Wanawake tunapenda Kupendwa, Kuheshimiwa, Kuthaminiwa, kusikilizwa,Kusifiwa, kuhudumiwa na mambo mengine mazuri kama hayo.
Kuhusu kupendwa
tunapenda upendo unaoonekana kwa vitendo, hususan uvumilivu wakati wa shida, na upendo wa kweli huondoa hofu na tunakuwa huru zaidi Na mwanamke aliye huru ndiye anang’ara zaidi.Halafu anakuwa sio mchoyo😜.
Kuheshimiwa mbele za watu na hata faraghani.Maoni yetu yawe na uzito. Tukiheshimiwa, ujasiri wetu unaongezeka. Na mwanamke mwenye ujasiri anajenga familia vizuri.Usitegemee kuheshimiwa kama hujisheshimu na huheshimu wengine.
Kuthaminiwa na kuwekwa kipaumbele hususan mbele ya watu. Kuchaguliwa sisi kwanza. Juhudi zetu pia ziheshimiwe
Tukijua sisi ni kipaumbele, tunafurahi na tunafanya bora zaidi bila kulalamika hususan kitandani.
Kusikilizwa. Mwanamke wakati mwingine anapitia changamoto nyingi huenda Kila mtu anaweza kumlaumu lakini ni vizuri akasikilizwa kwa upole na kueleweka kisha akapewa ushauri.Tukisikilizwa, mioyo yetu inatulia. Na moyo uliotulia unazaa mawazo mazuri.
Tunapenda kusifiwa mfano "Umejitahidi." "Umevaa vizuri." "Nimekuona umependeza” umepamba nyumba vizuri.
Sifa ndogo inaamsha Ile hali ya kuendelea kupenda na kuvumilia. Inatupa nguvu ya kujitahidi zaidi kila siku.
Kukumbatiwa. Tunapenda sana kwa sababu kunaponya uchovu wa siku nzima na kutoa faraja kwa mwanamke na kumfanya ajisikie vizuri.Kukumbatiwa kunatoa uhakika wa kuonyesha kuwa "nipo nawe". Hapo ndipo tunapopata nguvu ya kupambana tena.
Tunapenda kuhudumiwa.Mfano kununuliwa zawadi ndogo ndogo na hata kubwa. Mfano Nguo za ndani,Saa,Gauni,Viatu, Kupelekwa sehemu nzuri kupumzika, Pesa kidogo ya matumizi na vitu kama hivo. Tunapenda pia kuulizwa "Umekula?" "Umelala?" "Nikusaidie nini?
Huduma ni lugha ya upendo. Inatufanya tujisikie salama na kutunzwa.
Tunapenda ushirikiano,Mfano Katika malezi ya watoto kupeleka mtoto clinic,shuleni na kusaidiana kazi ndogo ndogo za nyumbani.
Mwanamume anaposhuka na kushiriki, mzigo unapungua. Na mwanamke asiyechoka ndiye anang’ara na kunawiri vizuri.
Kuhusu pesa si kipaumbele sana kwa mwanamke kama kutakuwa na upendo, heshima, ushirikiano na uwajibikaji.
Mpe mwanamke upendo, heshima, kipaumbele na ushirikiano. Utashangaa jinsi atakavyonawiri na katika nyumba yako upendo na amani vitatawala.
Huenda uzeeni ndio watu wanaishi vyema, maana huku ujanani mambo ni mengi sanaa, inakuwa mbanano mkali hadi unshindwa ushike kipi uaache kipi 😁Siipendi hii picha.
Umeanza lini haya mambo?
Unaonekana wewe ni mwanaume unaejali.Aiseeee...... mwanamke wangu ni mwendo wa mpera mpera !
Akiomba kitu kama sina ni sina yani .... hakuna maelezo na ataelewa ......
Mama mzuri kwa familia..... hilo najivunia....hata nikisafiri najua home pako salama na mishe zetu zinasonga kwa usimizi wake !
Namshukuru Mungu kwa hilo
Kujidai unapenda changamoto kwa kuangalia tu bila positive reaction ni uhuniuhuni tu.🤝 Napenda Challenge
Nani kasema ni shindano?Hii ni nipe nikugee!Haya sio mashindano.
Ni mahaba.
Mimi nasema jinsia tunayosimama tukiwa tunatoa haja ndogo, tujithamini, tujiheshimu na kujijali zaidi. Hii ni by experience.Wanawake tunapenda Kupendwa, Kuheshimiwa, Kuthaminiwa, kusikilizwa,Kusifiwa, kuhudumiwa na mambo mengine mazuri kama hayo.
Kuhusu kupendwa
tunapenda upendo unaoonekana kwa vitendo, hususan uvumilivu wakati wa shida, na upendo wa kweli huondoa hofu na tunakuwa huru zaidi Na mwanamke aliye huru ndiye anang’ara zaidi.Halafu anakuwa sio mchoyo😜.
Kuheshimiwa mbele za watu na hata faraghani.Maoni yetu yawe na uzito. Tukiheshimiwa, ujasiri wetu unaongezeka. Na mwanamke mwenye ujasiri anajenga familia vizuri.Usitegemee kuheshimiwa kama hujisheshimu na huheshimu wengine.
Kuthaminiwa na kuwekwa kipaumbele hususan mbele ya watu. Kuchaguliwa sisi kwanza. Juhudi zetu pia ziheshimiwe
Tukijua sisi ni kipaumbele, tunafurahi na tunafanya bora zaidi bila kulalamika hususan kitandani.
Kusikilizwa. Mwanamke wakati mwingine anapitia changamoto nyingi huenda Kila mtu anaweza kumlaumu lakini ni vizuri akasikilizwa kwa upole na kueleweka kisha akapewa ushauri.Tukisikilizwa, mioyo yetu inatulia. Na moyo uliotulia unazaa mawazo mazuri.
Tunapenda kusifiwa mfano "Umejitahidi." "Umevaa vizuri." "Nimekuona umependeza” umepamba nyumba vizuri.
Sifa ndogo inaamsha Ile hali ya kuendelea kupenda na kuvumilia. Inatupa nguvu ya kujitahidi zaidi kila siku.
Kukumbatiwa. Tunapenda sana kwa sababu kunaponya uchovu wa siku nzima na kutoa faraja kwa mwanamke na kumfanya ajisikie vizuri.Kukumbatiwa kunatoa uhakika wa kuonyesha kuwa "nipo nawe". Hapo ndipo tunapopata nguvu ya kupambana tena.
Tunapenda kuhudumiwa.Mfano kununuliwa zawadi ndogo ndogo na hata kubwa. Mfano Nguo za ndani,Saa,Gauni,Viatu, Kupelekwa sehemu nzuri kupumzika, Pesa kidogo ya matumizi na vitu kama hivo. Tunapenda pia kuulizwa "Umekula?" "Umelala?" "Nikusaidie nini?
Huduma ni lugha ya upendo. Inatufanya tujisikie salama na kutunzwa.
Tunapenda ushirikiano,Mfano Katika malezi ya watoto kupeleka mtoto clinic,shuleni na kusaidiana kazi ndogo ndogo za nyumbani.
Mwanamume anaposhuka na kushiriki, mzigo unapungua. Na mwanamke asiyechoka ndiye anang’ara na kunawiri vizuri.
Kuhusu pesa si kipaumbele sana kwa mwanamke kama kutakuwa na upendo, heshima, ushirikiano na uwajibikaji.
Mpe mwanamke upendo, heshima, kipaumbele na ushirikiano. Utashangaa jinsi atakavyonawiri na katika nyumba yako upendo na amani vitatawala.
Mabahili na wakatili wasiuone huu uzi
Mgongoo unachokaaa, bora kucheza na kambare wangu mashambani.. Mapenzi ni Options ( mnapokeana mnavyokutana ) 😅Umekata tamaa mapema sana 😝
Nawaona nawaona akina bamtuMabahili tupo hapa