Wakuu salaam kwenu,
Hizi ni miongoni mwa tabia ambazo zimekuwa zikiendekezwa na baadhi ya wanaume.
1: Mwanaume unahonga hela kwa mbwembwe zote hili uonekane kidume tena wengine utakuta binti kaomba 5000 yeye kwakujifanya kidume anatoa 50,000 alafu unakuja kulia lia humu JF tukusaidie nini sasa wakati unahonga ulikuwa unakenua tu meno.
2: Kujifanya unajali sana elimu hadi kumsomesha huyo unaemuita mchumba mwisho wa siku unajinyonga wakati kila siku tunasema humu mchumba hasomeshwi, kipindi unasomesha hata wazazi wako hawajui kuwa unasomesha ukishapigwa chini unaanza kulialia, wanawake wabaya sana kasomeshe yatima na ndugu zako, siku nikikuta unajinyonga kisa umeachwa nakutia bakora za kutosha kabla sijakutoa uko juu naona imekuwa too much sasa.
3: Ma password kwenye simu mpaka unayasahau unaficha nini ujanja wa kizamani huu password mpaka kwenye contact mtoto wa kiume.
4:Kila siku story zako ni wanawake tu hunaga story tofauti na hizo hunaga story za maendeleo.
5: Kila siku unaazima geto la mshkaji wako hili binti akija ajue mambo safi yaani geto lako unapita mwezi hujafagia unajivunia geto la mshkaji wako tafuta lako mtoto wa kiume maisha hayaendi hivyo.
Hizo ni baadhi tu kama una yako pia unaruhusiwa kuweka