Wanaume wa sasa hawana tofauti na Wanawake

Siku moja nikiwa na safiri kuelekea Dar esalam kutoka mbeya nikiwa kwenye kituo cha mabasi, kulikuwa na wazee wawili, walikuwa na maada ambayo walinifanya niwadadisi kwa undani zaidi ,wakidai kuwa vijana wa kiume wasasa hawana tofauti na mwanamke isipokuwa maumbile tu ndiyo yanawatenganisha mengine yote nisawa ,walitaja sababu 1. Vijana hawana ujasili. Wanaogopa kumukabili mwanamke 2. Kwenye ndoa mwanamke amekuwa na amri sawa na mwanaume 3. Waoga hata kumtokea mwanamke 4.wakikutanisha macho na mwanamke huwa wakwanza kuinamishwa kichwa chini 5. Akimtongoza mwanamke yeye ndiye wakuuma uma nyasi na kushika ukuta 6. Walio kwenye ndoa humpikia mwanamke wakidai haki sawa 7.huosha vyombo 8.mwendo wamelegea legea kama wanawake 9. Huongea kwa kurembua rembua 10.HAWANA NGUVU kila siku kwa waganga kutafuta nguvu za kiume 11.wanakubali kuhongwa wakiita zali la metali

Apo kwenye nyekundu kama wewe unaona jambo hilo ni la wanawake tu!! kaka umekula hasara!!! Mimi Ni mwanaume tena mwanaume wa haswa, na jikoni huwa naingia bila kufikiria jinsia yangu. Huwa napika mkuu na sio kwa wanawake tu hata madume wanzangu wakija kunitembelea huwa napika tena wengine kwa sababu mawazo yetu yapo sawa huwa wanaingia jikoni na sio kupiga story tu bali huniunga mkono ili mambo yaishe chap chap!! Tunapika na tunakula na kina dada ambao wao wakati wa upishi jikoni huwa tunawapiga marufuku. Upo hapo!? JE mimi unaniweka kundi gani??
 
Inawezekana kwa sehemu. Vijana wengi wa siku hizi wameendekeza starehe kuliko kazi. Hili imewaponza na kujikuta wakifanya hata yale wasipaswa kuyafanya ili mradi waweze kujikimu.
Wanatia aibu na wanapaswa kubadilika!
 
Apo kwenye nyekundu kama wewe unaona jambo hilo ni la wanawake tu!! kaka umekula hasara!!! Mimi Ni mwanaume tena mwanaume wa haswa, na jikoni huwa naingia bila kufikiria jinsia yangu. Huwa napika mkuu na sio kwa wanawake tu hata madume wanzangu wakija kunitembelea huwa napika tena wengine kwa sababu mawazo yetu yapo sawa huwa wanaingia jikoni na sio kupiga story tu bali huniunga mkono ili mambo yaishe chap chap!! Tunapika na tunakula na kina dada ambao wao wakati wa upishi jikoni huwa tunawapiga marufuku. Upo hapo!? JE mimi unaniweka kundi gani??

kwa mujibu wa wale wazee wewe ni mwanamke.
 
Asante kwa taarifa. Ingekuwa ngumu sana kuipata kwa mtu mwingine kwa kuwa wewe ni mmoja kati ya wanawake wachache waliofanya juhudi ya kuishi na wanaume wengi mpk ukazijua tabia za wanaume wengi.

Ila navyofahamu mimi, wanaume wa ajabu waliiishi zamani kidogo iliyopita. Huko vijijini wanaume hawaendi hata kulima, wake zao ndio hulima na kulea familia. Haya ukienda hata TGNP utayapata kwani ni kesi nyingi za ukatili zililala kwenye kraiteria hii

weweee acha ungese unaongea ongea tu.kuna watu akili zao ziko mkiani mmojawapo oyu!!!
mia!!
 
Kwani haki sawa mnazotaka ni zipi jama?
au ni kwenye raha tu ndo mnataka haki sawa ila kwenye majukumu awajibike baba tu?
Ndo maana siku hizi ili uolewe inabidi uwe na kazi,tena kazi ya maana kweli.

Mkiwezeshwa mnaweza,tume wawezesha sana somesheni watoto na lisheni familia hahaha.

kwanza hiyo ID yako du!!! you must be comedian lol!
 
naomba kusikia toka kwa mtu ambaye alikuwa kijana miaka ya 60, arafu akafa then akafufuka na kuwa kijana tena miaka ya 2005 sijui yupo????
 
Siku moja nikiwa na safiri kuelekea Dar esalam kutoka mbeya nikiwa kwenye kituo cha mabasi, kulikuwa na wazee wawili, walikuwa na maada ambayo walinifanya niwadadisi kwa undani zaidi ,wakidai kuwa vijana wa kiume wasasa hawana tofauti na mwanamke isipokuwa maumbile tu ndiyo yanawatenganisha mengine yote nisawa ,walitaja sababu 1. Vijana hawana ujasili. Wanaogopa kumukabili mwanamke 2. Kwenye ndoa mwanamke amekuwa na amri sawa na mwanaume 3. Waoga hata kumtokea mwanamke 4.wakikutanisha macho na mwanamke huwa wakwanza kuinamishwa kichwa chini 5. Akimtongoza mwanamke yeye ndiye wakuuma uma nyasi na kushika ukuta 6. Walio kwenye ndoa humpikia mwanamke wakidai haki sawa 7.huosha vyombo 8.mwendo wamelegea legea kama wanawake 9. Huongea kwa kurembua rembua 10.HAWANA NGUVU kila siku kwa waganga kutafuta nguvu za kiume 11.wanakubali kuhongwa wakiita zali la metali

Wazee wana haki ya kusema na kulaumu kama hapo juu kwa sababu nyakati zao mfumo dume ulikuwa ndo top fashion.Ndo wazee hawahawa wakiona mume na mkewe wanaelewana wanasema huyo mwanamume kakaliwa na mkewe. Lakini kuna kaukweli kuhusu vijana wa kisasa wanaosuka nywele, kuvaa hereni, kutumia dawa za nywele, kuvaa kata k's nk. Kijana kama huyu akichumbia na kuoa halafu wakaelewana na mkewe, ni kinyaa kitupu mbele ya wazee.
 
1. 'Wamukabili' mwanamke kwani mwanamke ni adui yao?
2. Kua na maelewano/majadiliano ndani ya nyumba kuna ubaya gani? Maana kinachowauma ni wazo la mwanamke kuweza kushauri/sisitiza kitu ambacho hata mwanaume anaona ndicho sahihi na sio zaidi ya hapo.
3. Wanafikia vipi kuoa? Na aliyekwambia kumtokea mwanamke ni ujasiri nani? Ujasiri onyesha kwenye kupambana na simba sio kutongoza.
4. Kumkodolea mtu macho kunamhakikishia vipi mtu uanaume wake umekamilika?
5. Hao unaowaongelea ni wavulana au tuseme watoto wa kiume na sio wanaume ndio wanaotongoza uchochoroni kwenye majani na kuta.
6.Kumpikia mke sio haki sawa, ni mapenzi na maelewano.
7. Wakati wanapokua single na wanaosha vyombo/au wale wanaofanya kazi mahotelini uanaume wao hua unachukuliwa na sabuni ehhh?
8. Unataka watembee kama wanajeshi wako jeshini?
9. Mtu anaongeaje kwa kurembua? Sauti nayo hua inarembua?
10. Wanawake nao wakipewa nguvu za kiume watakua wanaume? Wanaopata hayo matatizo kutokana na magonjwa kuumwa kwao nako ni kwasababu sio wanaume ehhh?
11. Hamna aliyezaliwa anacho. . . kika mtu anapewa kuendana na anachotoa.

Lizzy asante sana, umemaliza kutoa majibu yale niliotaka kumjibu mtoa mada awapelekee hao wazee wake wa enzi hizo. Sasa hivi ni digital mambo ya analog yamepitwa na wakati.
 
Back
Top Bottom