Rorscharch
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 1,431
- 3,068
Miaka inasogea, teknolojia inapaa, lakini ndoa na mahusiano kati ya wanaume na wanawake yanazidi kuyumba. Na hapa sina haja ya kuchagua maneno mazuri: hii siyo ajali ya ghafla, ni kosa la kurudia rudia, kizazi baada ya kizazi.
Na kama tukiweka kisogo kwenye ukweli, tutabaki tukitafuta visingizio vya “wanaume wa siku hizi” au “wanawake wa siku hizi” bila kugusa mizizi ya tatizo.
Kitchen party zimekuwa kama “bunge la wanawake” — ajenda ni moja tu: namna ya kumshika mwanaume. Lakini kinachoshangaza ni hiki: nani anaweza kukufundisha kuishi na mwanaume vizuri zaidi ya mwanaume mwenyewe?
Siku mkiamua kuwaalika wanaume kwenye kitchen party zenu kama Makungwi — walimu wa namna ya kuishi nao, heshima wanayohitaji, na makosa ambayo huwafanya waachane nanyi bila hata notice ya mwezi — ndoa zenu zitapumua upya.
Na usifikiri mwanaume wako hajui. Anaanza kuona tofauti. Na kumbuka, mama yake mwenyewe hutumia “naomba” — wewe ni nani usijishushe? Hapo ndipo kalenda ya kuachika inaanza kukatika siku.
Hufanyi kazi, huna mradi, hata kuuza ice cream mlangoni hufikirii, lakini kila kitu unataka kitoke mfukoni mwake. Na cha kushangaza zaidi, anapenda nywele zako natural, lakini wewe unalazimisha mbwembwe zisizo na maana kwake (kusuka nywele za 50,000/-).
Mwanaume anapenda kuona unajiongeza — kwamba unaweza kushughulikia angalau shida ndogo ndogo bila kila wakati kugeuka mteja wa kudumu wa pochi yake.
Ukijijengea sifa ya kuwa “pasua kichwa”, ataacha kukushirikisha, na hapo umeshasikia kengele ya mwisho ikipigwa.
Hapa ndipo kauli za ajabu kama, “Baba Fulani anafanyaga hivi kwa mke wake, wewe kwanini hufanyi?” zinapokamata nafasi.
Lakini kumbuka, mwanaume ni mtu mzima kabla ya kukutana nawe. Ukianza kumfanyia “programming” kana kwamba ni simu mpya unayoi-set, unampotezea heshima na uhuru wake. Na mwanaume akihisi hana nafasi ya kuwa yeye mwenyewe ndani ya ndoa, atatafuta mahali ambapo anahisi huru — na mara nyingi, hapo ndipo safari yako inaishia.
Mwanamke asiye na uwezo wa kutamka “samahani” anamtumia mwanaume wake ujumbe mmoja: sitaki kubeba lawama. Na huo ndio mwanzo wa mlango kufunguka taratibu.
Hitimisho:
Kitchen party zenu zinapaswa kugeuka mashule ya kweli ya maisha ya ndoa — na “walimu wakuu” wawe wanaume wenyewe. Waje waseme wazi: kile kinachotuudhi, kile kinachotufanya tubaki, na kile kinachotusukuma kutokomea.
Mkiendelea kufundishana wenyewe kwa wenyewe, mtaendelea kurudia kosa lile lile. Lakini mkikaa chini mkasikiliza mwanaume kama Kungwi wenu, huenda ndoa zenu zikawa na pumzi ndefu kuliko chai ya rangi ya saa kumi na moja asubuhi.
Na kama tukiweka kisogo kwenye ukweli, tutabaki tukitafuta visingizio vya “wanaume wa siku hizi” au “wanawake wa siku hizi” bila kugusa mizizi ya tatizo.
Kitchen party zimekuwa kama “bunge la wanawake” — ajenda ni moja tu: namna ya kumshika mwanaume. Lakini kinachoshangaza ni hiki: nani anaweza kukufundisha kuishi na mwanaume vizuri zaidi ya mwanaume mwenyewe?
Siku mkiamua kuwaalika wanaume kwenye kitchen party zenu kama Makungwi — walimu wa namna ya kuishi nao, heshima wanayohitaji, na makosa ambayo huwafanya waachane nanyi bila hata notice ya mwezi — ndoa zenu zitapumua upya.
1. Kutoka “Naomba” hadi “Nataka”
Mwanzo wa mahusiano ni kama mwezi wa asali — unamwomba kwa heshima, unamshukuru mara tatu. Lakini muda unavyosogea, neno “naomba” linatoweka, linachukua nafasi “nataka”.Na usifikiri mwanaume wako hajui. Anaanza kuona tofauti. Na kumbuka, mama yake mwenyewe hutumia “naomba” — wewe ni nani usijishushe? Hapo ndipo kalenda ya kuachika inaanza kukatika siku.
2. Kuamini sehemu zako za Siri ndio kila kitu
Dada, kama mchango wako pekee ni kitanda, umeshapotea. Mwanaume anaweza kuvutiwa, lakini hawezi kuendesha ndoa kwa “romance” pekee.Hufanyi kazi, huna mradi, hata kuuza ice cream mlangoni hufikirii, lakini kila kitu unataka kitoke mfukoni mwake. Na cha kushangaza zaidi, anapenda nywele zako natural, lakini wewe unalazimisha mbwembwe zisizo na maana kwake (kusuka nywele za 50,000/-).
Mwanaume anapenda kuona unajiongeza — kwamba unaweza kushughulikia angalau shida ndogo ndogo bila kila wakati kugeuka mteja wa kudumu wa pochi yake.
3. Kiburi, adui wa kwanza wa ndoa
Mwanaume anaweza kuvumilia kelele, anaweza kuvumilia hata ukali wa maneno mara moja moja, lakini kiburi cha kila siku? Hapo umekwisha. Amepambana na bosi kazini, akarudi nyumbani anakutana na vita nyingine juu ya rasilimali alizozitafuta kwa jasho lake.Ukijijengea sifa ya kuwa “pasua kichwa”, ataacha kukushirikisha, na hapo umeshasikia kengele ya mwisho ikipigwa.
4. Kuteka maisha ya Mwanaume kama 'Remote Control'
Hii ndiyo kasumba inayowafanya wanaume wengi wajisikie kama wageni kwenye maisha yao wenyewe. Unaanza kumweleza marafiki zake wa kukaa nao, unachuja ndugu zake wa karibu na wa mbali, na hata kumwelekeza namna ya kuonesha upendo kwako.Hapa ndipo kauli za ajabu kama, “Baba Fulani anafanyaga hivi kwa mke wake, wewe kwanini hufanyi?” zinapokamata nafasi.
Lakini kumbuka, mwanaume ni mtu mzima kabla ya kukutana nawe. Ukianza kumfanyia “programming” kana kwamba ni simu mpya unayoi-set, unampotezea heshima na uhuru wake. Na mwanaume akihisi hana nafasi ya kuwa yeye mwenyewe ndani ya ndoa, atatafuta mahali ambapo anahisi huru — na mara nyingi, hapo ndipo safari yako inaishia.
5. Kukosa uwezo wa kusema 'Samahani'
Hili ni janga la malezi. Wengi mnalelewa mkihisi kuwa mna haki kila wakati. Lakini ndoa si uwanja wa kutafuta nani yuko sahihi; ni sehemu ya kutafuta suluhu.Mwanamke asiye na uwezo wa kutamka “samahani” anamtumia mwanaume wake ujumbe mmoja: sitaki kubeba lawama. Na huo ndio mwanzo wa mlango kufunguka taratibu.