Wanaume wanaooa au wanaopenda kuoa wanawake wa kijijini ndo waharibifu wakubwa

Qurie

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
3,177
2,000
Wewe jirani weweeee may thunder strike you. Shenzi kabisaaa.

Ipo hivi hapa nnapokaa nna jirani yangu Ni mwanaume alioa mwezi uliopita zile ndoa za ramadhani zile... Sasa kilichonifanya nianzishe Uzi Ni jinsi anavo mtreat mkewe yaani sio sawa kabisa , kwanza binti wa watu ana miaka kumi na Tisa tuu kametolewa kijijini kuletwa mjini Kuja kuteseka kabinti kawatu kanapigwa na ndo kwanza ndoa Haina hata miezi mitatu.

Mwanaume Ni Malaya huyuuu kila nikirudi kutoka kwenye mizunguko yangu namfuma maeneo ya hatari ila najikausha tuu Leo nimeshindea kuvumilia kwakweli maana leo tena kampiga vibao mtoto wa watu kwa kosa la kijinga kabisa.

Swali langu kwa wanaume wa huku jf wenye tabia Kama hi kwanini ukaoe mtoto wa watu mdogo anaesalimia kwa kupiga goti uje umtese? SI Bora utafute gume gume za huku mjini tuuu.

Wito kwa wazazi na wale wenye ndugu zao vijijin msiozeshe mabinti zenu wadogo kwa mwanaume ambae hajajuana nae yaan amekuja tuu kijijin kwa ajil ya kutaftiwa mke tuuu wanakuja kuteseka huku jamani.

Uyu msichana anapenda kajifunika funika kumbe anaficha alama za alipopigwa

Wewe mwanaume wewe naomba Mungu uwe tuu jf uje usome hapa ili angalau uache ujirekebishe
 
Qurie

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
3,177
2,000
Mfuatilie binti huyo kwa karibu ukiona anazidi kudhalilishwa mlipue huyo punguani.
Yaan sijui hata nianzie wapi ilaa dawa ya uyu mwanaume inachemka.....
Kuna siku nikamwambia uyu binti kwanini usiwaambie nyumbani kuwa unapigwa???
Hapo alikua hajui kama najua kanapigwaga akaniambia simu yangu Haina ela nikamwambia nakupa ela ya vocha uweke uwaambie ndugu zako ila hakufanya hivyo nadhani anaogopa..... Uyu mwanaume anaweza akaja mchana kula chakula akikuta chakula bado hakijaiva anampiga mtoto wa watu hata kupika vizur hajui so siku akipika vyakula vibichi anapigwa pia yaani
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
100,324
2,000
Sad 😢

Miaka 19 ni mdogo sana.
Pengine hata mwanaume anaongea na vicheche wake mbele yake na hakafanyi kitu.
Huyo mwanaume angenioa mimi ningeshamkata naniii zake nichemshe supu. Nimechukia sana
Na huyo mwanaume Ni kichecheeee yaan uyu mpumbavu uyuu alishaishi na mwanamke wakashindwana Sasa cjui ndo anamalizia hasira kwa msichana wa watu..... Na hakaruhusiwi kutoka kwenda popote pale Yale haka katoto hata sokoni hakajui Ni wapi kila kitu kanaletewa kanaishia tuu dukani maskini
 
Qurie

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
3,177
2,000
Msaidie huyo binti hajui aanzie wapi kujikwamua kwenye hilo tatizo linalo mpata
Yaan sijui hata nimsaidiaje.... Nlimwambia awaambie nyumbani kwao akaniambia cm yake Haina ela nikampa ela akaweke vocha sijui hata Kama alisema......

Kenyewe kanasema nyumbani kwao wamemuambia ndoa Ni kuvumilia.... Aliniambia ivyo mtoto mwenzie ambao wanashinda wote..... Alaf Sasa saa zingine kanapigwa alaf kanatoka nje kanacheka na kuongea hata hakanuni jamani..... Nyie wanaume nyieee na nyinyi mtazaa tuu watoto wa kike
 
Born2xhine

JF-Expert Member
Aug 6, 2014
787
1,000

Sasa hapo muhanga inaonekana anavumilia kutokana na ideology za kizamani kuwa ndoa ni uvumilivu hata kama hamna furaha ..ndio isipokuwa na furaha hakuna maana ya uvumilivu..na inaonekana hata kama akitaka kusaidiwa huyo binti hawezi kutoa ushirikiano sababu ya hizo ideology za uvumilivu ..inakua ngumu kumpa msaada
 
Ndo hivyo maana anatoka kupigwa huko analiaaa then anatoka nje anaongea anacheka.... Nikamwambia Kuna baadhi ya vitu usione aibu kusema sema usaidike yaan hata kumpelekea uyu mpuuz polic tuu huenda angeacha kumpiga..... Leo amesahau kuchoma dawa ya mbu.... Narudia Tena dawa ya mbu ile ya kuchoma sijui Ni sh Mia tano sijui mwanaume akampiga mpaka huku nilipo nikasikia kakisema ( huku kanalia) Aya naendaa then aka kaa kama dakika tano akatoka nje kufata mkaa kwenye jiko Kuna mtu akamuongelesha akajibu as if hamna baya lililo mpata huko ndani nika shindwa kumuita.....
Roho inaniumaa namuona Kama mdogo wangu kabisa
 
Kizzy Wizzy

JF-Expert Member
Aug 2, 2013
3,116
2,000
Na huyo mwanaume Ni kichecheeee yaan uyu mpumbavu uyuu alishaishi na mwanamke wakashindwana Sasa cjui ndo anamalizia hasira kwa msichana wa watu..... Na hakaruhusiwi kutoka kwenda popote pale Yale haka katoto hata sokoni hakajui Ni wapi kila kitu kanaletewa kanaishia tuu dukani maskini
Toa taarifa kituo cha police

Huo anaoufanya ni unyanyasaji

Fanya haraka kabla hajamwambukiza Ukimwi mtoto wa watu.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
100,324
2,000
Sie wote tuko hivi Qurie ni baadhi tu wasiojitambua. Utasikia hawa wanawake waliosoma wanajifanya wanajua sana. Lengo lao ni kuwa na wake kama huyu wawanyase watakavyo kwa kuwa hawajui haki zao. Si ajabu kaishia la saba.

Sasa mwambie kama akijaaliwa kuwa na binti kwamba asiende shule akae nyumbani tu hadi atakapoolewa ili akawe mke mwema kwa mume wake badala ya kwenda shule maana atajifanya kujua ndani ya ndoa uone atakavyo NG’AKA.

Bado tuna safari ndefu sana ya watu kuangalia mbali badala ya kuangalia umbali wa pua na mdomo.

Yaan sijui hata nimsaidiaje.... Nlimwambia awaambie nyumbani kwao akaniambia cm yake Haina ela nikampa ela akaweke vocha sijui hata Kama alisema......

Kenyewe kanasema nyumbani kwao wamemuambia ndoa Ni kuvumilia.... Aliniambia ivyo mtoto mwenzie ambao wanashinda wote..... Alaf Sasa saa zingine kanapigwa alaf kanatoka nje kanacheka na kuongea hata hakanuni jamani..... Nyie wanaume nyieee na nyinyi mtazaa tuu watoto wa kike
 
Encryption

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
590
1,000
Wewe jirani weweeee may thunder strike you.... Shenzi kabisaaa.....

Ipo ivi hapa nnapokaa nna jirani yangu Ni mwanaume alioa mwezi uliopita zile ndoa za ramadhani zile... Sasa kilichonifanya nianzishe Uzi Ni jinsi anavo mtreat mkewe yaan sio sawa kabisa , kwanza binti wa watu ana miaka kumi na Tisa tuu kametolewa kijijini kuletwa mjini Kuja kuteseka kabinti kawatu kanapigwa na ndo kwanza ndoa Haina hata miezi mitatu.... Mwanaume Ni Malaya huyuuu kila nikirudi kutoka kwenye mizunguko yangu namfuma maeneo ya hatari ila najikausha tuu Leo nimeshindea kuvumilia kwakweli maana leo tena kampiga vibao mtoto wa watu kwa kosa la kijinga kabisa.....

Swali langu kwa wanaume wa huku jf wenye tabia Kama hi kwanini ukaoe mtoto wa watu mdogo anaesalimia kwa kupiga goti uje umtese???? SI Bora utafute gume gume za huku mjini tuuu.....

Wito kwa wazazi na wale wenye ndugu zao vijijin msiozeshe mabinti zenu wadogo kwa mwanaume ambae hajajuana nae yaan amekuja tuu kijijin kwa ajil ya kutaftiwa mke tuuu wanakuja kuteseka huku jamani...

Uyu msichana anapenda kajifunika funika kumbe anaficha alama za alipopigwa
Wewe mwanaume wewe naomba Mungu uwe tuu jf uje usome hapa ili angalau uache ujirekebishe
Samahani Mkuu,
Kwani mtoto anaanza na miaka mingapi?
Mimi nasikiaga kwa watu wakisema kuwa ndoa ni maridhiano ya watu wawili. Vipi ulijaribu kufuatilia kabila la jirani yako? Maana kunakabila linaruhusu mwanamke kupigwa na kwa kufanya hivyo inadhihirisha upendo wa mume kwa mke wake. Au ni stress za kuolewa ndy zinapelekea baadhi ya watu kufuatilia maisha ya watu wengine?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom