Wanawake tutambue thamani yetu

Doris Gabriel

JF-Expert Member
Jul 30, 2017
1,045
869
Habari wana JF,

Naimani wote muazima kwa uweza wa mwenyezi Mungu,

Jamani kama nilivoelezea hapo juu wanawake wenzangu ebu tuitambue thamani yetu sisi kama sisi jamani kiukweli tukianza katika mavazi jamani wanawake tunajiachia sana katika mavazi mwanamke unavaa nguo fupi inaonyesha maungo yako ambayo hayapaswi kuonekana.

Nje hovyo anaestaili kuyaona ni mumeo aliekuoa ndio maana wanaume wanatuzarau sana na tunajidanganya kuvaa nguo za kuonyesha maungo yetu sio kwamba ndio tunafanikiwa kupata mume tutaishia kufunuliwa na kuachwa pia hata ukiolewa utaolewa na mwanaume mwenye akili kama zako huwezi kuolewa.

Na anaejiheshimu wakati wewe hujiheshimu kuna hii imezuka wanawake kutuma maungo yao mitandaoni kwa wanaume msiowajua hata kama unamjua jamani hivi kabisa unakaa unavua nguo unajipiga picha unamtumia mwanaume ujue moja kakuomba umetuma hapo tayari kakuzarau pia umeshindwa kuheshimu utu wako hivi akisambaza mitandaoni siku ya siku zikawafikia wazazi, ndugu, jirani si ni aibu kwa familia jamani ebu tujue thamani zetu.

Pia kuna hii mwanamke unatongozwa asubuhi jioni ushatoa jibu umekubali hata kumpa ugumu gumu mwanaume na yeye anakuchukulia mrahisi hivyo hivyo mwanaume anapenda kusumbuliwa ninachoomba wanawake tujiheshimu turudishe heshima yetu pia tujitume tusipende kuomba omba pesa kwa wanaume kuwageuza vitega uchumi kukusaidia ni wajibu wake.

Ila muache yeye atambue wajibu wake labda uwe umebanwa kweli mpaka ata ukimuomba anashangaa hata kukopa atakopa atajua kweli mpaka kaomba anashida tutambue mwanaume huyo anawazazi pia lazima awakumbuke kwa chochote tena ukitaka kumteka unamwambia bebi umetuma hela kwa wazazi mwanaume ukipenda wazazi wake, familia yake kiujumla, rafiki zake hapo umemloga tosha hata ikitokea mnaachana unakuta unapendwa na wazazi wake , marafiki, tunapokuwa na wanaume zetu tuwachangamshe katika mawazo yakutafuta pesa kujiajili kumpa hamasha sasa.

Mwanamke jamani wewe unataka akutunze wewe tu jamani asikumbuke waliomleta duniani wakamsomesha mpaka hapo akapata hiyo kazi inayompa riziki sometimes wanawake tunasababisha wanaume waangaike kimaisha kwamanunguniko yawazazi wake kwahiyo hata kuomba omba kunakushusha thamani kwa mwanaume hivi sijui mimi mshamba ile unatoka kulala.

Na mwanaume unamuomba pesa hakiya Mungu jamani aibu mwanaume ataisi unajiuza muache akupe yeye kama unajijua huna nauli mwambie ukiwa kwenu baby siwezi kuja sina nauli atakuwa nauli yaani ili ukifika unajua huna nauli ya kwenda na kurudi ujue ndio maana wanaume wanasema bila pesa hakuna mapenzi hii imeletwa na sisi wanawake kutanguliza pesa mbele kuliko upendo hii inafanya mapenzi kuzalaulika.

Nachoomba wanawake tubadilikeni pia kuna mda tumkumbuke Mungu pia itasaidia.

Wanawake hii mada najua kuna wanawake watakao nisema vibaya ila ilihali nimeongea ukweli wakutujenga sisi wanawake na kutukumbusha thamani yetu.
 
Ni sawa wanawake mnatakiwa mtuzungushe kidogo msitukubali haraka tatizo kuna vidume vimejaliwa midomo mitamu balaa

Yaani kwa jinsi mtu alivyo na mdomo mtamu kwa sound zake utahisi ukimzungusha utakuwa umepoteza Almasi kwa kuifananisha na chupa
 
Ni sawa wanawake mnatakiwa mtuzungushe kidogo msitukubali haraka tatizo kuna vidume vimejaliwa midomo mitamu balaa

Yaani kwa jinsi mtu alivyo na mdomo mtamu kwa sound zake utahisi ukimzungusha utakuwa umepoteza Almasi kwa kuifananisha na chupa

Ila hapo kwenye kumpa ugumu ugumu mwanaume personally sipapendi, mm demu akinikataa Mara moja ndo kwaheri, half mademu wanaokuaga wagumu mwanzoni, Mara nyingi hawanaga mapenz ya kweli, speaking from my experience
 
Ahsante kwa ukumbusho my mdogo

Ila usisahau katika maisha tunayoishi kila mmoja amepitia malezi ya aina tofauti tofauti hivyo unaweza kitu ukakiona cha ajabu na hakifai ila mwingine akakiona kwa upande wake kipo sawa kabisa na kwa mtu wa hivyo hawezi kukuelewa hata iweje.

Ila kwa asilimia fulani ujumbe umefika.
 
maelezo mazuri

ila ila pesa zake usimpangie maisha.

haya mambo ya kumcontrol mtu nawakati yupo kwake nivigumu mno.

kilichobaki ni kujionea maonesho ya miili tu sikuizi.
 
Maungo gani yanayo onekana?
Mwanamke ni papuchi na maziwa ndiyo hayapaswi kuonekana.

Lkn mapaja, sijui tumbo hvyo ni vitu vya kawaida sana.
Tatizo African tunaendekeza Ngono sana, na pengine hatujazoea, lkn km mtu umeishi Nchi za kibepari, huwezi andika uzi km huu.
 
Ni sawa wanawake mnatakiwa mtuzungushe kidogo msitukubali haraka tatizo kuna vidume vimejaliwa midomo mitamu balaa

Yaani kwa jinsi mtu alivyo na mdomo mtamu kwa sound zake utahisi ukimzungusha utakuwa umepoteza Almasi kwa kuifananisha na chupa
Ni kweli hata shetani alianza kumdanganya Hawa sawa ila tunapaswa kuwa jasiri Mimi hata uje umesomea kunitongoza sisubutu kukubali sikuhiyohiyo
 
Ila hapo kwenye kumpa ugumu ugumu mwanaume personally sipapendi, mm demu akinikataa Mara moja ndo kwaheri, half mademu wanaokuaga wagumu mwanzoni, Mara nyingi hawanaga mapenz ya kweli, speaking from my experience
Ukiona mwanaume unamzungusha anakata tamaa huyo alikuwa nia yake aguse asepe
 
Ahsante kwa ukumbusho my mdogo

Ila usisahau katika maisha tunayoishi kila mmoja amepitia malezi ya aina tofauti tofauti hivyo unaweza kitu ukakiona cha ajabu na hakifai ila mwingine akakiona kwa upande wake kipo sawa kabisa na kwa mtu wa hivyo hawezi badilika hata iweje.

Ila kwa asilimia fulani ujumbe umefika.
Dada nimekubaliana nawewe kweli malezi tofauti tofauti ndomana tunakuwa tofauti
 
Safi sana wanawake kama wewe ni wachache sana, acha kina miss chaga maana jana nimeona anawapotosha wenzake sijui watumie kondomu, sijui waombe pesa..
 
Back
Top Bottom