GedsellianTz
JF-Expert Member
- Jul 5, 2016
- 1,348
- 1,803
Kuna mwanaume anayefanya kazi kwa kujituma na kidogo anachokipata hurejesha nyumbani kwa mkewe ili kuweza timiza matumizi ya lazima kwa ajili ya familia na malezi ya watoto.Baadhi ya wanawake wamekosa karama ya kutunza pesa na kuwa na budget nzuri ya familia,ukweli humuweka mtu huru sababu kuna wanawake wana pairs za viatu nyingi kuliko mume wake na watoto wake.
Kuna wanaume wanajinyima kwa mambo mengi sana kwa ajili ya familia yake,lakini bahati mbaya ipo kwa mwanamke asiyejua kutambua umuhimu wa kila pesa anayopewa na mumewe.Ni kazi rahisi kununua Brazilian wig na ni vigumu sana kutoa mawazo chanya ya ujenzi wa familia na kuwa na mbinu za kutunza pesa kwa ajili ya kesho.
Wanaume Wana siri nzito sana mioyoni mwetu ,kuna nyakati mtu unatafuta pesa kwa njia ngumu na za majuto ili familia iweze kupata mahitaji ya lazima,kama afya,elimu na malazi ila wanawake baadhi yao hawajui uchungu tunaupata kwenye kutafuta pesa za kuweza fanikisha utilities bills zote ,water,electricity na house rent.
Kisukari ,pressure ,unyonge ni magonjwa ambayo wanaume wengi wameyapata kutokana na stress za wanawake na kutuacha tukiwa na simanzi muda wote sababu pesa ikiwepo wanawake wanakuwa na mapenzi ila pesa ikikimbia wanawake wanakimbia .Hakuna mwanaume anayependa kuona mtoto wake analelewa na mwanaume mwingine sababu ya ujinga wa baadhi ya wanawake.
Ni wakati sahihi wa wanawake kutambua na kuelewa changamoto za maisha na kuwa na wigo mpana wa maarifa na nidhamu ya pesa kwa kila shilingi ambayo mume na mke wanaipata, familia kwanza na urembo baadaye,ndoa huwa tamu sana pale inapokuwa na furaha katika Nyanja zote za shida na raha.
Hata sisi wanaume tuna nyama na moyo pamoja na damu ,tunapenda kupendwa,kubembelezwa kuambiwa maneno matamu na kuitwa majina matamu siku zote ,wanawake tupeni faraja na mapenzi ya dhati ili tulee kwa pamoja watoto wetu na Mungu atupe uzima na afya kuja shuhudia harusi za watoto wetu,tupumzishine na stress,pressure na visukari.
Commitment is like trust, never commit if you can not make it. Nothing wrong to say no on the face than making someone a fool.
#GedsellianTz