Umenikumbusha mwaka 1995 na utundu wa uvulana rijali. Ilitokea kama zali siku moja kwenye daladala nilikua nimekaa siti moja na demu mkali sana majira ya kama saa mbili usiku, hatukua tunasemeshana lakini alipokuja konda yule dada akatoa nauli kumpa konda akimwambia akate ya watu wawili yaani yake na yangu!
Kidume nikaona nyota ya jaha imenidondokea, dada akawa anashuka kituo kinachofuata na mimi japo hakikua kituo changu nikashuka nae. Sasa bana nikajidai na mimi naenda muelekeo anaoenda yeye huku naanza kumsemesha. Hatua chache tu dada akasimama ghafla akanigeukia na kuniuliza 'unakwenda wapi?kukulipia nauli imekua nongwa? Mawazo yako yanakutuma nimejitongozesha kwako, hivi wanaume mkoje?' Basi nilikula za uso za kutosha, lakini kwa vile ilikua ni usiku watu wengi hawakushtukia, mimi huyo nikageuza nikarudi kituoni kusubiri gari niendelee na safari yangu