Wanawake Acheni Roho Mbaya!!

King Kong III

Platinum Member
Joined
Oct 15, 2010
Posts
64,362
Reaction score
99,092
Nimeutoa Ujumbe Huu kwa mdada mmoja Facebook akiwashauri wanawake/wadada wenzake nikaona ni-share na nyinyi.

"Wanawake acheni roho mbaya huko majumbani house girl kwako na yeye kwao ni mtoto, pamoja na kumtuma kazi mpaka kutandika kitanda unacholala na mumeo na kukufulia underwear lakini bado unamsimanga na maneno tena unavizia muda wa chakula alichopika mwenyewe ili tu asuse asile, huo ni ulimbukeni, we mwenyewe umeokolewa na ushukuru ungeishia kuwa house girl wangu vile vile, wazazi wa mumeo umewasimanga watu wanakuangalia tu, sura bayaaaaa mashauzi tu, hiyo sura mbaya si ungei dilute na roho nzuri? na ukiendelea na roho hiyo mi nakutwanga live ukome, ndugu zako unawanenepesha kama panya buku wa mwenzio unawazushia ili wasikae ma.ni.na zako"
 
Baadhi ya Michango:

Commentor1
me wangu na wanangu! Ninampa mahitaji yake kama mwingine,anapumwa humtibia,kula anakula meza moja na sie sio kama mabosi waengine ambao hawafanyi hivyo, kama anapenda kusali awe muisilamu ama mkristo hupata haki yake ya kuabudu! Nilianza kumlipa msichana mwaka 2005 sh 40,000 lkwa sasa msichana namlipa 100,000 kutokana na kubadilika kwa hali ya maisha kwani na yeye msichana ana hitaji kujipanga na maisha! Naomba nyie wanawake wenzetu wenye roho mbaya kama wakaanga sumu. Muacha tabia hizi ni mbaya sana waone mijuso yao
1 hour ago-·-Unlike-·-2

Commentor2
duh
1 hour ago-·-Like

Commentor3
Safiiiii sana kama atakuwa kachungulia atabadirika tuu chezzea madam **** www!!! Amemnyoosha @****a
1 hour ago-·-Like

Commentor4
**** mdogo wangu umeongea kitu cha maana sana mie sielewi wanawake wengine wana mioyo gani msichana anamfanya kama mtumwa ana raha hata ya kufanya kazi,mie dada nimempata ana mwezi kwangu huko alikotoka amekaa miaka mitatu bila kulipwa mshahara kanisani alikuwa anakataliwa kwenda mpaka majirani wamefanya kumtorosha kwa jinsi alivyokuwa anateswa ,dada mwenyewe anajituma mpaka namwambia wakati mwingine pumzika basi lakini huko alikotoka kasheshe ameipata,jamani tuwapende wadada kama wadogo zetu wana uwezo wa kutulisha vitu vyovyote vibaya tuwajali,tuwathamini ni binadamu kama sie
34 minutes ago-·-Unlike-·-1

Commentor5
Wape makavu mamaa @**** yani Hg(Mercury) anafanya kazi kama punda halafu anaishia kupata buku 30 per month,Big Up @A**** aminia!!
13 minutes ago-·-Like

Commentor5
@M**** K*****o umeongea point sana kuna kipindi nshawahi sikia Hg kawalisha sumu watoto wa3 wa boss wake halafu akasepa,ni jambo zuri kuishi vizuri na hg,kuna familia flani hv nilienda yani hauwezi kumtofautisha hg na mtoto wa boss wote kama kufanya usafi,kuosha vyombo wanapiga mzigo pamoko.
9 minutes ago-·-Like
 
Last edited by a moderator:
sweetlady kweli hg ni binadamu kama sie wengine sema tu ni mgawanyo wa kazi unakuwa hivyo.
pia kumbuka kuwa wengine huwa hawabebeki.

Ila ni dhambi isiyosameheka kumnyanyasa mtoto wa mwanamke mwenzio Mamndenyi, mtoto wa watu kaletwa na shida zake then waja muongezea, watu wengine sijui hizo roho zao zikoje jamani. Kwani hg sio binadamu?
 
Last edited by a moderator:
nawaheshimu sana hawa mahg haswa linapokuja suala la kumuachia mtoto anashinda naye wakati wazazi mpo katika kusaka mapene! mwenyewe nikirudi namwamkia "dada shikamoo"...............wink!!
ila, penye ukweli aambiwe ukweli - kama kaharibu anaambiwa, na kama kafanya vizuri anapewa complement inavyostahili!

kuishi na watu kazi jamani!!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…