Wanaume wenye experience na jambo hili naomba ndio wanijibu

unajua haya mambo yanaitaji majadiliano tu na mwenzako.
sisi enzi hizo mama alikuwa anamleta mdogo wake amzalie mime watoto,yote hayo kumrizisha asitoke nje ya ndoa.
inakuwa sio poa baba kutoka nje kimya kimya kisa anatafuta mtoto.
wanawake wa siku hizi sio waelewa wanaona wao ndio wanajua kupenda sana.
mimi nona mfano mzuri tu,kuna shangazi yetu hakubaatika kupata mtoto kwenye ndoa yake,alichofanya ni kumconvice mume na mdogo wake,mdogo mtu akakubali na akamzalia mume watoto.
kuna sehemu inafikia unaweka mambo ya ndoa penbeni,eti mke mmoja for the benefit of your family.
Igeuze baba yako ndiye mgumba, halafu mama yako analalwa na baba mdogo au mkubwa ili mama asitoke nje ya ndoa kutafuta watoto
Igeuze iwe mjomba wako ni mgumba! Halafu Shangazi ashauriane naye azae na mjomba mdogo ili kuficha aibu ya mjomba asiyezaa!
Iweke pia kwa namna hii wewe ni mgumba mke wako ashauriane na wewe alale na kaka yako ili mpate watoto! Washambulie wanawake iwapo jamii nzima imekubali kwamba mke au mume asiyezaa ni jambo la heri kutafuta replacement ili watoto wapatikane, halafu wanawake wakatae ndo uwanyoshee vidole! Otherwise huna right hiyo!
 
It goes both ways bana maana wenye matatizo sio wanawake pekee....tatizo ni rahisi kwa mwanaume kugundulika amechepuka maana yeye habebi mimba....ila kiafrika mama akijua mzee ndo mwenye matatizo kuna akina mama walio seniro kwake wanamshauri cha kufanya jamaa anapata watoto japo sio wake biologically.
 
Sijui ni uzoefu wa aina gani unauhitaji kwenye hili lakini mi naona hili linaweza kujibiwa na yoyote yule anaethamini ubinadamu

Kimsingi hakuna anaeweza kuwa na mapenzi na watu wawili tofauti
Mapenzi huenda na kuheshimiana pia
Huwezu kudai una mapenzi na mtu halafu una mwanamke mwingine huo ni uongo

Suala la kupata mtoto ni majaaliwa na mtu yoyote anaefikiri kidogo tu anaweza kuliona hilo
Kama mmekwenda hospital na kuangalia na mkaambiwa hakuna mwenye matatizo ni kwanini unamuadhibu mwenzako kwa adhabu ya kibazazi kama hii?
Kwanini usimuache tu akajua moja?

Kama wewe mtoa mada ni mwanamke tambua hapo huyo jamaa hakuwa anajua hata upendo ni kitu gani wakati anakuona na hajui upendo ni kitu gani

Wakati anakuoa alikuwa anakuona kama mashine ya kufyatua watoto na sio kweli kuwa alikupenda kama alivyokuwa anakuambia

Kama anakupenda ni kwanini afanye jambo la hovyo kama hilo?

Mtoto ni kitu gani hadi uamue kumfanyia mwenzako unyama wa aina hii?

Huwa sipendi sana hii .......!!!!!!

Umekosea kitu kimoja
U can love two people but you can't be inluv with two people
 
Duuuuuu umeongea point tupu,kuna umuhimu wa kubebeanaizigo ma hpo ndipo upndo wa kweli umapoonekana
 
kama mume mkewe hajabahatika kumzalia mtoto. lakini mume anaye mwanamke nje ya ndoa anamzalia watoto halafu mwanaume huyo anaendelea kumwambia mkewe eti bado anampenda sana, je ni kweli anampenda mkewe? Naomba wajibu wanaume ambao hili jambo limewatokea tafadhali.

Kwa maelezo yako na swali ulilouliza: Jibu ni kwamba KWELI ANAMPENDA MKEWE kama mwenyewe atamkavyo na alichofuata kwa huyo mwanamke wa nje ni hao watoto tu ambao mkewe hajabahatika, akibahatika kuzaa tu ujue huyo wa nje ndiyo kwishney uhusiano, wala haihitaji experience kukujibu.
 
Inawezekana sana kuwa anakupenda sana kwani asipokupenda atakuacha. Sote tu binaadamu na tunaongozwa na mazingira na hamu ya jambo au kitu ni moja ya mazingira hayo.
Hata hivyo ili kuondowa kuonekana udanganyifu ndipo mungu ameweka ndowa za zaidi ya mke mmoja (waislamu). kukosekana kwa uwazi ndio kunasababisha kutofahamiana na matatizo mengi ya kuzaa watoto nje ya ndowa!
Yuko mtu mmoja, tena ni shemeji yangu, alikuwa na the same problem na mke wake na kuamua kutafuta watoto nje ya ndoa. Aliwapata. Baada ya hapo mke wake aliamua kuondoka kwa sababu aliona kitengo kilichofanywa na mumewe si sahihi. Mke alipotoka tu kwa mumewe akapata mwanaume mwingine na ndani ya miezi Sita akawa mjamzito. Cha kushangaza sasa, Yule shemeji yangu alikuja kugundua kuwa wale watoto wote watatu si wake. Issue hapa ilikuwa baada ya mke wa nje kugundua kuwa tatizo la Yule bwana ni watoto, aliamua kumchota kwa kumchomekea watoto wasio wake. Shemeji yangu hadi Leo hajaweza kupata mtoto. Wanaume tuwe waangalifu sana. Samahani shemeji Kama nimekugusa
 
Duuuuuu umeongea point tupu,kuna umuhimu wa kubebeanaizigo ma hpo ndipo upndo wa kweli umapoonekana
Pia yuko bwana mmoja tena ni maarufu sana hapa bongo. Alikataa na mke wake for more than 15years bila mtoto. Siku alipoamua kutafuta mtoto nje ya ndoa, mwanamke wa nje alipopata mimba na mke naye akapata mimba almost kipindi hicho hicho. Mke wa ndoa akatangulia kuzaa na after a week mke wa nje akazaa, wote watoto wa kike
 
Mi siku zote sipendi kuona kuwa cheating ni kinyume cha loving.
Sio sahihi kutumia kigezo cha cheating kupima upendo.
Sio watu wote wanaochiti hawawapendi wenzi wao...
Sio watu wote wasiochiti wanawapenda wenzi wao...
Sio wote waliozaa nje ya ndoa walifanya hivyo kwa sababu wake zao hawazai au hawazai idadi ya kutosha ya watoto...
Sio wote wasio na watoto na wakazaa nje ya ndoa walidhamiria kuzaa nje ya ndoa
Sio wote wasio na watoto na hawajazaa nje ya ndoa hawatoki nje ya ndoa

Hitimisho: kutembea nje ya ndoa kutakakopelekea kuzaa au kutozaa nje ya ndoa sio kigezo cha kukosa upendo kwa mwenzi.
Wapo wasiotembea nje ya ndoa and yet hawana hata chembe ya upendo kwa wenzi wao
Wapo wanaotembea nje ya ndoa and yet wana mapenzi tele kwa wenzi wao...
 
Yuko mtu mmoja, tena ni shemeji yangu, alikuwa na the same problem na mke wake na kuamua kutafuta watoto nje ya ndoa. Aliwapata. Baada ya hapo mke wake aliamua kuondoka kwa sababu aliona kitengo kilichofanywa na mumewe si sahihi. Mke alipotoka tu kwa mumewe akapata mwanaume mwingine na ndani ya miezi Sita akawa mjamzito. Cha kushangaza sasa, Yule shemeji yangu alikuja kugundua kuwa wale watoto wote watatu si wake. Issue hapa ilikuwa baada ya mke wa nje kugundua kuwa tatizo la Yule bwana ni watoto, aliamua kumchota kwa kumchomekea watoto wasio wake. Shemeji yangu hadi Leo hajaweza kupata mtoto. Wanaume tuwe waangalifu sana. Samahani shemeji Kama nimekugusa

Hili la kubambikiziwa huweza kufanyika hata ndani ya ndowa isipokuwa tuna assume kuwa kila muhusika atakuwa muadilifu kwa mwenzake ndani ya duara.
 
Mbona unakwepa swali la msingi? Wewe Kaizer uko tayari mke wako wewe wa ndoa azae na mwanaume mwingine ikiwa wewe sperms zako haziwezi kuzalisha? Naona unakwepa mara oooh mila zakiafrika, mara oooh zamani kijijini oooh kuchapiwa siri ya ndani!!!!!!!!!....... jibu swali Mkuu!

Sorry Cyan6 sikuona post hii.mapema..ukisoma my contributions kwen hii sredi utajua nasimamia wapi...kwa uzoefu huu huwa hatujibu ndio au hapana tunajibu kwa muktadha...wasome na wengine pia
 
Last edited by a moderator:
Mi siku zote sipendi kuona kuwa cheating ni kinyume cha loving.
Sio sahihi kutumia kigezo cha cheating kupima upendo.
Sio watu wote wanaochiti hawawapendi wenzi wao...
Sio watu wote wasiochiti wanawapenda wenzi wao...
Sio wote waliozaa nje ya ndoa walifanya hivyo kwa sababu wake zao hawazai au hawazai idadi ya kutosha ya watoto...
Sio wote wasio na watoto na wakazaa nje ya ndoa walidhamiria kuzaa nje ya ndoa
Sio wote wasio na watoto na hawajazaa nje ya ndoa hawatoki nje ya ndoa

Hitimisho: kutembea nje ya ndoa kutakakopelekea kuzaa au kutozaa nje ya ndoa sio kigezo cha kukosa upendo kwa mwenzi.
Wapo wasiotembea nje ya ndoa and yet hawana hata chembe ya upendo kwa wenzi wao
Wapo wanaotembea nje ya ndoa and yet wana mapenzi tele kwa wenzi wao...

Duh, kweli ni great thinker, cheers!
 
Labda anakupenda, na unaweza kutambua hilo wewe mwenyewe. ukweli ni kwamba hakuna mtu miongoni mwa wana jukwaa anayeweza kutoa jibu la fumbo hili. wanajukwaa watakupa maoni na ushauri lakini jibu utalipata wewe baada ya kuchunguza kwa makini mapenzi ya mumeo kwako katika kipindi hichi. Ushauri: soma bible.
 
ndiya anampenda sana,yule alienae nje ni wa kuzalisha watoto tu na aliepo ndan ni wa mapenzi ya dhati!!
 
Igeuze baba yako ndiye mgumba, halafu mama yako analalwa na baba mdogo au mkubwa ili mama asitoke nje ya ndoa kutafuta watoto
Igeuze iwe mjomba wako ni mgumba! Halafu Shangazi ashauriane naye azae na mjomba mdogo ili kuficha aibu ya mjomba asiyezaa!
Iweke pia kwa namna hii wewe ni mgumba mke wako ashauriane na wewe alale na kaka yako ili mpate watoto! Washambulie wanawake iwapo jamii nzima imekubali kwamba mke au mume asiyezaa ni jambo la heri kutafuta replacement ili watoto wapatikane, halafu wanawake wakatae ndo uwanyoshee vidole! Otherwise huna right hiyo!

nazini hujanielewa vizuri,hayo uliyo ya assume yapo ma yanafanyika tu kwenye familia nyingi tu.
cha msingi ni kukaa kama wana familia na kulizungumuzia swala hili,nimekupa mfano mmoja,,shangaz yangu alikuwa haku baatika kuwa na kizazi,baada ya kupima na kujadiliana na mume wake wakaamua mume aowe mke wa pili,ambaye ni mdogo wa shangazi.
so wewe kama wewe kipi bora kwako mume ai mke acheat nje akuletee watoto au ndoa uvunjike? enzi za mababu zetu kama baba alikuwa mgumba then mdogo mtu anazaa na shemeji yake kuifichia siri familia,kama mama hana kizazi then anamleta mdogo wake aolewe na mume familia ibaki intact .
tatizo la kizazi hiki especially sisi wakristo ni kwamba tumekumbatia maandiko sana,eti mke mmoja,sasa kama mke hazai nimfukuze au nife bila mtoto eti ndoa imenifunga nooo,i strongly oppose that.
i cant cheat but ntaoa mwanamke mwingine kwa maelewano na majadiliano ya kina kati ya mu wife and entire family.
kama mimi ndio mgumba then its up to my wife kama anaweza kutembea na ndugu yangu only on dangerous days bila mimi kujua ili apate mimba anizalie watoto.if she cant then let her go,but i cant accept mtoto from ukoo mwingine.
 
kama mume mkewe hajabahatika kumzalia mtoto. lakini mume anaye mwanamke nje ya ndoa anamzalia watoto halafu mwanaume huyo anaendelea kumwambia mkewe eti bado anampenda sana, je ni kweli anampenda mkewe? Naomba wajibu wanaume ambao hili jambo limewatokea tafadhali.
Hivi kumbe nalo hili linahitaji wenye experience?
 
wenye experience na jambo hili, maana yangu ni kuwa mtu ambaye amewahi au yuko katika hali kama hii inayonipata anaweza kuielezea vizuri zaidi ya mtu ambaye mambo yake kuhusu ndoa na uzazi yako poa.
 
Back
Top Bottom