Wanawake: Mume ghafla anaanza kukosoa chakula chako………! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake: Mume ghafla anaanza kukosoa chakula chako………!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jul 25, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Nimechoshwa na aina ya vyakula unavyopika humu ndani, sasa hiki ni kitu gani.......!

  Inawezekana chakula kikawa na kasoro ndogo tu ya kawaida ambayo siku za nyuma alikuwa wala haisemi mpaka wewe mwenyewe umweleze kuwa chakula leo kimezidi chumvi kidogo au kina kasoro fulani, na yeye kwa upendo anakujibu tu kwamba siku hazilingani na maisha yanaendelea.

  Lakini inatokea ghafla tu mumeo au mpenzi wako anaanza kukosoa chakula chako kwa njia yenye kukera. Tabia hiyo siyo ya siku moja, inakuwa ndio tabia yake. Karibu kila siku haridhishwi na aina ya vyakula unavyompikia.Nawaomba wanawake wanipe uzoefu wao katika jambo hili........

  Je utafanyaje iwapo utakutana na kisirani hiki.......................?
   
 2. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi ngoja kwanza niende siasani nitarudi baadae...............hapa patamu kweli.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,738
  Trophy Points: 280
  naona unakimbia
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,738
  Trophy Points: 280
  Ngoja nijifiche hapa pembeni nione itakuwaje match ya leo!
   
 5. chelsea fc

  chelsea fc JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 835
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  mpe jiko apike cha kwake kitamu!lol
   
 6. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  yaani rutta umenichokonoa nije halafu wewe umekwenda kukaa pembeni kuangalia lol! ila ukweli hakunaga mwanaume wa aina hii ila kama ni mimi nitavumilia siku ya kwanza na ya pili ikishakuwa tabia yaani wala hainisumbui najisemea tu nimemzoea huyu. na achana naye so long as menu iko fresh yeye ni kisirani chake basi wala simkohoi siriaz.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #7
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Je akisema atapika huko huko kazini kwake hivyo asihesabiwe kula hapo nyumbani itakuwaje..............?
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  gfsonwing hapo kwenye bold, sijaelewe...... eti unasemaje?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  yaelekea wewe rutta ndo mwenye hilo gubu kama miye ndo mkeo mbona wala huninyimi usingizi? yaani hunikolezi kabisa
  aaaaa!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  namaanisha hakunaga mwanaume mwenye gubu milele ila pia kama yupo basi nitafanya kama nilivyoeleza manake wanaume hawana kanuni bana.

  lkn pia Mtambuzi wanaume wengine sababu kama hizi unakuta tayari ameshapita hongera bar pale pembeni sijui panaitwaje wanakula minyama na mabia akifika nyumbani ndo karaha zake mwingine kesha fika kwa zainab huko kala akirud nyodo khaa! tena hawa ndio wale wanaolishwaga manyama yaliyavundikwa kwenye utupu ndi visirani hadi basi yaani niliondoka manake hapa naweza kusema nikapata ban bureeee
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #11
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  gfsonwin, hapo kwenye BOLD NYEKUNDU nimekuelewa sasa.............. Ahsante sana.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. M

  Mauu Member

  #12
  Jul 25, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 48
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ukiona hivyo ujue keshaanza kuvuliwa soksi na nyumba ndogo, then anaulizwa utakula "ubwabwa na khukhu?", ikifika hapo lazima ataona chakula cha nyumba kubwa hakina radha, tee tee tee

  napita tu jamani
   
 13. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #13
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Lakini pia sio vibaya kama mkijaribu kuwashirikisha kupika waume zenu kwani mchuzi ukichachuka, hakuna lawama hapo.....

  [​IMG]

  [​IMG]
   
 14. mito

  mito JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,612
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi naona unaendelea kuwa biased, safari hii sikutetei ng'o!
   
 15. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #15
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  mito hii ya leo sijasema kitu ila nimeuliza tu.......................
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #16
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  dalili ya mvua ni mawingu,hiyo ni dalili tosha kwamba yupo mwenzio haupo peke yako
   
 17. mito

  mito JF-Expert Member

  #17
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,612
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Ngoja basi nikupe evidence: Nawaomba wanawake wanipe uzoefu wao katika jambo hili........

  Pamoja mkuu, just kidding!!!!
   
 18. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #18
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  sasa Mtambuzi umenichokonoa yaani nyongo imesha tumbuka naomba MODS MSINIPE BAN ILA mniruhusu niwachambe hawa wababa wa aina hii na hapa nasema kwa hasira sana manake siku zote muhanga wa hili ni mwanamke.

  Jmanai wababa msiopenda kula majumbani mwenu ama mkirudi mnarudi na gubu ili tu usiweze kula useme sijui menu mbaya ama sijui nimekwazika ni wapumbavu sana. Hivi huko mnakokula mnajua lakin wanachokifanya? jamani mnalishwa uchafu sana ma limbwata ndipo yanapowapata yaaani unakuta watu mnalishwa hadi nyama za maiti mkirudi nyumbani mnawaona wake zenu kama kinyesi na kuona wanawanukia kama choo lol!

  jamani tuseme siye tulioko humu jamvini jamania walioko majumbani wanateseka sana sana.wanaowatesa na hawa ma ma belzebuli ambao ni washirikina halafu wanategemea ulonzi tu. to me hawa wnaume yaani wananichefua hadi hasira. nina mama jiran yangu hapa mume anamuona kama choo god forbid halafu utasema wanaume ni watu wa kuonewa huruma? yaani nyie hadi mfie kwa makahaba ndipo mtakapo jua kwamba kisamvu kitam ni cha mpira. tena nisiendelee naweza kujaza kurasa kwa hasira , aaaaaaaaaaaaaaaaaaaggggggggggggggggrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #19
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  mmmmmmmh kama ni kweli chumvi imezidi sitakuwa na tatizo..... au kama tatizo analolisema lipo wala sitakuwa na tatizo, kama ananiambia kwa jinsi ya kukera nitanuna dakika mbili tatu lakini nitafanyia kazi maneno yake.....

  ila kama hakuna tatizo, ananiambia hivyo ili anikere tu.... nitamvumilia mara 4.......

  mara ya 5 nitamwambia...

  1. aongeze fungu la chakula na asema anataka kula nini.... na standard gani (maana sie wengine kupika mashalaaah tuna kipaji ...)
  2. kama ana kisa anieleze wazi....
  3. kama vipi aingie jikoni kupika....
  4. kama kuna mahali amepata anakula huko asema na mie nitafute pa kula {yes, najiua kuna watu watapinga hili...lakini sometimes usipokuwa bandidu, mwanaume atakutia presha, sometimes you have to learn your lesson a hard way...}

  lakini zaidi ya yote nitachunguza chanzo cha kero hizo ni nini...
  - je kweli standard ya chakula imeshuka?
  - je anafrustration zake kashindwa jinsi ya kuzitua ananitafutia sababu?
  - je kuna mahali anachakachua; hivyo akirudi anaanzisha ugomvi makusudi ili asile au nisimwombe dushelele?
  - je ni visa tu kaamua kufanya?

  ila nitamweleza wazi sipendi jinsi anavyowasilisha hilo tatizo, nitamwambia kuwa ananikera, na moja ya udhaifu wangu ni kuwa ukiniudhi nami nitakutafutia kisa nikuudhi zaidi, kwa hiyo nitamwonya mapemaaaaaa sitaki ugomvi mie......

  bai zee wei karibu msosi Mtambuzi...

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #20
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  hahahahah tuliza munkari gfsonwin.........
  mijanaume ndivyo ilivyo...loh.........

  keshakula nyumba ndogo akirudi home visa...aaaarggghhhhhhh ......... kama hutaki kula si useme tu?
  halafu wanadhani wanawake kwa kuwa tu wamezaa hawawezi kuwa na small hausi, kumbe wenzao wanaheshimu tu ndoa zao....

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...