Wanawake wa hivi ni wachache sana, wengine wamepotelea wapi?

Wanawake wa hivi ni wachache sana, wengine wamepotelea wapi?

Mwifwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2017
Posts
48,777
Reaction score
126,726
Katika vitu vinavyojenga ndoa imara, upendo ni mojawapo ya vitu hivyo.

Upendo sio uwe baina ya wanandoa tu, bali hata kwa jamii inayokuzunguka.

Upendo kwa wazazi wenu ninyi wanandoa ni muhimu sana.

Kuna baadhi ya wanandoa wanapendana wao lakini unakuta mmoja wa wanandoa hawapendi wazazi wa mwezi wake au wazazi wake.

Mathalani, mke hawapendi wazazi wa mume wake na kinyume chake.

Kuna wanawake wachache sana ambao wanaweza kumkataa mwanamme kisa tabia zake sio nzuri japo ana utajiri mkubwa.

Unakuta mwanaume kajitajidi kutafuta mali na kafanikiwa kuipata lakini kutokanana na haiyo mali yake anapoteza mapenzi wa wazazi wake, anacha kuwathamini kabisa, wengine wanasaidiwa na wazazi kwa nna moja au nyingine kupata mali ila wakipata wanawasahau wazazi wake.

Kuna wanawake wachache sana wanaoweza kuwakataa wanaume wa namna hii endapo wakitaka kuwaoa. Kuna hekima kubwa sana katika haya maamuzi.

Lakini kwa sasa ni nadra sana kupata mwanamke wa hali hii maana 900 huwa inapendeza sana kwenye upendo bila kuzingatia mengine......

Mapenzi ya kweli hudumu ila pesa zinaisha kwa sekunde tu.
 
Ubepari ndio umesababisha.
Ujima tumewaachia mama zetu.
 
Ila wanaume msikuze mambo jamani, there is a person for every one. Wanawake mbona wanawapenda tu na hali zenu na mnawaoa? Maana ndoa nyingi zinazofungwa ninazozishuhudia ni za wenzangu na mie tu. Au mnataka wanawake gani???
 
Back
Top Bottom