Wanawake huwa mnafikiria nini?

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
1,057
Reaction score
1,868
Katika mahusiano kuachana ni jambo la kawaida hasa unapopata mpenzi unaeona ana vigezo ulivyokuwa unavihitaji.

Lakini kwa upande wa kina dada huwa hawatumii saikolojia anapotaka kumuacha mpenzi wake.

Yeye muda wowote atakapoamua kutamka neno la kuachana anatamka bila kuzingatia anaemfikishia ujumbe atachukua uamuzi gani.

Mimi sijui huwa wanafikiia nini.
 
katika mahusiano kuachana ni jambo la kawaida hasa unapopata mpenzi unaeona ana vigezo ulivyokuwa unavihitaji
Sasa kama ana vigezo unavyovitaka unamuacha wa nini?
.lakini kwa upande wa kina dada huwa hawatumii saikolojia anapotaka kumuacha mpenzi wake.yeye muda wowote atakapoamua kutamka neno la kuachana anatamka bila kuzingatia anaemfikishia ujumbe atachukua uamuzi gani. mimi sijui huwa wanafikiia nini.
Hili umelijuaje?
 

kama kuachana ni jambo la kawaida,kinachokushangaza ni nini? Na wanaume wao huwa wanaachaje tofauti na wanawake unaowalalamikia?
 
Ukinichosha nakuacha,,,, nikipata bora zaidi yako sikutaki
 
kuna sayansi ya kuacha kumbe.... mi papuchi ikinichosha nakwambia tu ukweli, bana sisikii utamu!!!! bhasi..........
 

Hivi mnataka mtu asemeje......?.......wengine hatujui longolongo.........sikutaki........mimi na wewe imekwisha.......basi.......
Maneno gani tena zaidi ya hayo.......?
 
Ulitaka umfumanie ndo ujue hakutaki??? Ushukur kuambiwa sikutaki umepunguziwa mzigo??
 

akufukuzae hakwambii toka ila wanaume mnaacha sana subiri na nyie muachwe
 
Yaani nikitaka kukuacha lazima nikuombe ruhusa....alaaa. Kwani nyinyi huwa mnatufanyaje.
 
Yaani nikitaka kukuacha lazima nikuombe ruhusa....alaaa. Kwani nyinyi huwa mnatufanyaje.

Kwa sasa tunatakiwa kubadilika hakuna kutoa taarifa wala nini unamwambia tu nimekuchoka anza kule. Atajibeba huko mwenyewe. Kwanini uendelee kukaa na stress had ufe mwache anza maisha upya huko. Na usifikirie chochote kile.
 
akufukuzae hakwambii toka ila wanaume mnaacha sana subiri na nyie muachwe

Tumesha waacha sana hawana maana hawa. Mimi mmoja had leo haamin macho wala masikio yake. Anashangaa tu kama dudu vile, nilimwambia kama utani ila ikawa ndio hivyo. Nilimwambia tu byeeeeeeeeeee.
 
Ulitaka upewe notice ya mwezi mmoja kama mliingia mkataba? kama mwanamke mmekaa nae muda mrefu na akafikia kukutamkia hakutaki ujue alikuvumilia au ulikuwa unamyeyusha yaani hueleweki mwisho akaona ajivue gamba kabisa
 
Yupi bora? Ke anayekwambia sikutaki au mimi na wewe basi,na yule Me anayeuchuna ukipiga simu hapokei ukituma meseji hajibu akimuona ke wake anakunja uso. Bahati nzuri Ke hanaga nidhamu ya uoga anakupa hapo hapo nimepata bwana mwingine tusijuane ukikata sikio wewe kata lakini ukweli utabaki kuwa ukweli SIKUTAKI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…