Wanawake ndoa ni zaidi ya mnavyoelewa

Wanawake ndoa ni zaidi ya mnavyoelewa

Innocent Kirumbuyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2014
Posts
4,647
Reaction score
4,495
Kati ya 100% ya wanawake ni 15% tu ndio hujua wajibu wa ndoa zao ni wajibu wa nini maana ya kuitwa mke wa mtu. Lakini hii 85% hawa wote hujua ili kuwa mke wa mtu lazima utimize haja za kimwili kwa mumeo.

Ni 5% ya wanaume kati ya 100% hawa nao huoa kwa ajili ya kutimiza haza za miili yao,hawa nao huwa ni wale wanaume wasiojielewa ambao huwa hawawezi kutumia akili badala yake hutumia sana miili yao

Kuwa mke wa mtu si kwamba umeolewa kwa lengo la ngono hapana maana hata mbuzi wanafanya ngono ila hawaoani.

Kuna kitu zaidi ya ngono ambacho wanawake wengi wa siku hizi hawakijui,kuna wanawake ambao hawa huwa wamejiweka tayari kwa kutumiwa kimwili, na hawa ndio husema kuwa "nyumbani nilikuwa nakula, navaa, naoga, na kufanya kila kitu ila kuna kilichonileta kwako "kwa maneno haya hubainisha kabisa kuwa mwanamke huyu kaja kwa lengo flani kama si pepo la ngono basi ni jini mahaba.

Lakini kama wewe ni mwanamke na ni mmoja kati ya wanawake unayejielewa, basi lazima ujue kuwa kuna kitu unatakiwa ufanye kwenye ndoa yako zaidi ya ngono kwasababu uzuri ulionao kwa sasa ipo siku utakwisha na hapo ndio utakapokumbuka Mwana Wa Mfalme alimaanisha nini
 
Mkuu nimejarbu kusoma mara tatu lakini sijaelewa point yako hasa ni nini.
 
Ni kweli ndoa ni zaidi ya ngono naungana na wewe, ila kiimani ya dini ya kiislam, ili ihesabike ndoa basi lazima ngono iwepo hata Mara moja.
Pili uislam huo huo unamkataza mwanamke kukataa ngono kwa mumewe
( unaweza kataa kumpikia usipate dhambi,kumfulia nk) lakini unapomkatalia ngono unapata dhambi,

Ndoa ni miili miwili kukubali kuishi na nafsi moja, kwa maana ya maridhiano, kama mumeo hapendi unywe pombe acha. Kama mkeo hataki hiki au kile acha.nk
 
Ni vizuri pia ungewaelezea wanatakiwa waweje kwenye ndoa zao ili wajirekebishe...

Badala ya kushusha shutuma peke yake...


Cc: mahondaw
 
ndoa bila ngono hilo halipo hata kama mbuzi anafanya ngono bila ndoa hilo haliondoi ulazima wa ngono kwenye ndoa, huenda unapointi lkn ulivyoiwasilisha umeondoa maana tena umekosea sana.
 
Back
Top Bottom