Wanawake wa hii mikoa, nawapa hongera sana

Nimecheka kwa mara ya kwanza. Ila naomba nitofautiane kidogo au nichangie mawazo yangu. Sijui TFDA wametumia factor gani. Hiyo mikoa inayoongoza inawafanyabiashara wengi hasa wajasiliamali inawezekana kabisa walinunua stock kubwaukilinganisha na wengine. Pili weusi wao ni Ule wa Sudan haukubali mkorogo hivyo ni rahisi kuwa sample. Hawa wengine wanatumia mikorogo kuongeza rangi zao. Kwa utafiti wangu wa macho DSM wangeongoza ni manjano ndiyo yanawafichia siri. ACHEN jamani ni kuendeleza utumwa.
 
Salaam Jf!

Baada ya kuiona ripoti ya TFDA inayohusu mikoa inayoongoza kwa kujichubua, nimegundua kuwa mikoa ya kaskazini ina viwango vidogo sana vya matumizi ya kemikali hizi zinazoharibu ngozi. Mikoa hii iko chini ya 3% huku njombe na Mbeya wakiwa na viwango vikubwa sana vya wanawake wanaojichubua wakiwa ni asilimia 9, kwa 14.

Mikoa hii ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro naipongeza sana kwa kuwa na kiwango kidogo sana cha matumizi ya kemikali hatari kwa ngozi na kuwafanya wanawake kuwa katika hali zao za asili. Aidha, Dodoma na Tanga nao wapo vizuri

Kwa Tanzania visiwani, nadhani kule ndio wanawake hawajali kabisa kuhusu kujichubua, hongereni sana!!

Mikoa mingine hii inatisha maana mingi iko 4% na kuendelea wakiongozwa na.kinara Mbeya na njombe
Mwanamke mweupe pepee wa Manyara na huko Machame juu, achichubue aweje sasa, muzungu?
 
Back
Top Bottom