Wanawake hebu tujitahidi sasa kujishusha kwa wanaume wetu Ili kunusuru hali

Status
Not open for further replies.
dharau hipo watu tuna hustle day and night ila hakuna hata siku pole mume wangu najua jinsi gani una tabika kwajili yetu hata kua appreciate, asa na hayo yote unaletewa dharau mwanaume suruali etc yani nakutia makofi
Aise wengine tunatamani kuwa na wenza muda wote akiwa hayupo kazini yaani ni shida mstaarabu anapata janga sijui kwanini wasikutane wao kwa wao, labda akiwa mbàli na kwao itasaidia, pole sana
 
Pole mkaka huyo wako mcharuko kuna family zipo hivyo yaani kuna wengine koo zao zipo kama panya kila kitu wanafanana au uswahili mwingi endelea kumkanya anakiburi kwasababu mpo karibu na familia yake sasa sie wengine ukitaka kwenda nyumbani safari siku 2 mpaka 3 utaongea saa ngapi kwanza watanishangaa kuwasimulia badala yake utasomewa hutadhubutu tena, endelea kumkanya usimpe uhuru sana ila kama ni ukanda wa pwani hii ya bahari duu labda uhame mkoa, pole kaka
Haswa umeongea nimetamani kupatakazi haya sumbawanga hivi,jeuri kwao hapa hapa tabata.
 
una ya fanya na upati kinacho kuhusu.
Huo ukanda ni balaa kuna ndugu yangu katumbukia huko mie nilimwambia huyu ni kaka yangu akipata mwanamke mwingine mie ni wifi yangu shauri yako mie kwangu napalilia na matunda yapo yakutosha
 
Umeongea ukweli kabisaaaa! Kama mwanaume hajaamua ndio basi tena! Ndio maana unaona wanagugumia hadi uzeeni wanaume wakiamua kubadilika wanarudi kumalizia uzee.

Kuna kaka aliwahi sema yuko kwenye ndoa mwaka wa 20 na hajawahi kuchepuka wala kufikiria. Akaulizwa kawezaji wakati wenzie wanasema ni nature? Aliwajibu tu "NILIAMUA TU" maana nilitaka kuwa na familia bora yenye kiongozi bora na yenye furaha. Akaongezea kuwa ni nature ya mwanaume kupenda sex na sio kuwa na wanawake wengi, na anaipata kwa mkewe.

Akasema mwanaume anaewaza sana sex na kufikiria kuwa na wanawake wengi ni kwakuwa ameamua hivyo, na hatotafuta sababu maana ameamua.
Dah aiseee, natamani kuliongelea hili kwa upande wangu ila kuna muda nasita kuweka mifano inayonihusu ili kuepusha uzi kuwa personal! Ila ntaliongela hili siku moja.

Kuna wanaume hawachepuki, wala hawachepuki, tena hawachepuki! Inshort hawachepuki!
 
Waman
Aise wengine tunatamani kuwa na wenza muda wote akiwa hayupo kazini yaani ni shida mstaarabu anapata janga sijui kwanini wasikutane wao kwa wao, labda akiwa mbàli na kwao itasaidia, pole sana
Wamanyema sio kabisa, wana mdomo, asaivi ilivyo fikia Mie na wakwe zangu bef live na Mimi ndo nimeliwasha live baada ya kugundua live walikua wana nisengenya live ,nikawatumia kua ujumbe nimepata live
 
Thanx sis darling, I'm humbled, ubarikiwe sana, your words are full of wisdom, sijui umetokea wapi weyeee..my brother is so unlucky to be rejected by you
How sweeeeeet of you. Tunashukuru angalau bado kuna watu wanaona thamani ya their wives' s worth, ego, pride and dignity, kwa kweli ubarikiwe tu. Ingawa hiki kizazi cha nyoka watu kama wewe ndo wanaonekana fake, wamefulia, hawana mvuto eti, watakudiscourage hao, but ain't worried about you since I know you know what you NEED kwenye ndoa yako. Kwa kweli mpendane tu leo kuliko jana na shetani na malaika zake wachafu kila watakapowakaribia, waone moto tuuuu. Bado tunahitaji sana wanaume wenye imani ma choices kama zako. (Khaa leo utaombewaaa ahhaha). Love you mnooooo (teh nibanie tu)
 
naona unaenda into details, we chukua maudhui ya uzi. si kwa kulazimishwa, ila kwa kupenda mwenyewe, mfurahishe mwenzio uone kama atakuwa anachelewa kurudi na kama atakufanyia ww vibaya
Kaka kuna wanawake wanakufa huko kuzitetea ndoa zao, wanahangaika huku na kule for their ungrateful husbands, wanawake wenzetu wanateseka out there. Mwanamke wawatu mashallah kajipikilisha pishi lake mwanaume akirudi amekula baa kashiba ndiii, chakula kinamdodea. Wenzetu wanateseka jamani na hawaioni njia, Nenda kwenye dawati la jinsia utarudi hapa kuhadithia.

Si tunaopiga kelele humu, labda tunafanya hivi kwaajili yetu, labda tunafanya hivi kwaajili ya wenzetu ambao wako huko hawana pakusemea, tunawaambia NYIE waume zao msitutesee wanawake wenzetu. Tunatamani muelewe kuwa mwanamke hawezi kuwa jeuri kama kichwa cha familia kinajua ni kwanini chenyewe ni kichwa. Hivi mnakwama wapi? Wapi hapaeleweki? Wapi pagumu? Hii mbona ni hesabu rahisi kabisa 1+1=2, naona wanaume hamuelewi wala hamjitahidi kujua tatizo ninini, tunawajua mna Big egos, hebu jaribuni kubreak your egos for good ili mambo yaende sawa. Daaah naanza kuwa emotional sasa.
 
Wasalaam!

Nianze moja kwa moja kwenye mada. Ni kweli maisha ya sasa ya mahusiano na ndoa kwa ujumla hapo tete sana.

Sasa wanawake wenzangu, si vibaya tukakaa chini na kufikilia nini chanzo. Japokuwa sisi wanawake tunavumilia mengi kwenye mahusiano na ndoa kwa ujumla, lakini tuna jukumu na nguvu kubwa kunusuru mahusiano yetu na kuishi kwa amani na furaha.

Tujitahidi yafuatayo:

1. Tusiwe watu wa gubu
Wanaume wengi hawapendi mwanamke mropokaji, mjuaji, mkorofi. Tujishushe!

2. Tupende ndugu wa mume
Hili nalo ni changamoto sana. Mara nyingi sana huwa tunajisahau, tunaona ndugu wa mume ni maadui zetu. Mama mkwe si adui, hapana tuwapende. Hata wao wakiwa miiba kwetu tujishushe wataona aibu na tutaenda sawa.

3. Heshima
Hakuna kitu kizuri kama Heshima, nawaambia. Mwanaume yeyote anapenda kuheshimiwa kwani 'naturally' iko hivyo. Mwanaume ni kichwa cha nyumba, yatupasa kuwatii na kuwaheshimu.

Inapotokea Mungu kakubariki na kipato zaidi ya mume au mwenza wako, hiyo isiwe tiketi ya ujeuri, kuchelewa kurudi nyumbani wala vurugu.

4. Uaminifu
Hii ni kubwa kuliko yote. Asikudanganye mtu, uaminifu ni kitu kikubwa sana. Uaminifu unapopotea mwanaume anakuacha! Mwanaume anaweza akakuvumilia yoooote but faithfulness is one among those things men need from you!!

5. Mapenzi
Hapa naongelea mapenzi kwa ujumla jinsi unavyomhandle mpenzi au mume. Mfano:- katoka kazini, hata akiwa mbali umemuona mpokee chochote alichobeba hata gazeti. Mvue viatu, ikiwezekana mchumu kidogo(" pole mpenzi Wangu kwa kazi"). Hiyo itamfanya ajisikie vizuri sana na kuondoa stress. Hawa waume, wapenzi wetu msiwaone hivyo, wanaumiza sana kichwa kwa ajili ya future zetu na watoto hivyo tuwaenzi.

6. Mapenzi ya kitandani
Hii ilitakiwa iwe ya kwanza. Iko hivi, kitu cha kwanza mwanaume anachofuata kwa mwanamke yeyote ni hiyo starehe, mengine yanasindikiza tu. Sasa ewe mwanamke mwenzangu unayelemaa kitandani, hujibidishi, hukatiki viuno, umelala tu, unaiua ndoa yako au mahusiano yako mwenyewe.

Jitahidi uwe mchezaji hodari. Ukiwa uwanjani hapo sahau yote hakikisha anaomba maji ya kunywa. Naelewa wapo wanaume waliojaaliwa na wasiojaaliwa nikimaanisha mihogo ya Jang'ombe na vibamia. Kama ana kibamia siku hizi kuna utaalamu mwingi nasikia, kibamia kinaweza nenepa(fuatilia). Usiache kumfurahisha kitandani eti ana kibamia wala usimwonyeshe kama hakikukuni bali jitahidi hivyo hivyo huku moyoni ukiapa kumtafutia dawa ya kuinenepesha( zipo sana) uvivu tu wa kufuatilia.

7. Usafi
Asikuongopee mtu, mwanaume yeyote hapa duniani anavutiwa na mwanamke msafi kuanzia chumbani, nje ya nyumba na mwilini. Mfanye mumeo awahi kurudi nyumbani, kila wakati nukia marashi au spray au perfume. Vitu hivi siku hizi vinapatikana tena at an Affordable price.

8. Ubahili
Sawa najua, mwanaume kama kichwa cha familia ni wajibu wake atunze, ahudumie nyumba. Jamani hata kama mada zangu nyuma nimewatetea sana wanawake wenzangu lakini kutokana na hali ya maisha ya sasa, na hasa kama ewe mwanamke una kibarua chochote, tafadhari sana wekeni mezani mnachopata kwa jili ya kuboresha maisha yenu. Usimkomoe mwanaume, lenu ni moja.

9. Kumsikiliza mpenzi/mume
Kila wakati mume au mpenzi anapotaka kuongea na wewe hebu hayo masimu yazime, acha kila kitu msikilize. Imekuwa kawaida sana mume anaongea wewe upo busy unachati, hivi ndugu yangu unajipenda kweli wewe au ndo umefika tena hapindui? Ukiachwa oooh nimerogwaaaa, Wapiii umejiroga mwenyewe. Respect ni muhimu.

10. Ibada
Mwanamke mwenzangu, unapopitia magumu yooooooote kwenye ndoa au mahusiano Usimwache Mungu. Mahusiano au ndoa huzaa familia na familia hutoka kwa Mungu. Sali sana kwa imani yako.

Nakwambia ukweli, ipo nguvu kubwa katika kumtegemea Mungu. Hebu anza leo kuomba, kuhudhuria ibada na kusoma biblia mambo yote yatanyoooka.

Amen!
Ujumbe mzuri sana
 
Huyu Ndo Ulweso.Undefeated woman!!Hivi ukiwa Na moyo wa kushuka kidogo.Unapunguziwa nini.Asili.ya.Wanaume IPO hivyo.Mfano.Sasa hivi umwambie Raise ajishushe kwa Mama Samia.Ataanzaje.Siwatetei.Ila Lazima wawe juu yetu.Kwa jili ya Heshima.Ulweso.Kwanza samahani.Wewe Kabila gani.Mimi.mnyakyusa.
Hehehe eh Heloo me nilijua wewe wa mahaba zone. Mnyakyusa wa wapi jamani? Hahaa hongera sana mweeh
 
Haha!, Ulweso kanichekesha sijui kwa nini Mozambique..lol

Ile point ya mtu kuambiwa umrudie mumeo wakati yuko dakika za majeruhi, eti akafe vizuri mweh!
Yaani kafaidi huko na michepuko halafu wewe ndo umbulie mzoga!
Huyu Heloo asipoelewa hili somo kwa kweli basi tena, she's going to be taken advantage of, big time!
Ndo haya mambo tunayoyakemea. Mtu akiwa mzima haoni thamani ya mkewe, at his death bed ndo anaona thamani ya mkewe. Tooo late
 
Dah aiseee, natamani kuliongelea hili kwa upande wangu ila kuna muda nasita kuweka mifano inayonihusu ili kuepusha uzi kuwa personal! Ila ntaliongela hili siku moja.

Kuna wanaume hawachepuki, wala hawachepuki, tena hawachepuki! Inshort hawachepuki!
Jamani ongea tu, mimi napenda jamani kusikia habari nzuri nzuri za married men. Yani naweza nikasmile utadhani ndo mume wangu
 
Espy Give and take umeitoa wapi mwanamama Wewe.Kuwa.Na moyo wa kushuka Na kupondeka.Mume akiwa juu Wewe unapiga Goti Na kusema 'Mume Wangu nisamehe unamshika mguu'walahiii.Hii Ni best way ya.ku Conquer moyo wa Mume Na atajirekebisha.Atajiuliza.why.nimrkuwa.mkaliiii yy Leo kashukaa???Na Kumbuka.mabadiliko huna taratibu.Tufanye.hivyo.Naamini.we will make our Lives to be much better than that.
Shuka piga goti ukiwa na uhakika mumeo si yule mtu ambaye ukipiga goti atakubutua teke.
Kuna wanaume ambao ukikosea ukapiga goti atakunyanyua, ila kuna wale ambao ukimkosea salama yako ni kukimbia, tena nasema kimbiaaaa, ongeza mwendoooo. Kisa cha kupigwa teke la tumbo au nyonga? Hello acha kuwashauri wenzio as if wameolewa na mwanamme mmoja.
 
Shuka piga goti ukiwa na uhakika mumeo si yule mtu ambaye ukipiga goti atakubutua teke.
Kuna wanaume ambao ukikosea ukapiga goti atakunyanyua, ila kuna wale ambao ukimkosea salama yako ni kukimbia, tena nasema kimbiaaaa, ongeza mwendoooo. Kisa cha kupigwa teke la tumbo au nyonga? Hello acha kuwashauri wenzio as if wameolewa na mwanamme mmoja.


sure binti kiziwi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom