Wanawake mkoani Tanga wagoma kubeba Ujauzito kutokana na changamoto wakati wa kujifungua

Wanawake mkoani Tanga wagoma kubeba Ujauzito kutokana na changamoto wakati wa kujifungua

Heparin

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
440
Reaction score
3,211
1000042536.jpg


Wanawake wa Mwembeni, Kata ya Madanga Mkoani Tanga wamegoma kubeba ujauzito baada ya makubaliano na waume zao kwasababu wanapata shida wakati wa kujifungua kwani wanalazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya huku wengine wakijifungulia njiani jambo linalohatarisha afya zao.

Kufuatia hatua hiyo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abrahaman Abdallah amesema awali kijiji hicho kilikuwa na Zahanati ambayo ilijengwa chini ya kiwango cha ubora hali iliyopelekea Serikali kuifunga kwa muda mfupi kutokana na majengo yake kuchakaa hivyo kuwalazimu wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.

Bw. Abrahaman Abdallah amehimiza pia kuharakishwa kwa ujenzi wa Zahanati unaoendelea kijijini humo ili changamoto hiyo iweze kumalizwa na kuondoa matatizo ya wananchi yanayowakanbili kwa sasa.

"Tayari shilingi milioni 28 zimetolewa na Zahanati imeshaanza kujengwa na ndani ya mwaka huu tutahakikisha inamalizika na kukamilika tayari kwa kuanza kutoa huduma, kwahiyo wakinamama wa Mwembeni ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, ruksa kubeba mimba sasa" alisisitiza Mwenyekiti Rajab.

"Waliniambia wakinamama wa Mwembeni kwamba wamekubaliana na waume zao kwa muda sasa wasibebe ujauzito kwasababu wanapata shida inapofika wakati wa kujifungua kwakuwa wanakwenda mbali na muda lakini wakati mwingine wamekuwa wanajifungulia njiani hali inayohatarisha afya zao, " alisema Mwenyekiti huyo.
 
Kwani mimba ni takwa la kisheria? Sisi kama serikali tunapambana kuhamasisha uzazi wa mpango.
 
Back
Top Bottom