Wanawake, msing'ang'anie wanaume ambao hawawataki

Wanawake, msing'ang'anie wanaume ambao hawawataki

Na tutakoma kweli tusipobadilika basii tena sikio La kufa yaani ukija huku JF dongo ukienda mtaani magu basi tabu tupu.mtuonee huruma jamani khaah
Duh, poleni sana
 
Mwanamke hawezi kung'ang'ania sehemu ambayo haina maslahi. Je ipi bora kusalitiwa na mahurrier unanunuliwa au kwenda kwa maskin na kuvumilia usafir wa pikipiki+upepo maisha hayaeleweki
Enhee, kwani wee unaonaje?
 
Mungu sio Mwigulu Nchemba

hahahahahahhahahahahahahahahahahahahahahaha
 
Zaidi ya watu wa 5 wameshakueleza kwamba jamaa hana time na wewe na ameshachumbia mtu mwingine hukuamini. Mungu sio Mwigulu Nchemba, siku 1 akiwa kwenye mishemishe za kuchepuka simu yake ikajipiga ukamsikia anaongea na msichana mwingine na baada ya muda ukawasikia wanapiga kwinchi kwinchi Live wakati alikuaga muda huo yuko kwenye kikao cha harusi. Mungu akaamua kukuonyesha kitu live.

Ulipomuuliza akaruka futi elfu 6 kwamba unamsingizia una kila ushahidi kwamba huyo jamaa ni kimeo ila kwa sababu akili yako ina ujibwa ulezi uliochanganywa na alizeti ukamsamehe, sasa leo amekuoa na tabia zilezile walizokuonya rafiki zako zimeendelea, unashinda unalia na kuimba Pambio la bwana tenda miujiza usiaache mpaka mwaka huu upite.

Alishatenda muujiza kukuonyesha ushahidi hukutaka kumsikia, ukapenda zaidi matarumbeta ya harusi bila kujali ndoa itakuwaje. Pole hakuna muujiza hapo, jipigie matarumbeta kwa kujitendea muujiza. Kamwe usidharau Mungu akikuonyesha (clear Signs) kwamba mtu uliyenaye ni shida. Using'ang'anie kuwa mjumbe wa bunge la katiba kama unahisi posho haitoshi achia ngazi.

Heri ukose harusi leo ujiandae kwa ndoa bora ya keshokutwa.
Umenifanya nicheke sana.. Eti pambio tenda miujiza.. Sijui huwa mnatoa wapi hayo maneno
 
Back
Top Bottom