Wanawake wa hii mikoa, nawapa hongera sana

Value

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
252
402
Salaam Jf!

Baada ya kuiona ripoti ya TFDA inayohusu mikoa inayoongoza kwa kujichubua, nimegundua kuwa mikoa ya kaskazini ina viwango vidogo sana vya matumizi ya kemikali hizi zinazoharibu ngozi. Mikoa hii iko chini ya 3% huku njombe na Mbeya wakiwa na viwango vikubwa sana vya wanawake wanaojichubua wakiwa ni asilimia 9, kwa 14.

Mikoa hii ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro naipongeza sana kwa kuwa na kiwango kidogo sana cha matumizi ya kemikali hatari kwa ngozi na kuwafanya wanawake kuwa katika hali zao za asili. Aidha, Dodoma na Tanga nao wapo vizuri

Kwa Tanzania visiwani, nadhani kule ndio wanawake hawajali kabisa kuhusu kujichubua, hongereni sana!!

Mikoa mingine hii inatisha maana mingi iko 4% na kuendelea wakiongozwa na.kinara Mbeya na njombe
 
Jamani halafu hawaTFDA hawajakosea kabisa, kwani hili suala linakera kweli, ila hawa viumbe ni wabishi hata kama wawe wamesoma vipi, mtu msomi kabisa na ni mkeo wa ndani kabisa hata umwambie vipi mtabishana mpaka atakuharibia siku, ili mradi tu aendelee na mambo yake ya kujipaka michubuo.
 
Hapa ndipo lilipo anzia tatizo.
Eee Mungu msamehe huyu ni binadamu mwenzetu
anaye kukosoa.

FB_IMG_1546770748354.jpeg



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom