Wanawake walilia faragha na waume zao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake walilia faragha na waume zao

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Raia Fulani, Mar 8, 2010.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,217
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  WANAWAKE wanaoishi katika makambi ya waathirika wa mafuriko Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, wamesema wanahofu kubwa juu ya kuvunjika kwa ndoa zao kutokana na kutengwa na waume zao kwa muda mrefu kufuatia adha ya mafuriko iliyowakumba mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu.

  Wakiongea na HabariLeo jana, katika kambi ya Mazulia (mojawapo ya kambi zinazowahifadhi), waathirika hao walisema hofu hiyo imekuja baada ya kutengana na wazazi wenzao tangu mwezi Januari mwaka huu hadi sasa.

  Walisema makazi yao ya sasa hayaruhusu faragha inayostahili. Wanawake hao walisema wanaishi familia nne katika hema moja hivyo kuwalazimu kuishi wanawake pamoja na watoto wao wa kike peke yao , huku waume zao wakiishi katika mahema mengine na watoto wa kiume.

  Wamesema hali hiyo imekuwa ikiwaathiri sana kisaikolojia kutokana na mazoea ya hapo awali ya kuishi na wazazi wenzao pamoja, na kueleza kuwa hali hiyo imekuwa ikiwakosesha raha kutokana na kuingiwa na hofu ya kuhatarisha ndoa zao.

  " Tangu tumehamia kwenye haya mahema tumekuwa na mawazo sana juu ya hizi ndoa zetu…tutaishi hivi hadi lini, maisha haya kwa kweli ni magumu sana , japokuwa serikali inajitahidi kutupatia chakula, lakini ndoa zetu zipo matatani" walisema.

  Walisema licha ya kuhofia kuporomoka kwa ndoa hizo, pia wamekuwa na hofu kubwa ya kupata magonjwa ya zinaa ikiwa ni pamoja na kupata maambukizo mapya ya virusi vya Ukimwi kutokana na wanaume hao kupata nafasi ya kutoka nje ya ndoa zao kutokana na visingizio vya kuishi tofauti na wake zao.

  "Kama unavyojua hawa wakina baba kipindi hiki kwao wanaona ni neema, kwa kuwa wana uhuru wa kuzurura na kurudi kwenye mahema muda wanaotaka kwa kuwa hatupo nao, wanafanya maamuzi yao, jambo ambalo ni hatari sana linaweza huko baadaye likatuletea magonjwa ya zinaa hata maambukizi ya Ukimwi" walisema kwa masikitiko.


  Wanawake hao walisema kutokana na adha hiyo ya mafuriko hivi sasa gharama za nyumba za kupanga zimepanda mara mbili, na kueleza kuwa chumba cha bei ya shilingi elfu tano hivi sasa ni shilingi elfu kumi, huku bado kukiwa na uhaba mkubwa wa nyumba za kupanga.

  Waliongeza kuwa kutokana na kupanda gharama za nyumba hizo, ili hali wakiwa na kipato kidogo wanalazimika kuendelea kuishi kwenye mahema hayo ili kuweza kupunguza gharama zaidi za maisha.

  Wakizungumzia juu ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo ilianza tangu Machi mosi, walisema hawawezi kuifurahia siku hiyo kutokana na matatizo yanayowakabili hususani katika kipindi hiki kigumu ambacho wamelazimika kutengana na wazazi wenzao kufuatia adha hiyo ya mafuriko.

  Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Kambi hiyo Said Madogoya alisema imelazimu familia hizo kuishi kwa mtindo huo kutokana na uhaba mkubwa wa mahema unaowakabili, na kueleza kuwa mahema hayo yasingetosha kuhifadhi familia moja katika kila hema kutokana na uchache huo.

  Kambi hiyo ya Mazulia ina idadi ya mahema 744 yaliyojengwa, ikiwa ni sambamba na vyumba 57 vilivyogawanywa ndani ya kiwanda cha Mazulia.

  Huku wanawake wengine duniani leo wakiadhimisha sikukuu yao, wanawake wa Wilaya ya Kilosa wataingia wakiwa na dhiki kubwa za kifamilia.

  maoni yangu
  kumbe hata amid crises kama hizi bado wanandoa/watu wanakumbuka hii kitu? Mungu watimizie haja ya mioyo yao na kuwafanya hao waume zao wasiruke hovyo hovyo. Amen!
   
 2. Sydney

  Sydney Senior Member

  #2
  Mar 8, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwanza natoa pole zangu kwa wanawake hao, jamani poleni sana! Na pili naomba niseme ninachowaza, nimesoma imesikitisha sana, lakini nimekaza moyo na kuandika maana inanihusu kwa kiasi fulani maana ni wanawake. Na leo ni siku ya wanawake duniani. Hivi serekali ya chama tawala iko wapi? Na kama sikosei uchaguzi mkuu ni siku kadhaa zijazo sio mwakani ni mwaka huu huu, ina maana wanawake itafika kipindi watakuwa na hamu hata ya kuchagua kiongozi mwanaume kweli? Licha ya hayo matatizo yanayowaangalia usoni ya kuishi mbali na waume zao, na magonjwa ya kuambukiza. Hivi jamani ubinadamu uko wapi? kweli nimesikitika sana. Lakini nawaomba wawe wavumilivu maana mungu hamtupi mja wake, na atawanusuru na hilo! mwisho natoa: HERI YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI, kwa wana JF woooooote! wake kwa waume!
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,217
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  kwa kilio hiki wangewajengea eneo maalum la kukutania na kukidhi hamu zao basi. hii ntawaondolea msongo na hofu walizo nazo juu ya wenza wao. hadi kutoa kilio hiki, ujue wamefikia ukomo
   
 4. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kweli kabisa.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...