Wanaume wanaooa au wanaopenda kuoa wanawake wa kijijini ndo waharibifu wakubwa

inawahusu hata nyinyi wa kijijini, msikabidhi dada zenu kwa mabazazi wa mjini
Haswaaaa.... Na pia Kama mmewakabidhi Basi waambieni kabisa hao binti zenu kama wanateseka waseme wasiogope kusema
 
Bora na huyo anayejua njia hata akatoroka.... Huyu hata stand ilipo hajui ..... Yaan kanaishia dukani tuu sokoni mwanaume ndo anaenda yeye
 
Yaani wakiona MTU anatoka mjini ameulamba kila MTU anatabasamu na kusema mambo yameiva kumbe wanakuwa wameficha mambo mengi
Saaana..... Hapo wazazi wake wanajua mtoto wao huku mjini anakula good time kumbe Cha Moto anakiona....
Na uyu mwanaume sio kwamba hata Ni Mambo Safi Sana Wala mfano mzuri juzi hapa kwenye sikukuu ya idi msichana Dada ake alimwambia wachange ela elfu kumi kumi watume nyumbani kwao kwa ajili ya sikukuu msichana akawa anaogopa kumuambia mme wake kwamba anaomba elfu kumi ya kumpa mzazi wake kijijin.....
Na hapo alikua anaongea na cm nipo jikoni napika Cha jioni nikasikia maongezi nikajiambia elfu tuuu jamanii mmhh
....
 
Mimi uyu binti natamani awaambie wazazi wake huko kijijin kweli kabisaa
 
Mpaka nimelia aisee inaumiza sana

Wanaume mkituoa wadogo mjue na kutulea jamani khaaa!!!

Anamtengenezea tatizo baya mno la kisaikolojia huyo binti, saiv akipigwa hanuni sababu bado mchanga lakini siku akichoka huyo mwanaume ajiandae kwa rangi zote atakazopewa

Hebu msaidie kabla hajaambukizwa ukimwi huyo binti

Hizo ndoa za utotoni na za wazazi hizi ni zigo la misumari kichwani
 
Anamuonea kwa vile mtoto jamani, lakini sio vizuri hata kwa bed nahisi hakaandaliwi kanashtukia mashine inazama tu duh.
Hayo Ni ya ndani siwezi kujua ila Kuna Yale yanayo jionesha kabisa yaani inatia huzuni
 
Si wote bhana, usituaribie wengine mimi ndiyo kwanza naenda kuchumbia lushoto,
Hizi za mjini na wameshajua utamu wa umbea wa instagram huwa zinakuwa ngumu kumeza!
Na huyu ametokea vijiji vya huko huko TANGA ila sio lushoto...... Kenyewe kanasema kalikua kanafanya kazi za ndani wazazi wake wakakaita ili kaje kaolewe
 
Sasa na record ushahidi gani jamaniiii.....

Mungu amsaidie tuu maskini
 
Yuko mafunzoni huyo binti atakuwa binti wa kikurya amekuwa huku akishuhudia vipigo kwa ***** sasa kwa nini yeye asipigwe,
Mhimu kama yuko hapa town fanya juu chini nipate namba yake ili tumzibue masikio,baada ya hapo mmewe lazima ataomba poor
Wala sio mkurya.... Alaf Nia yangu sio azibuliwe masikio Nia yangu Ni asiteseke kwa ndoa yake
 
Ila Kuna mtu kanipa ushauri mzuri Sana pm nitaufanyia kazi..... Mungu akubariki this may work hakika.... Leo jioni nikirudi kutoka kwa shughuli zangu ntafanya Kama ulivyoniagiza Mungu akubariki aisee mkuu
 
Acha apigwe tu akome kuparamia mjini
 
Kila la heri utuletee mrejesho wa yatakayojiri
Ila Kuna mtu kanipa ushauri mzuri Sana pm nitaufanyia kazi..... Mungu akubariki this may work hakika.... Leo jioni nikirudi kutoka kwa shughuli zangu ntafanya Kama ulivyoniagiza Mungu akubariki aisee mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…