Wanaume wa JF sio wakweli hata kidogo

Humu Jamii Forums kila kitu hakina uhalisia uongo, utapeli kujifanya maisha ya juu. Nakumbuka mwaka 2010 kuelekea 2011 kulikuwa na mpango wa kuanzisha Jamii Empowerment Saccos yaani kuna mtu alikuwa ni mstaarabu sana na alikuwa ni kivutio kwa jukwaa la MMU na katika huo mchakato yeye alikuwa kama Excutive Secretary akaniazima laki 3. Nilimdai mpaka nilichoka na akaamua kuni block na humu JF simuoni tena.pole kwa yaliyokukuta humu JF watu wanaiwanaishi maisha ya kuigiza.
Umenena ukweli mtupu hapa JF usanii mwingi ndo unatoboa
Mfano mimi nikitumia ID yangu hii ambayo nimejiweka wazi kwamba mimi ni muuza majeneza ila cha ajabu kila mrembo nkimtokea anaishia kunikataa !
Lakini nikilogin kwa id yangu fake ambayo imejaa posti za uongo mtupu kuhusu biashara za magari na michongo ya America nikimfuata mdada huyo huyo inbox nikaomba mzigo huwa hawachomoi (wanaamini nina hela sana kutokana na posti zangu za hiyo id)
Sasa kwa hali hiyo kwa nn tusiwatafune kwa uongo?
 
Back
Top Bottom