Wanawake wanadhulumiwa kwa kubakwa

Wanawake wanadhulumiwa kwa kubakwa

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
Shirika la kutetea haki
za kibinadamu, Human
Rights Watch, limesema
kuwa makundi
yaliyojihami nchini
Somalia ikiwemo majeshi ya serikali,
yamefanya vitendo vya
ubakaji, kuwachapa na
kuwadhulumu watu
walioachwa bila makao
au wakimbizi. Ripoti ya shirika hilo
imegusia wale watu
waliokimbia vita tangu
mwaka 2011 kwa
sababu ya njaa, na sasa
wanaishi katika kambi mjini Mogadishu. Katika ripoti hiyo mpya,
shirika hilo limesema
kuwa wasimamizi wa
kambi hizo ,
wanaojulikana kama
walinzi, huiba msaada wa wakimbizi hao na
hata kuwadhulumu. Shirika hilo linasema ,
kuwa wakimbizi wa
ndani, hasa wanawake
wameripoti kubakwa
na kudhulumiwa na
watu waliovalia sare za kijeshi na wengine
wanaoaminiwa kuwa
wapiganaji wa
makundi ya waasi. Linasema kuwa baadhi
ya vitendo vibaya vya
dhuluma
walivyofanyiwa ni
pamoja na dhulma za
kingono dhidi ya wanawake na
wasichana. Kadhalika ripoti hiyo
imewanukuu
wanawake wanaodai
kubakwa akiwemo
mwanamke mwenye
umri wa miaka23 aitwaye, Quman. Anasema alikuwa na
ujauzito wa miezi, tisa
alipobakwa na kundi la
watu asiowajua ingawa
walikuwa wamevalia
magwanda ya kijeshi. Mwanamke mwingine,
Safiyo, alilazimika
kukatwa mguu wake
baada ya kubakwa na
kisha kupigwa risasi. Aidha ripoti hiyo
inasema kuwa visa vya
ubakaji haviripotiwi
sana kwa sababu ya
hofu ya wanawake
kuwa watafanyiwa unyanyapaa na
kutengwa na jamii. ''Uchunguzi wetu
umeonyesha kuwa
watu katika kambi hizo
huwekwa kama
watumwa. Hawawezi
kuondoka, walinzi wa kambi hizo wenyewe
wanafanya dhulma.
Wao huiba msaada
ambao hutolewa kwa
wakimbizi. Watu wengi
kwa sasa wanahitaji msaada wa haraka,''
ilinukuu ripoti hiyo. Human Rights Watch
pia limefichua visa vya
ubaguzi wa kikabila
hasaa kwa wale
wanaotoka katika jamii
fulani. Linasema kuwa watu wengi
wamelalamika kuhusu
visa vya kukamatwa
kiholela na hata
kudhulumiwa. Licha ya
serikali ya mpya ya Somalia kupiga hatua
bado inakabiliwa na
changamoto nyingi.

Source:BBC Swahili
 
Back
Top Bottom