Wanawake mnaobugia miudongo mnaboa sana!

Wanawake mnaobugia miudongo mnaboa sana!

ngoja tusubiri waje watiririke wenyewe.

Ok.....ila wakati nipo sekondari kuna kaka alikuwa ananipenda mpaka watu walikuwa wanamuonea huruma.Jina lake kama hii ID yako...teh teh
 
mim nilikuwa nakula wakat wa preg

uliachaje? make mwanamke akianza hii kitu ni ngumu sana kuacha--ugumu wake hauna tofauti na ugumu aliopitia ray C wakati anajiandaa kuacha kubwia unga!
 
Wewe ni mweupe sana katika mambo ya sayansi ya afya. Tena yawezekana ndio nyie wake zenu akiwa mja mzito akatamani kande ama samaki, unamwambia hakuna kupika kande wala samaki kwa kudhani eti ni tabia mbaya ya kujiendekeza.

Kama unataka kupata scientific reasons, ungeuliza kwa wataalamu wa Afya ya wanawake ili wakupe kitu sahihi kuliko kujifanya unajua na mtu uko shallow ki hivyo. Vinginevyo labda uwe m mama ili uelewe unachokisema. Kinyume cha hapo, kwa jinsi ulivyoiweka hoja yako hapo juu, unaonekana mburura na mnyanyasaji wa wa mama. Pole.
 
Aise hii hali inatokeaga tu unakuwa na hamu ya udongo yani kuna kipindi nisipokula kabla ya chochote au lecture sielewi mi na marafiki zangu yani shida nikasemwa wee eeh i.thank God nimeacha kula udongo aisee ukiona wanawake wanaula ujue wana tatizo

tupe uzoefu jinsi ulivyoacha mkuu. was it easy to stop that habit?
 
yawezekana kweli alikuwa na upungufu wa madini ya chuma. Lakini kama damu imepungua sana kwa ajili ya kuchoropoa mimba ovyo, lazima ale.
 
Itabidi elimu ya lishe iwe compulsory kuanzia std 3 kuondoa huu usumbufu. Hii kitu ni mbaya no wonder tunazaa watoto wenye akili ndogo kisa mama alikosa health food. Badala ya kucheja na kuwakasirikia wanaokula kana jamii tutafute njia mbadala ya kuwasaidia ili tuweze kupata jamii yenye kizazi cha akili nzuri.

very constructive idea mkuu. inabidi somo la human nutrition liingizwe kwenye curriculum ya elimu ya msingi na sekondari ili kuwakoa hawa wenzetu wanaopotea kwa kukosa maarifa. hii itasaidia kuwakomboa wanawake wanaoathiriwa na minyoo na appendix kutokana na kubugia uchafu.
 
Hahaaa mtoa mada umezidisha....alikula kiroba kizima? Btw umenichoma haswaaa... Mimi sista alikuwa anakula sana udongo na mpaka kesho anakula sana tu kwa hiyo at the age of 7 na mimi nilikuwa nimeshaanza kula udongo kwa kuiga....nikajikuta nimezoea nikafikia hatua ya kuchimbua kuta za nyumba (nyumba za kule kwetu sio za hapa mjini). Kuna siku niliomba ushauri Jf doctor nikaambiwa nitumie sana dagaa. Thanx God sasa hivi nna miez mitatu sijagusa udongo japo kaham kanakuja lkn naweza kujikaza sio kama zamani nikisikia hamu naweza kukurupuka hata kitandani nikazama magengeni kusaka udongo

ndio hivyo mkuu--bi shost kafakamia kiroba kizima cha udongo hadi kazimika. inaonekana alikuwa na hamu nao sana.

halafu inakuwaje hii hamu ya udongo iwa-affect kina mama tu? hili ni suala la kufanyia utafiti wa kina.
 
Kuna jamii flani nliwai kaa nayo, wanawake wa lile eneo wanakula udongo sijawai ona.Wakisha pata lunch lazima ashishie na udongo kama vile ndo maji.Wenyewe wanakuambia akishushia na udongo ndo anajiskia kushiba vzr.
 
Ok.....ila wakati nipo sekondari kuna kaka alikuwa ananipenda mpaka watu walikuwa wanamuonea huruma.Jina lake kama hii ID yako...teh teh

hahahaha! inawezekana ndio mimi mkuu.
 
Nimefanya utafiti huwa ni aina flani ya majini huvaa watu ndio wanakula udongo
Ukiona mtu anakula sio yeye ni pepo
 
Mwe mim kipindi hicho nilikuwa nakula sana ubuyu wa vinto....wenye pilipili....

umenikumbusha kuna ubuyu nikuwa nanunua kwa waarabu sijui walikuwa wanachanganya na nin nikila tu nalala usingiz wa hatar
 
uliachaje? make mwanamke akianza hii kitu ni ngumu sana kuacha--ugumu wake hauna tofauti na ugumu aliopitia ray C wakati anajiandaa kuacha kubwia unga!

sio kawaida yangu kabla ya hapo sikuwa nakula hata nilipojifungua sijautia mdomoni
 
Wewe ni mweupe sana katika mambo ya sayansi ya afya. Tena yawezekana ndio nyie wake zenu akiwa mja mzito akatamani kande ama samaki, unamwambia hakuna kupika kande wala samaki kwa kudhani eti ni tabia mbaya ya kujiendekeza.

Kama unataka kupata scientific reasons, ungeuliza kwa wataalamu wa Afya ya wanawake ili wakupe kitu sahihi kuliko kujifanya unajua na mtu uko shallow ki hivyo. Vinginevyo labda uwe m mama ili uelewe unachokisema. Kinyume cha hapo, kwa jinsi ulivyoiweka hoja yako hapo juu, unaonekana mburura na mnyanyasaji wa wa mama. Pole.

mkuu unachosema ni kweli kabisa, hii kitu hata mimi inanipiga chenga. ndio maana nimeiweka hapa ili wajuzi muidadavue. ninachojua ni kwamba wanawake wanaokula udongo wana upungufu wa iron. kama wewe unajua kuna sababu nyingine, imwaga hapa tujielimishe.
 
Teh teh teh kama wewe basi umekua....

kweli. tangu tulipokutana Mkwawa 1997 hadi leo ntakuwa mkubwa tu mbona? si unanikumbuka lakini nilivyokuwa mdogo kipindi kile?
 
Back
Top Bottom