wengi pale wanapoamua ni nani wa kuoana naye:

  1. Kosa la kwanza, unaolewa na mtu ambaye unajua kabisa ni dhaifu na mkorofi, ukitarajia kwamba ataondoa kasoro zake akiwa ndani ya ndoa. Hili ni kosa kubwa. Kama huna furaha sasa na mtu kabla hujaoana naye, usikubali kuingia huo mkenge. Huwezi kutegemea mtu kuadilika aiwa ndani ya ndoa.

  2. Kosa la pili, unaolewa na mtu asiye sahihi kwa sababu ya msisimko wa mwili kimapenzi lakini si kwa sababu ya tabia zake. Kuwa mwangalifu na neno "Nakupenda" neno hili mara nyingi maana yake ni "Nina uchu nawe." Ndiyo amevutiwa nawekimaumbile, lakini undani wa tabia yake unaujua? Hapa kuna mambo manne… Kwanza, Je anapenda kutomfanyia binadamu mwenzie mabaya kama mabavyo yeye hataki kufanyiwa? Pili, anaishi vipi na watu wengine? Anaishi vipi na watu ambao ana uadui nao, Anawasamehe au analipiza visasi? Je anatoa misaada kwa masikini? Tatu, je ni mkweli, anachokisema ndicho anachokifanya? Je anaaminika? Majukumu anayoahidi kuyafanya anayatimiza? Nne, je anajipenda? Je ni mtu ambaye yuko imara kimapenzi au ni mtu wa kuyumbayumba na asiye na msimamo? Sio mtu akishauriwa na marafiki zake au ndugu zake huko, anakuja na maamuzi yasiyo na kichwa wala miguu

  3. Kosa la tatu, unaolewa na mtu ambaye hamna malengo na vipaumbele vya aina moja vya maisha. Je mna utashi wa aina moja? Kwa mfano ni vyema mwanamuziki akaolewa na mwanamuziki mwenzie kwa kuwa anajua mzingira ya kazi ya mwenzie ili kupunguza wivu wa kupindukia usio wa lazima

  4. Kosa la nne, unaolewa na mtu asiye sahihi kwa sababu mnakutana kimwili mapema mno. Kukutana kimwili kabla ya ndoa kunaweza kuleta matatizo makubwa mno. Tendo la ndoa kabla ya ndoa hufunika uwezo wa mtu kufikiri. Mtu anabaki kufaidi na kubaki kujali mapenzi ya kimwili na kusahau kukuna ubongo juu ya mambo mengine. Ni lazima mwanamke akune ubongo ili kujua kama huyo mpenzi anakidhi vigezo vyote vya mume mtarajiwa.

  5. Kosa la tano, unaolewa na mtu ambaye huna msisimko wa kimwili umwonapo. Kuna uwezekano mkubwa mwanamke akavutiwa na mwanaume kwa sababu ya aina ya gari analomiliki. Hapa hakuna msisimko wa kimwili bali mwanamke kavutwa na gari au rasilimali alizo nazo mwanaume huyo.

  6. Kosa la sita, unaolewa na mwanaume anayependa kudhibiti. kuwa na tabia ya kudhibiti wenzako ni ya dalili za mtu jeuri na mwenye kujisikia na mfujaji. Naomba kutofautisha kati ya "kudhibiti" na "kutoa mawazo." Mtu anayekupa mawazo ni kwa faida yako, lakini anayekudhibiti ni kwa faida yake.

  7. Kosa la saba, unaolewa na mtu asiye sahihi kwa sababu unakimbia matatizo uliyo nayo. Unaweza kuwa hujaolewa na huna raha wala amani na ukataka kuolewa. Ndo haiwezi kukutatulia matatizo yako binafsi ya kisaikolojia nay a kimapenzi. Badala a kuyapunguza matatizo hayo, ndoa itayaoneza. Kama huna amani na huyafuahii maisha, chukua jukumu la kurekebisha matatizo hayo sasa kabla hujaolewa. Itakuwa ni faida kwako na kwa mmeo mtarajiwa.

  8. Kosa la nane, unaolewa na mtu asiya sahihi kwa kuwa yuko ndani ya pembe tatu. Mtu ambaye anaishi na wazazi wake ni moja ya mfano wa mtu anayeishi katika pembe tatu. Watu wengine wanaoweza wakawa wanaishi ndani ya pembe tatu ni kama wanaofanya kazi saa 24! Huyu mtu halali? Watu wengine walio katika pembe tatu ni watu wanaotumia madawa ya kulevya, mtu anayetawaliwa na "hobbie" zake, anapenda sana michezo (Mpira), kuperuzi mitandao ya kijamii na anapenda sana fedha. Hakikisha kwamba wewe na mpenzi wako , nyote hamtawaliwi na pembe tatu. Mtu ambaye anatawaliwa na pembe tatu hawezi kumtimizia mpenzi wake haja ya upendo atakapokuwa anahitaji. Kama mpenzi wako anatawaliwa na pembe tatu kwa kiasi kikubwa, wewe huwezi kuwa kipaumbele chake.

  Chanzo: utambuzi na kujitambua
   
 2. Gwamahala

  Gwamahala JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 3,568
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Duh hiyo ya pembe tatu imenifurahisha kweli!
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,407
  Likes Received: 81,437
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2012
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ....thread yako nzuri sana. Utambuzi na kujitambua. Safi sana. Pamoja na "makosa" yote yanayotokea wakati wa kuchagua mume/mke bado TUNATHUBUTU kutenda kinyume, kwa visingizio "mke mwema" hutoka kwa bwana...
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
 6. Mahmetkid

  Mahmetkid JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 557
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Ni vigumu kumpata mwanaume aliyemkamilifu kila idara, ndio maana wanathubuti kwa kutegemea kuwa utabadilika baadae.

  Tusiwaangushe madada zetu, kama yupo free kukwambia tabia hii na hile si nzuri kwako, kuwa tayari kubadilika.
   
 7. Rapunzel

  Rapunzel JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 1,089
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  me mmoja wapo nilivaa mkenge sikumpenda, ila nilipenda pesa zake na kuishi ulaya nikapigwa ndoa huyoo germany sasa simtaki hata kumsikia moyoni hayupo hata kidogo, soon tuna divorce, i can't wait....
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  he he hee but waonekana hujutii sana
  labda huwa unajiambia 'Lakini Ujerumani nimefika lol'...
  ha ha haa
   
 9. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  huyo mwenye blog aache kuiba mada za mtambuzi....:sleepy:
   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  i wish maisha yangekuwa marahisi kufanya analysis kama alivyofanya huyu.

  Kusingekuwa na divorse wala kutelekeza watoto.
   
 11. Catherine

  Catherine JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 1,263
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Dunia ya sahivi full kujilipua. Kuna wanaume washajiwekea malengo kuwa gentlemen ndani ya ndoa. Waweza mpotezea nje kumbe ni mmojawapo wa husband materials.
   
Loading...