Mwanangu nakuasa, huyo rafikiyo ni moja kati ya haya mawili:
1) Ana akili sana kiasi baada ya muda atakuliza, kwani hicho ni chambo na kuna siku utakuja kumeza, chambo, ndoano, chubwi na mshipi (bait, hook, line and sinker) vyote pamoja.
Kwa hili anza kumkatalia kila anachokupa na uridhike na ulicho nacho na umueleze kuwa haupo comfortable kwa hilo.
2) Ana matatizo ya akili (hii ni serious sana). Kuna mambo kama hayo nayajuwa yanatokana na mtu mwenye matatiozo ya akili (Mungu amuondoshee) na huwa anafanya kama ulivyoelezea, kama hujui unamuona ni normal tu, pengine utakuta hata hivyo vitu anavyokupa vya thamani navyo si vyake na huvichukuwa kwingine akakuletea wewe na itafika siku akachukua vyako akavipeleka kwingine.
Kwa hili, anza ku list down kila anachokuletea na uvihifadhi vizuri na usivitumie. kuna siku utakuja adhiriwa na mwenye chake akikikuta umekivaa.
Mwisho nawaasa vijana wote wenye tabia ya kuazimana vitu personal, muache kabisa, si tabia njema.