Wanawake msikilizeni mwalimu wenu

Wanawake msikilizeni mwalimu wenu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
1. Anakupigia simu mara kwa mara na kukuuliza siku yako imeendaje. Anafanya hivi kirafiki na kwa upendo, haigizi. Anakupenda kweli.

2. Anakutembelea mara kwa mara, anakuwa karibu na wewe kipindi unaumwa, hii inamaanisha kwamba yupo tayari kukuvumilia katika shida na raha. Mpende mwanaume huyu.

3. Anawapenda ndugu zako kama ndugu zake. Anaongea nao vizuri na kusaidiana mambo ya hapa na pale. Mtizame kwa jicho la tatu huyu mwanaume!
4. Anaongea na wewe kwa adabu na kwa upole, anakukosoa bila wasiwasi kama kuna mambo unaenenda visivyo. Anakuelekeza njia zilizonyoka..sio wa kumuacha huyu!

5. Hakulazimishi kufanya mapenzi. Anakupenda sana kiasi kwamba hawezi kukulazimisha jambo ambalo hauko na hiari nalo. Yupo karibu na wewe wakati wote na sio tu anapokutaka kimapenzi, huyu ni bonge la bwana.

6. Anakusaidia fedha pale unapokua umekwama kabisa, yuko na jukumu la kukusaidia kiuchumi. Anapenda kukupa kile ambacho amejaaliwa nacho. Hana mkono wa birika, Huyu anakupenda!

7. Anazungumzia future yake na wewe, mipango ya baadae pamoja na wewe, huyu anayo dhamira ya dhati kutoka moyoni mwake ya kukufanya uwe mkewe.

Hizi ni moja ya dalili kwamba mwanaume wako anakupenda na anataka atengeneze future pamoja na wewe. Usikate tamaa juu ya mwanaume wa aina hii.

Hao wenye sixpack sijui eight pack, wabeba vyuma, wavaa milegezo, wanyonya midomo na mahandsome wavaa hereni, waume za watu, masupa staa, watoto wa vigogo, hawatakusaidia lolote, utabaki ukiumizwa tu moyo wako.

Kabla hujajipendekeza kwa wanaume wa aina hiyo, jiulize wanawake wanzako wangapi wameshajipendekeza kwa sababu ya hzo pesa zake, hivyo na wewe unajiongeza kwenye foleni!

Mvumilie mwanaume wako, anazo ndoto njema, mapenzi ya kweli ni vigumu sana kuyapata. Ila pesa na mali ni rahisi sana kuzipata kama utajibidiisha.

Usipende mitelemko, mitelemko mingine ni njia ziletazo mauti! - Ukishikwa shikamana, ukipendwa, pendeka!

My wisdom, "Don't date a rich man, date a GOOD MAN, Good man will spend his life trying to keep u happy, no rich man can buy that!" Share

Mwl Tweve Hezron
 
Aiseee mi hata kama umeyatoa haya maelezo mahali Fulani..


BADO NAKUPONGEZA KWAKUTOA MUDA WAKO KWENDA KUMSIKILIZA UYO MWALIMU AU KUSOMA MAKALA ZAKE NAKUJA KUANDIKA HUMU !!!..

kinachonifurahisha zaidi ,,Hamna post yako ilowah zungumzia habar zisizojenga mahusiano I.e kibamia,hogo +pesa .

You always show up yourself !!!! GOOD GIRL ,YOU ARE SUCH AN INTELLIGENT , PRACTICAL ,DETERMINED, DECIDED , UNCHANGEABLE WOMAN ...LOOKING FOR NOTHING BUT ONLY CHANGING OUR NEGATIVE ATTITUDE TO A POSTIVE !!!.
 
Mwenye macho na auone ujumbe huu muhimu,,kwa Mimi nimeuchagua kufunga nao mwaka.
 
Ukinibania namba 5 ni ngumu sana kupata namba 6 hata kama uwe umeniwekea limbwata
 
wakati hata maigizo unaweza yaona kama ukweli lakini ni maigizo tu. Suala la mapenzi asikudanganye mtu sijui ukiona nini ujue ukweli ama hakupendi-mapenzi yanatofautiana sana kutoka mtu mmoja kwenda mwingine hivyo huwezi yageneralize kirahisi kama hivyo
 
wangu hana hata sifa moja na ndo maana simtambulishi na nikitongozwa kwingine nakubali nampiga tu kiswahili
 
mwanaume hana hata sifa moja halafu ukisema upo single anamind eti mimi ni nani wako? jithamini ujue wewe ni nani usinipangie
 
wakati hata maigizo unaweza yaona kama ukweli lakini ni maigizo tu. Suala la mapenzi asikudanganye mtu sijui ukiona nini ujue ukweli ama hakupendi-mapenzi yanatofautiana sana kutoka mtu mmoja kwenda mwingine hivyo huwezi yageneralize kirahisi kama hivyo
Respect
 
Wanawake mwalimu wao Kipofu,nauliza tu mkuu na ww ni Kipofu?kama la basi Ujue somo halitaeleweka
 
Wanapatikana wapi hao wanaume wenye sifa tajwa hapo juu mtoa uzi
 
Back
Top Bottom