Wanawake kwa hili hapana mjirekebishe

Wanawake kwa hili hapana mjirekebishe

Uta Uta

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2016
Posts
3,740
Reaction score
8,765
Wanawake ni viumbe muhimu sana hapa duniani. Umuhimu wao upo ktk nyanja mbali mbali kwanza wao ndio mama zetu waliotuzaa, pili wao ndio wake zetu na pia wao ndio wenye uwezo wa kipekee wa kutuondelea msongo wa mawazo na maisha pia.

Mi nawaheshimu sana wanawake na ikitokea mtu amewasema vibaya huwa nahuzunika sana. Ila leo na mimi nainua mkono kwa hii dosari ndogo ninayoiona mara kwa mara. Mnapokuwa ktk daladala huwa hamuwatendei vizuri wanawake wenzenu, utakuta amepanda mama ana mtoto mgongoni au anatumbo kubwa amesimama na wanawake mliobaki hamna watoto wala nn ila mnawaacha wenzenu wamesima na watoto mgongoni au na tumbo (mimba) kubwa na ninyi bila kujali.

Mara zote nawaona wanaume ndio wakijali hali hizi. Kinachonishangaza ninyi mnaujua vizuri uchungu wa kusimama na mtoto au mimba kwa mda mrefu kuliko wanaume. Lakini kwa nn eneo hili mnakosa huruma? Au mpaka ianzishwe taasisi ya kutetea wamama vijacho na wanaonyonyesha?

Naomba nyie muwe mfano wa kuwasaidia wanawake wenzenu. Na mwisho nawapongeza sana wanaume kwa kuwa na huruma ktk eneo hili naomba muendelee na moyo huo.

Asanteni nawasilisha
 
Unawaonea tu mkuu, wao wenyewe huwa hawajielewi ni wakusaidia tu, ndivyo walivyo.

Akili zao wanazijua wao wenyewe, kama mwanaume pale tunapoweza kuwaisaidia let we do our best to help them.

Hili ndo linalotofautisha response kati ya mwanamke na mwanaume. Kwamba mwanaume response yake ni ya hapo kwa hapo katika kutoa msaada. Ila mwanamke ataona huruma tu then baadae sana ndo anaweza akafikiria labda atoe msaada.

Wanaweza wakawa wamekaaa wanamwangalia mwanamke mjamzito au aliyebeba mtoto mgongoni, WANAMHURUMIA SANA tu, ila sasa maamuzi ya haraka kutoa msaada ndo kashekashe. Usishangae kuona wanaume kutoa msaada haraka haraka ndivyo tulivyoumbwa kwa akili zetu. Na hili ni mojawapo ya tofauti kati ya mwanaume na mwanamke, ukiacha nyingine nyingi zilizopo.​
 
Mi siwalaumu natoa tu ushauri walione na hili
 
Kwa upande wangu huwa nikiona mzee,mjamzito au mama mwenye mtoto huwa napisha.
Pia inategemea nimekaa sehemu gani mana kama nimekaa mwisho kabisa ni ngumu.
Kuna siku moja nilikuwa natoka mjini naelekea sehemu basi zile gari zilikuwa hazitki mpaka zijaze kabisa ndio nyingine inapakia na hapo ilikuwa mida ya saa mojamoja jioni.
Nikapanda kwenye gari na siti nikapata tena mwanzoni mwanzoni tu.Gari ilipojaa akapanda mzee mmoja ikambidi asimame basi gari ikaanza kuondoka.Ila gari kabla haijaondoka nilikuwa nsjishauri kumwachia siti yule mzee au niendelee kukaa.
Mwishoe rohoni nikajisemea nakaa asimame tu kwani kwenye gari nipo peke yangu nimpe nafasi mbona wengine wamekausha tu.
Njiani sasa yule mzee alivyokuwa anapata shida gari ikiyumba na yeye anayumbishwa mara huku mara kule halafu kila nikimuona nafsi inanisuta.Mzee wa watu akashuka njiani(alifika alipokuwa anaenda).Njia nzima mpaka nafika nafsi ilikuwa inanisuta kila mara ile picha inanijia.
Nilijisikia vibaya kwakweli mana ilinichukua muda kusahau.
Ila toka hiyo siku nikikuta mtu wa aina hiyo amesimama tena karibu yangu nampisha tu akae.
Nilijifunza kwakweli.
 
Naomba utusamehe, tumekuelewa mno. Kwangu mie nabebaga watoto wa wamama kwenye gari siku moja kidogo niachiwe mtoto ila bado sijaacha, ila asante kwa kukazia hilo
 
Kwa upande wangu huwa nikiona mzee,mjamzito au mama mwenye mtoto huwa napisha.
Pia inategemea nimekaa sehemu gani mana kama nimekaa mwisho kabisa ni ngumu.
Kuna siku moja nilikuwa natoka mjini naelekea sehemu basi zile gari zilikuwa hazitki mpaka zijaze kabisa ndio nyingine inapakia na hapo ilikuwa mida ya saa mojamoja jioni.
Nikapanda kwenye gari na siti nikapata tena mwanzoni mwanzoni tu.Gari ilipojaa akapanda mzee mmoja ikambidi asimame basi gari ikaanza kuondoka.Ila gari kabla haijaondoka nilikuwa nsjishauri kumwachia siti yule mzee au niendelee kukaa.
Mwishoe rohoni nikajisemea nakaa asimame tu kwani kwenye gari nipo peke yangu nimpe nafasi mbona wengine wamekausha tu.
Njiani sasa yule mzee alivyokuwa anapata shida gari ikiyumba na yeye anayumbishwa mara huku mara kule halafu kila nikimuona nafsi inanisuta.Mzee wa watu akashuka njiani(alifika alipokuwa anaenda).Njia nzima mpaka nafika nafsi ilikuwa inanisuta kila mara ile picha inanijia.
Nilijisikia vibaya kwakweli mana ilinichukua muda kusahau.
Ila toka hiyo siku nikikuta mtu wa aina hiyo amesimama tena karibu yangu nampisha tu akae.
Nilijifunza kwakweli.
Kwa hiyo inawezekana alichokisema mwanawao kina kaukweli kidogo, eti mnakuwa wazito ktk kitoa maamuzi?
 
Sio wanawake wote wako hivyo.

Wapo wenye Adabu, Utii, Heshima na Huruma waliofunzwa nyumbani kwao

Ila umefanya vizuri kuwakumbusha.
 
Ni kweli sio watu lakini wengi hawaguswi na hili
 
Kwa hiyo inawezekana alichokisema mwanawao kina kaukweli kidogo, eti mnakuwa wazito ktk kitoa maamuzi?
Yawezekana pia
Mimi hiyo haikuwa tabia yangu ila siku hiyo nikajilinganisha na wenzangu nikaona hapana leo ngoja nikae mbona wengine hawajitolei?
Kilichonikuta sasa ndo nikajua kuigaiga si kuzuri na toka siku hiyo hata sijiulizi nanyanyka tu nampisha
 
Kwann usimame ilihali unamtoto au mimba ,tatizo wamezoea hata gar limejaa anaingia tu kisa akijua ninamtoto watanipisha,ilitokea watu wlimshusha hyo Dada asubil gar lingne otherwise kuwe hakuna usafir mwingne
 
Mimi naomba niongee hili kitofauti katika awamu tatu:

1. Mimba sio ugonjwa. Sio muda wote kwa sababu una mimba basi ndo huwezi kusimama hata kutoka morocco hadi makumbusho. Tuache kujiendekeza!

2. Mama una mtoto au tumbo kubwa, subiri gari lenye siti au gari ikisimama tu muombe konda au dereva akuwekee siti eboo(mimi nimetumia hii method kwenye ujauzito wangu na sikuwahi kupata shida ya kusimama kwenye basi). Mtu yuko mwanzo wa gari, lets say Makumbusho, gari likishajaa ndo huyo anapanda na mwanae. Sio fair kwa abiria wenzio.

3. Halafu wanaume mnasaidiaga si kutoka moyoni bali ili muonekane maana mwanaume akimpisha mama mjamzito au mwenye mtoto basi discussion kwenye basi inachange, ni "wanawake wana roho mbaya" mpaka mwisho. Wewe mwenye roho nzuri mbona hutendi wema ukaenda zako?
 
nilishasema simpishi Mwenye mimba wala Mwenye mtoto labda kizee tu

Unaona gari imejaa unapanda ya nn?
 
Mimi naomba niongee hili kitofauti katika awamu tatu:

1. Mimba sio ugonjwa. Sio muda wote kwa sababu una mimba basi ndo huwezi kusimama hata kutoka morocco hadi makumbusho. Tuache kujiendekeza!

2. Mama una mtoto au tumbo kubwa, subiri gari lenye siti au gari ikisimama tu muombe konda au dereva akuwekee siti eboo(mimi nimetumia hii method kwenye ujauzito wangu na sikuwahi kupata shida ya kusimama kwenye basi). Mtu yuko mwanzo wa gari, lets say Makumbusho, gari likishajaa ndo huyo anapanda na mwanae. Sio fair kwa abiria wenzio.

3. Halafu wanaume mnasaidiaga si kutoka moyoni bali ili muonekane maana mwanaume akimpisha mama mjamzito au mwenye mtoto basi discussion kwenye basi inachange, ni "wanawake wana roho mbaya" mpaka mwisho. Wewe mwenye roho nzuri mbona hutendi wema ukaenda zako?
Kwa gali za Mbagala ili upate gari yenye siti labda usubiri miaka 10. Halafu kwa yale magari yanatoka maeneo ya mjini kutoka nje ya mji huwa yanajaza yalipotoka, kwa hiyo ili upate siti inabidi ukapandie mjini au usisafiri kabisa
 
Toka mapema, panda gari ugeuze nalo. Huwezi simama na usubiri kudra za Mungu upishwe siti.
 
Back
Top Bottom