Wanawake waliopitia maisha magumu hunyanyasa wasaidizi wao na watoto wa kambo

Justine Marack

JF-Expert Member
Jul 31, 2014
606
1,675
Amani iwe kwa wote wana MMU.

Ni mara chache sana naweka mada jukwaa hili kwa sababu ninazingatia kuwa ni vema kuwa na jambo lenye mashiko na sio kuandika lolote jambo.

Nimejaribu kuchunguza katika jamii zetu tunazoishi hasa kwa wanawake waliowahi kupitia maisha magumu na baadae kufika hatua flani ya maisha yenye ahueni kidogo au sana.

Maisha niliyochunguza ni yale ya pangu pakavu (kutokea familia za ukapuku), katika jamii hii ndiko wanakotoka hawa wadada wa kazi au kama tunavyowaita housegirl au house maid na wengine tunapunguza ukakasi kwa kuwaita wasaidizi.

Wanawake waliopitia maisha haya ikitokea ameolewa na kuishi maisha ya kitajiri au akipata uwezo wa kumiliki housegirl, huwa wanasahau kabisa kama walipitia maisha hayo na ndio wanaoongoza kwa kuwatesa wadada wa kazi na watoto wa kambo.

Tafadhali kwa yeyote aliyewahi kugundua hili unaweza ku share nasi ili tutafakari kujua sababu.

Nawasilisha..
 
Sipingi utafiti wako mkuu, ila ujue ni kazi sana mtu kutoa au kukupa kitu asichokua nacho. Wengi unaowasema hawajapitia maisha ya kujaliwa kupendwa, wame experience manyanyaso na ukatili sasa unategemea nini kutoka kwao?

Hali kadhalika ukimpa cheo mtu aliyeishi maisha ya umaskini ghafla inaweza kuleta shida japo sio mara zote.
 
Hiyo ya pili nakubaliana nayo kabisa, Mtu alopitia maisha magumu au umasikini walio wengi ukuwapa cheo huwa vimeo yaani njaa njaa,kujikweza na unoko mwanzo mwisho. Asante ka kunikumbusha hilo.
 
Back
Top Bottom