Wanawake huwa mnapatwaga na ibilisi gani?

Wanawake huwa mnapatwaga na ibilisi gani?

UrbanGentleman

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2016
Posts
2,584
Reaction score
1,886
Salam sana waungwana...

Nimeona niwashirikishe katika kupeana mawazo maana haya mahusiano yaliponifikia ni CLIMAX na nguvu ya kuendelea ni ndogo mno. walau kwa ushauri wenu labda i will go extra miles,pengine nimekosea mahala na sifahamu kama nimekosea.

Mwaka 2010 nilianza mahusiano na binti flani mwanafunzi wa alpha akiwa form 4 na mimi UDSM 1ST YEAR Infact maisha ya mwanzo katika mahusiano yalikua poa sana nilifurahia mnoo sababu kila mtu alimpenda mwenzake

Tulidumu kwa miaka kazaa tukawa karibu sana at first tuliishi kwa kupeana mapenzi ya mdomo(kissing) and all that sikuruhusu hisia zangu zinitawale kwake sababu sikutaka kufanya makosa katika lolote ambalo mwenzangu hakupenda kabisa kwa hilo nilifanikiwa kabisa na alinipenda zaidi nikampenda sana.

Nakumbuka alikua akisema hajawahi kuguswa yaani hamjui mwanaume na anataka mwanaume wake wa kwanza awe mume kwake infact nilifarijika sana sababu achilia kauli tu she was too innocent to be played n kiukweli nilikua namuaona mke katika utashi kujituma katika misimamo yake,mtu wa dini na anajitambua kwa umri mdogo tu.

Miaka mi3 baadae alichaguliwa Mzumbe wakti huo mimi nilikua niko mtaana tayari nimeshaingia katika harakati za kimaisha baada ya kisomo,ikawa furaha kwetu sote. Niliweza kumfanyia chochote alichoisi angefurahishwa nacho,sikupenda ajihisi mpweke kwa kukosa uwepo wangu au kushindwa kuwa msaada kwake pindi unapoitajika.

Nilikua nimeshamjua vizuri i mean touching her as mwanaume wake wa kwanza. Na aliwafahamu ndugu zangu vizuri kama mimi nilivyofahamika kwao, malengo yalijikita kwenye ndoa zaidi tukapanga akifika mwaka wa 2 tuanze process za ndoa.

Nikawa najipa moyo nashukuru Mungu na nini, mambo yangu yakawa yanakwenda vizuri na support ya mzee katika biashara zangu nikawa kwa namna flani financially niko sawa, si tegemezi tena, nikaweza kumiliki kiwanja mpaka kujenga inshallah nikawa nna kwangu na kila hatua nikawa namshirikisha mwenzangu uku tukifurahia pamoja.

Sasa kuna wakati flani nikawa nikienda kumtembelea naweza kua morogoro week nzima au akaja dar weeknd nikamrudisha chuo mpaka alipo maliza chuo lakini kunamabadiliko nilianza kuyaona,ambayo hayakuwahi kua sehemu ya tabia yake kabisa.

Ilifika wakati alikua anakuja dar sipati taarifa kama yuko dar ila nilikua nikipata taarifa kutoka kwa washikaj kua wamemuona sehemu flani na, mi sikustushwa na yeye kuja dar nikawa natulia kuobserve.
Sasa katikati hapo nikavunja ukimya nikazama sonara flani nikanunua pete moja ya uchumba ili nianzishe process ya kumposa na nini.

Weeknd flani nikajiandaa nikaandaa marafiki nikamuita dada ake na kaka zake nikawaamba nataka nimfanyie engagemnt huyu mwenzangu nitafanya kwa mstukizo msimwambie lolote, infact the idea was perfect kila mtu alipenda.

Siku imefika tumejiandaa jioni flani,marafiki, happy moments japo nilikua nikimuangalia mwenzangu naona kama hayuko sawa flani,nikimuuliza kunashida yuko amna niko sawa,basi namsogeza karibu yangu kiutu uzima asihisi namtenga, nikavunja ukimya kwa kuomba attention toka kwa washikaji na kumtambukisha rasmi kwa watu kama mchumba uku nafungua kibox changu nimvike pete chanda changu.

Akawa excited kiaina na kufurahi kawaida lakini katika marafiki zangu wote walinotice kitu. Cha ajabu baada ya hapo tuligonga cheers lakini alitoka na dada ake pembeni akawa kama anamuonya hivi na nini, nilihisi hayuko sawa. Baadae dada ake akaja na excuse kua atakua anaumwa ulcers uwa anasumbukiwa na ulcers na mi nikajifanya kuvunga kuwa nimeelewa.

Baada ya muda kama wa wiki akaniomba tumeet, nikamuliza kunanini yuko kuna mazungumzo nikasema sawa ngoja nikamsikilize bibie......
Kufika nahoji vipi mbna kama una uzuni mama kuna shida gani,unataka kuniambia nini leo mke wangu uku namuangalia usoni... Akawa kimya kwa muda, nikasema niambie tuu niko hapa kwa ajili yako.....

........daaaah!!! Akaanza ooh unajua ME i dont feel u same way i use to, so sizani kama ni busara kwa sisi kuendelea na sitaki nikudanganye sababu sipendi uumie zaidi, najua unanipenda lakini sitakua tayari kukupenda hivyo kama unavyonipenda, to be honest lets stop this sitaki uumie zaidi, akanichoma zaidi kwa kusema haya "najua umesacrifice alot ur time ur wealth lakini mimi im not read for this"

Nikajikuta nalengwa na machozi na uku nikihisi anatania lakini namfahamu akimaanisha kitu anakuaje, nilioji kwa unyonge tatizo ni nini akadai hakuna tatizo shez just not into marriege n thats it...
Sio siri nilitokwa na machozi japo nilijikaza sana tukaondoka nikamuacha kwao nikarudi home siko sawa na ndugu wote wanajua mambo ndo yameshika kasi kijana soon napeleka posa.

Hapa nilipo jamaa,marafiki wote wanajiandaa wakihoji vipi mbna shemeji hatumuoni nakosa la kujibu naishia kuvunga tu, sometimes nashindwa kwenda bash za washkaji sababu ntashindwa kudanganya....
Ndugu zangu nimetumbukia nipigeni tafu japo kimawazo sielewi nimekuaje ... I wish nitoe haya maumivu moyoni yani naumia mnoo, yani najisikia ovyo sanaa this is worse experience in my life...Mbaya zaidi inanitesa na ni ngumu kusahau najitaidi kujisocialize lakini bado inanitesa nisaidieni wadau...
 
Dah.....pole sana, najua ipo siku atakutafuta lakini atakuwa amechelewa.

Piga moyo konde, maisha lazima yaendelee. Huo ndo ukubwa.

Nakuonea huruma tu kuwa baada ya hapo hutamuamini mwanamke yeyote tena
 
Jamani good people sijui kwa nini huwa wanapitia majaribu mengi hivi. A broken engagement is better than a broken marriage. Je utamlazimisha mtu akupende? Utaishi na mtu ambaye unajua kabisa moyo wake na akili yake yote ipo kwa mtu mwingine? Muache tu aende, no matter how it hurts. She simply wasn't meant for you
Ila you made a mistake, kuna "red flags" alianza kukuonesha mapema afu ukaziignore. Kama alikuwa anakuja hadi Dar bila kukwambia + changes kwenye tabia, hukuhisi kuwa something is wrong, ufanye uchunguzi?? Wewe ukachukulia poa, ukaendelea hadi na engagement, ona kilichotokea sasa.

Anyway mshukuru Mungu kwa yote, inauma haswa but jipe tu moyo, its going to be well with your soul. Huwezi jua Mungu kakuepusha kitu gani na hujui huko mbeleni kakuandalia kitu gani. Kingine jisamehe na msamehe huyo binti, usije ukajenga uchungu moyoni mwako na wala usije kubadilika ukawa mtu "mbaya" kwa sababu ya mtu mwingine. Muachilie moyoni mwako, kaishi kwa amani

N: B idea yako ya kupropose nimeipendaaaa. Romantic men do still exist[emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Mkuu pole sana,, duh......mahaba niue......ila umejifunza kitu...... ulianza nae akiwa bado hajajichanganya duniani, so alivyoanza chuo mambo yalibadilika,,, akakutana na new experience......hii imewatokea wengi sana...unakamata aliemaliza chuo......keshakuwa used balaa.....chunguza yeye 10-12months......then vuta ndani....kamua fasta fasta.....then muanze kula life.....hiiii mengine mnajitakia,,, mwache atunzwe na wazazi wake, mnaingilia malezi......anyway pole sana, maisha lazima yasonge mbele......wako yuko mahali....na usikurupuke braza.....tulia kwanza.......
 
Pole sana kikubwa kubaliana na hali usijitenge nenda kwa washkaji zako waambie kila kitu anza upya uzuri kakwambia mapema kuliko ungepata hasara ya ndoa uko angeenda kukuchezesha sankoro sisi wanawake wengne wanatafta nafas kama hzo hawapat pole aisee
 
Mkuu pole...hawa viumbe usiingie miguu yote hata iweje...mi pia nilikua nadem kipindi nipo chuo ye alikua a level na sikuwahi kupiga game hadi alipomaliza. Ajabu hadi alipoanza chuo akawa ananiletea hizohizo za hataki tusex hadi ndoa nikajisemea huyu hanijui huyu...nikaanza kujiachia kula mizigo mingine hadi mwenyewe akatangaza kunishindwa.. mpaka leo najipongezaga kwa uamuzi ule japo ye anadai nilimuumizaga hadi akataka kufeli chuo nikamwambia 'I'm also selfish' lazima nijiangalie mimi kwanza.. nahisi ingefika huko ilikofika yakwako maana hadi ndugu na washkaj walikua wanamjua ila ilikua siri yangu kwamba sijala tunda bado tena kwa kipindi cha karibu 3 years.
 
Afadhali amekuambia mapema,mshukuru Mungu kwa yote. Fanya mambo yako,ongeza bidii kwenye biashara zako ila usije mpa nafasi tena. Mwanamke harudiwi,najua atazunguka na wavulana wa uko chuo ila akimaliza na kukutana na maisha ya mtaani atakukumbuka na kuanza kukutafuta.
Usiwe na haraka ya kuoa,endelea kuwagegeda uku ukiwa unaendelea na research ya kutafuta mke bora.
Pole sana mkuu
 
Pole sana kaka, hii ishu ya wanachuo imewakuta wengi sana, hapo unakuta kuna msela na vitz yake anamzuzua kichizi. Tafuta maisha, hii changamoto ikupe usongo wa kusaka mkwanja zaidi ili siku akikukuta hata atamani kukukimbia.
 
Back
Top Bottom