Wanawake wa Mitandaoni (Online Girls)

Pia chagua jibu moja kati ya haya unaloona lina nguvu zaidi kuliko hayo mengine

  • Online chats huweza kumpatia mtu mume/mke/mchumba

    Votes: 2 15.4%
  • Online chats ni hatari huweza ukampata mtu mwenye mahusiano mengi au magonjwa hatari kama HIV

    Votes: 7 53.8%
  • Online chats huweza kumpatia mtu rafiki mzuri wa kubadilishana mawazo

    Votes: 4 30.8%

  • Total voters
    13
  • Poll closed .

Udakuzi

New Member
Apr 29, 2013
3
2
Habari za Asubuhi wadau wa MMU!

Kutokana na maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano (teknohama) pamoja na utandawazi, inazidi kuwa rahisi sana kukutana na mtu wa aina yeyote yule unaemhitaji. Kwa wale ambao wanataka wapenzi, watu wa kufanya nao biashara, watu wa kubadililshana mawazo ya kidini, marafiki, etc. imekua rahisi sana kuwapata.

Nataka nigusie zaidi kwa upande wa wapenzi na hasa wanawake wanaopatikana kwa njia za kielektroniki na kimtandao (online). Mitandao hii inazidi kuwa maarufu kwa hapa Tanzania ambayo wanawake na wanaume wanaotafutana hukutana (dating sites). Mimi pia kutokana na vishawishi vya hapa na pale nimewahi kuonana na wanawake kadhaa kutoka kwenye hiyo mitandao.. Sasa nina mambo kadhaa amabayo nimeyagundua napenda niwashirikishe.

1. Wengi wao hutoka katika vyuo vikuu hasa CBE, Tumaini, KIU na baadhi ni waliomaliza form four ambao wako tu nyumbani hawana kazi au wanasubiri matokeo.
2. Wengi wao pia huwa mitandaoni kwa malengo makuu mawili, kutafuta mwanaume mwenye hela wa kuwaweka mjini au hawana mwanaume so wako desperate kutafuta mtu wa kuwa nae.. cha ajabu ni kwamba pia wapo wachache ambao wanapenda kuwa na wapenzi wengi tu bila sababu, wanafurahia hilo.
3. Kinachoshangaza zaidi ni kuwa wengi wao wako tayari kutembea na wewe hata kesho yake tu, pia wengi wao hawapendi kutumia kondomu wanapokutana na watu wao. Hii inamaanisha nini?
4. Pia wengi wao wako tayari kutembea au kuwa na uhusiano na mwanaume yeyote, awe ameoa au ana mchumba wako tayari tu hamna shida.

Sasa kutokana na observations zangu za hapo juu napenda kuwauliza wana MMU, tatizo liko wapi? je, ni kwamba hao wanawake wanaokuwa online kuchat huwa wengi wao wanaingia kwa malengo maalumu kama ambavyo wanaume wanaowatafuta wanavyochat nao kwa lengo maalumu?
 
Pole kwenu mnaouziwa mbuzi ndani ya gunia

Funguka zaidi, unamaanisha kuwa wengi wa unaokutana nao wametulia kuliko wale ambao hawajatulia? au ni una bahati tu ya kukutana na watu wazuri online?
 
Kwa nini uhangaike kutafuta mtu online wakati offline wamejaa tele...
Huo utaratibu at first katika ulimwengu wa ICT uliwekwa kwa ajili ya mingling between people of different cultures...
Kama unataka kupata mtu anayekidhi vigezo, ni vyema kutotumia mitandao

Funguka zaidi, unamaanisha kuwa wengi wa unaokutana nao wametulia kuliko wale ambao hawajatulia? au ni una bahati tu ya kukutana na watu wazuri online?
 
Kwa nini uhangaike kutafuta mtu online wakati offline wamejaa tele...
Huo utaratibu at first katika ulimwengu wa ICT uliwekwa kwa ajili ya mingling between people of different cultures...
Kama unataka kupata mtu anayekidhi vigezo, ni vyema kutotumia mitandao

umemjibu vizuri sana mkuu.
 
na wanafanya hivyo kwa sababu wanajua kwamba watawapata watu kirahisi.... ila jamani inakuwaje unawasiliana na mtu humjui mnapanga kukutana mpaka mnaishia kufanya mapenzi siku hiyo hiyo ... hivi ni tamaa au ni pepo? Mungu atusaidie
 
Sioni mantiki ya mtu kuingia mtandaoni na kuanza kutafuta mtu ukiwa na mategemeo atakuwa gf au bf wako na mkaendana kweli, mbaya zaidi anaekubali siku hyo hyo ya kwanza. Bila shaka hapo mtafutaji na mtafutwaji wako katika kundi moja na nia moja.#kugegedana101
 
Mimi wangu nimempata humu humu JF..! Na tunaendelea vizuri kabisa na mahusiano yetu..!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom